Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara yaikataa taarifa ya Wizara ya Viwanda

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
Kamati ya bunge ya viwanda na biashara imeikataa taarifa ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji na kumpa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt Adelhem Meru, muda zaidi kuandaa taarifa itakayokidhi haja na matakwa ya kamati hiyo, juu ya uendelezaji wa biashara na sekta ya viwanda nchini.

Dkt Meru ametakiwa kukamilisha taarifa hiyo na kuikabidhi kwa kamati hiyo kabla ya kikao cha bunge la bajeti kitakachoanza mwezi April mwaka huu.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dkt Dalali Peter Kafumu ametoa agizo la kuikataa taarifa hiyo, ambayo amesema haioneshi hali halisi ya viwanda nchini ikiwa ni pamoja na viwanda vilivyobinafsishwa, vinavyofanya kazi, vilivyokufa, sababu ya viwanda hivyo kufa na hatua zinazochukuliwa na serikali ili mpango wa Rais Dkt John Pombe Magufuli wa kujenga uchumi wa viwanda kutekelezeka.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bi. Vicky Kamata amemtaka Katibu Mkuu huyo kuhakikisha kuwa taarifa atakayoikabidhi inakuwa na mpango wa jinsi serikali itakavyotekeleza ujenzi wa viwanda katika mkoa wa Geita, hasa kutokana na jinsi mkoa huo unavyohitaji viwanda kwa ajili ya kuongeza thamani mazao kama maziwa, ngozi na nyama ya ng'ombe kutokana na kuwa na idadi kubwa ya mifugo.
 
Back
Top Bottom