Kamati ya Lowassa yachanganya mambo


Jibu la swali lako ni rahisi sana. Hawana mamlaka hiyo na ushawishi pekee ni fedha walizopewa. Timing ya safari yao na choice ya nchi ya Morocco haikuwa ya bahati mbaya. Hawa jamaa wamethibitisha kwamba hawan integrity na nitashangaa kama Serikali haitawashukia ku-denounce upuuzi huu na hata kupendekeza Bunge liwawajibishe kwa kuiuza nchi kwa vipande thelathini vya fedha.
 

This is absurdity of the highest order na sas tunahesabu masaa tu kuujua msimamo wa kweli wa Tanzania na sasa tutajua nani aliyelamba fedha katika hili, kama wanavyolamba katika hayo mengine.
 

Mpaka nahisi kwamba maradhi yamekula akili mpaka anashindwa kujua anachokifanya, au kama anakijua, basi hajui kwamba ni kibaya. Huwezi kujilipua hivi huku ukijua kwamba huko mbele utaaibika kama kichwa chako kiko timamu! Mfuatilieni huyu bwana vizuri. Has he recovered?
 

Hii dhana ya kuwagonganisha mimi siioni kwa sababu msimamo wa Tanzania ambao Rais aliurejea mwaka jana haujabadilika na ndiyo anaousimamia Membe. Sasa kama Lowassa, ambaye anajijua kwamba hana mamlaka wala madaraka ya kulitolea msimamo hili. Huyu bwana anajiona yeye ni serikali na kiu iliyopitiliza ya fedha na kujikweza vimemfikisha hapo. Hii ni misimamo ambayo aisngepaswa kuitoa hata alipokuwa waziri mkuu.
 

Uko sahihi kabisa. Kimsingi Morocco ilijiondoa OAU kwa sababu ya msimamo wa Afrika kuhusu Morocco na Sahara Magharibi. Hakuna kilichobadilika. Ndo maana tunajiuliza Kamati hii inatoa wapi huu umagumashi wake?
 
Tunajuwa kwamba Moroco kwa muda mrefu ilikuwa inatafuta walambaji rushwa wa serikali ya Tz ili watugeuze msimamo wetu juu ya Sahara Magharibi wanayoikalia kwa mabavu, it seems Moroco has found what she has been looking for: Lowassa.
 

Inaonekana Mwalimu alikuwa anaunga mkono harakati za maeneo ya Mataifa mengine Africa kujitenga,nadhani ni katika mantiki ya kuepuka machafuko, hivi wakati wake haya malalamiko ya wanzibar yalikuwapo?
 
Watu wa CCM bwana, kila wanalofanya lazima liwe na matatizo, au ndio magonjwa kaanza kukataa uji?
 
Naona Mama Shelukindo anacheka jino pembe. Nasikia alishajisalimisha kambini.

Huyu mama Sherukindo si ndo aliambiwa na Joshua wa Nigeria kwamba EDO ndio the next president?
 
Reactions: FJM
Wanajichanganya katika matamko yao kuanzia ndani ya nchi mpaka nje ya mipaka, Ndio aina viongozi wa chama hiki kilivyo.
Na hii ni system tayari haiwezi kubadilika mpaka M4C ishike dola
.
 
huyu mzee lowassa si mlixema anaumwa amepitishwa eapoti kimyakimya? au?
 
mmmmmmmmmmmmmm sijiu maana Tanzania ni kama familia isiyokuwa na malezi mazuri yaani kila mmoja anaweza toa msimamo wake bila kujali nani anajukumu la kufanya hivyo
 
Naona Mama Shelukindo anacheka jino pembe. Nasikia alishajisalimisha kambini.

rais mtarajiwa,yupo kazin,,,,,,,,hii ni iwapo cdm ikikosea ikawa na migogoro itakayo i nccr,,mageuzi,,,,,ndani ya ccm nani,,yuko wapi,,,,real hakuna,,,tena heri tu wamproud atawasaidia kupata wabunge,,,,wakimpondaaaa ,,,siku zaja,ccm ni kanu,
 
hivi leo hii mimi kama mtanzania...why should i care about western sahara...is that our problem, do we give a shoot about them...cmon..sisi wenyewe hapa tanzania tuna matatizo yetu mengi tuu..hawa wazee wa hii kamati kama hawana kazi za kufanya kuliko kutumia hela za walipa kodi kujipandisha kwenye ndege na kwenda kukaa kwenye 5star hotel huko ni bora wakamuone zitto kabwe..ana kazi chungumzima za kuwapa zenye maendeleo ya nchi hii:angry:
 
Hii safari ya kamati ya Lowassa huko Morocco imenipa maswali mengi sijui hata pa kuazania?

Kwanza hii safari ina maslahi gani na Jamhuri ya muungano wa Tanzania? Ni nani anahusika kutoa vibali kwa kamati za bunge kusafiri ndani na nje ya nchi? Na hii safari walienda kwa sababu zipi? Kwa nini Morocco? Walikuwa wanataka kutatua tatizo gani kwa niaba ya wananchi wa Tanzania?

Kama issue ni Morocco na Western Sahara kwa nini kamati ilifanya mazungumzo na upande mmoja tu (Morocco) na sio pande zote mbili? Kwa nini baada ya kuongea na viongozi wa Morrocco Kamati haikwenda kuonana na uongozi wowote toka upande wa pili wa shilingi (Western Sahara)? Huko sio kuchukua side? Ina maana Tanzania tumebadilisha msimamo wetu kama nchi?

Hapa nadhani Spika wa Bunge anatakiwa atoe majibu, kamati ya bunge ilikwenda Morocco kwa lipi? na wamepata nini?
 

My concern sio kuitambua au kutoitambua bali ilikuwaje Kamati hiyo ikaenda Morocco!! Ina maana Kamati za Bunge huwa zinaenda nje ya nchi?! Anyway, lakini hata kama, mbona sioni kama kuna mafungamano yoyote kati ya TZ na Morocco iwe kisiasa, kiuchumi au hata kiutamaduni?! At least ningesikia Misri, nisingeshangaa sana; lakini Morocco?!!
 
Reactions: FJM
This must be officially addressed by gov of Tanzania kuweka mambo sawa.Lowassa anazidi kujiharibia. hiyo ziara inaibua maswali mengi
 

Hili lisikushangaze ,Membe naye alikuwa ana mambo yake binafsi kwa kutoa matamko yanayolemea upande wa mapenzi yake kwa faida yake binafsi.Ila soon mtajua kwamba ule ulukuwa ni msimamo wa nchi ama Membe.

Kwa wale wafuatiliaji mtakumbuka Membe kipindi ambacho serikali ya Gadaffi imeanguka alitoa tamko la kutoitambua Serikali mpya ya iliyotwaa madaraka.Haya aliyatoa pale alipoulizwa swali BBC kuhusu kushushwa bendera ya Libya (Utawala wa Gadafi) kwenye ubalozi wa Libya -Tanzania.
Siku chache zilizofuata ikaguundulika ilikuwa sio msimamo wa nchi bali Membe alitoa tamko lile kutokana na msukumo wa uswahiba wake na aliyekuwa raisi wa Libya (M. Gadaffi)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…