Ni wajibu wa TCRA kuwazuhia kampuni za simu kufanya yafuatayo: Kulazimisha wateje michezo ya bahati na sibu kwa kuwalaghai na maneno ya kitapeli, na mteja husipokuwa makini unakuta unakatwa shilling mia tano per SMS, kupoteza muda kwa kusikiliza matangazo ya biashara kabla hujaunganishwa - mtu kama una simu ya emergency unaweza kutupa chini simu kwa hasira, utangazaji wa biashara kwenye simu umezidi sana wateja wanahitaji mawasiliano siyo matangazo ya biashara-kama kunamteja anahijati huduma hizo za biashara basi a-subscribe na siyo kulazimishwa kusikiliza clap! TCRA imewapa a blank cheque kampuni hizi kufanya watakalo, mtu unaweza kufikili hakuna chombo cha Serikali cha kuratibu mambo hayo.
Kilichowahi kunishangaza zaidi kuhusu TCRA, ni pale walipo sema walikuwa hawajuhi SMS zilizokuwa zinatumwa kwa wateja wa simu za mikononi wakati wa vugu vugu la uchaguzi wa RAISI zilikuwa zionatoka wapi; we fikilia ajabu hiyo, lakini pale una ambiwa kuna Mkurugenzi wa ICT, naibu wake na maafisa chungu mzima wanao husika na ICT, watu hawa walishindwaje kujuwa nani alikuwa anasambaza SMS za uchochezi; bila juhudi za ITV ku-trace origin za SERVERS zilizokuwa zinatumika kusambaza SMS hizo hakuna mtu yeyote ambaye angejuwa kilichokuwa kinaendelea na nani muhusika!