PreGE2025 Kamati ya Bunge yaipongeza Serikali ukarabati wa soko la Kariakoo. Wafanyabiashara 1,002 tayari wamepangiwa maeneo

PreGE2025 Kamati ya Bunge yaipongeza Serikali ukarabati wa soko la Kariakoo. Wafanyabiashara 1,002 tayari wamepangiwa maeneo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,439
Reaction score
6,692
Haya ndio madhara ya Bunge na Serikali vyote kutoka kwenye chama kimoja. Yaani hizi kamati za Bunge kazi yake imekuwa ni kupongeza tu. Sijawahi kuona hata mradi mmoja ambao hizi kamati zimesema kama hauendi vizuri.

Tukisema hizi ni kampeni za Uchaguzi mtakataa?

====================================

Kamati ya Bunge yaipongeza serikali kwa kufanikisha ujenzi na ukarabati wa Soko la Kariakoo, ambalo limeboreshwa na kuwa na viwango vya kimataifa.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Justin Nyamoga, Aprili 12, 2025, Dar es Salaam, wakati wakikagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo na maandalizi ya kuwarejesha wafanyabiashara.

“Sisi kama Bunge tumekagua na kujionea kazi kubwa ya Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan aliyetoa shilingi bilioni 28.03 ili kujenga soko jipya na kukarabati lile lililoungua, mradi huu utanufaisha watu wengi,” amesema Nyamoga.

Nyamoga ameongeza kusema wabunge wameridhishwa na viwango vya ubora na usalama vilivyowekwa katika Soko la Kariakoo, unaolifanya kuwa na taswira ya kimataifa.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI Festo Dugange, amesema mradi huo ulianza kutekelezwa mwaka 2022 umefikia asilimia 98 ukigharimu zaidi ya Sh bilioni 28, utaongeza nafasi za biashara toka 1,662 hadi 1,907.

Dugange alieleza kuwa lengo la serikali ni kuweka mazingira bora ya ufanyaji biashara katika Soko la Kariakoo, ambalo litafanya kazi kwa muda wa saa 24 kuwa maandalizi yamekamilika.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amesema soko litafunguliwa hivi karibuni na kwamba Serikali itahakikisha wafanyabiashara wote wenye sifa wanapatiwa maeneo kulingana na sifa zilizoanishwa.

kkoosoko.png

Akitoa taarifa kuhusu maandalizi ya kuwarejesha wafanyabiashara sokoni hapo, Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo, Ashraph Abdulkarim amesema tayar wafanyabiashara 1,002 kati 1,520 wa kundi la kwanza wamepangiwa maeneo ndani na mfumo wa TAUSI.

Abdulkarim ameongeza kusema, wafanyabiashara 518 kati ya 1,520 wana changamoto mbalimbali ikiwemo 194 kuwa na madeni ya nyuma, 134 hawajajaza fomu maalum na 190 hawana namba ya kitambulisho cha Taifa (NIDA) na Namba ya Mlipa Kodi (TIN), hivyo hawajapangiwa maeneo hadi sasa.

Source: Nipashe
 
Back
Top Bottom