Kamati ya Bunge ya viwanda na biashara yaagiza Serikali kupiga marufuku mifuko ya plastiki kutoka nje ya nchi

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
4.JPG
Dodoma. Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira imeiagiza Serikali kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki kutoka nje ya nchi ili kulinusuru Taifa na madhara yanayotokana na mifuko hiyo.

Maagizo hayo yalitolewa baada ya kamati hiyo jana kukutana na Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

Akizungumza jana, mwenyekiti wa kamati hiyo, Sadiq Murad alisema walipata maelezo kutoka serikalini kuwa uzalishaji katika viwanda 41 vya plastiki nchini ulikuwa ni tani 73 katika mwaka 2016.

Hata hivyo, alisema mifuko iliyoingia nchini kupitia bandarini na mipakani ilikuwa tani 1,375.

“Kamati ilishauri ipigwe marufuku mifuko ya plastiki kutoka nje ya nchi na iwekwe tahadhari katika mipaka yetu,” alisema.

Alisema kamati inaitaka Serikali kufanya uhakiki wa uzalishaji katika viwanda vya nchini ambavyo vimepunguza uzalishaji ili waweze kukaa chini na kuzalisha mifuko ambayo itakayokidhi mahitaji na vigezo.

“Na hii itakuwa ni ya muda kuzalisha mifuko hiyo kwa masharti ya vigezo baadaye Tanzania isiwe na uzalishaji wa mifuko hii tena inayoharibu mazingira,” alisema.

Murad alisema zipo nchi nyingine kama Kenya, Rwanda, Uganda na Zanzibar ambazo zimepiga marufuku uzalishaji na uingizaji wa mifuko hiyo na kutafuta mifuko mingine inayotengenezwa na nguo, karatasi na majani.

Alisema mfano mzuri ni Zanzibar ambayo imepiga marufuku mifuko hiyo tangu mwaka 2016 na mtu anapoingia na mifuko hiyo bandarini hunyang’anywa na kupewa mingine.

“Tueleweke kabisa sisi kama kamati hatutaki kiwanda chochote kifungwe, tunataka uzalishaji kwa kufuata masharti na vigezo. Tunaunga mkono juhudi za Rais John Magufuli za kuipeleka nchi katika uchumi wa viwanda lakini vigezo na masharti lazima yazingatiwe,” alisema.

Akizungumzia agizo hilo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba alisema hawaja japelekewa rasmi hayo mapendekezo. Hata hivyo alisema watapiga marufuku mifuko yote ya ndani na nje. “Wenye viwanda wajiandae maana yake dhamira ya Serikali wanaijua tangu mwaka 2016,” alisema


Chanzo: Mwananchi
 
Kupiga marufuku wakati wewe unahitaji sio fair. Waongeze kodi kwenye hiyo mifuko ya Rambo.
 
Kwa bahasha wanazopata kutoka kwa Jumuiya ya wenye viwanda hivi sidhani, watapiga chenga tu. Labda magufuli atangaze mwenyewe ila sio mawaziri au manaibu wao.
Huyu waziri na naibu wake hizo bahasha zitakuja kuwatokea puani. Tani 73 tu ndio tunazalosha, lakini zaidi ya tani 1,300 zinaingizwa toka Kenya, hii maana yake ni kwamba Tanzania tunageuzwa dampo la taka za sumu toka Kenya kwa manufaa ya uchumi wa Kenya,nthis is not fair. Kila siku watz wanakumbwa na magonjwa ya kansa, uchafuzi wa mazingira na mafuriko kwa sababu ya hii mifuko, serikali ifanyie kazi hayo mapendekezo ya kamati ya bunge.
 
Bila bila

Ova
Kwani tumekwama wapi?
====================================
By JAMES KARIUKI
More by this Author


High-level consultations are underway to allow firms that manufacture plastic bags for export to remain in business in a bid to save the Sh3 billion a year industry, representing 38 per cent of all sector export earnings.

Statistics indicate that in 2016, sale of plastic bags earned Kenya Sh1.38 billion for 6,911.4 tonnes of sacks and bags from DRC Congo; Sh731.7 million for 3,826.8 tonnes (Burundi), Sh354 million from 1,379 tonnes (Comoros Island) and 1,192 tonnes worth Sh316 million from Mozambique.

Other countries receiving Kenyan products include South Sudan, Uganda, Malawi, Somalia, Zambia, Madagascar, Colombia, Ethiopia, India, Djibouti, Denmark, Tanzania, Chad, Switzerland and America.

Sources within the Trade and Environment ministries said they had formed a committee together with the Kenya Association of Manufacturers to come up with a working modality that will end the month-long stalemate since the machines went silent.

Most of the 160 plastic packaging companies have remained closed, with workers declared redundant following the ban that took effect on August 28.

Last week, manufacturers roped in the Export Promotion Council (EPC) in their quest to have their operations re-opened. They agreed to discuss various options that could see them re-launch their operations.

The manufacturers say their products are not for the Kenyan market, adding that their cargo could be loaded onto containers, sealed and an electronic tag placed on them to ensure they are transported to their destinations.

Contacted, EPC chief executive Peter Kibet said Kenya is looking at all avenues to grow its export volumes from last year’s Sh578.1 billion against imports of Sh1.43 trillion.

“We fully support the plastic packaging products ban and would wish to see Kenya embark on waste management investments that provide a leeway for plastic bag-for-export manufacturers to resume operations. Kenyans need to change their attitude on disposal of waste to facilitate recycling,” he said.

READ: Traders, makers of plastic bags denied the export option

The National Environmental Management Agency (Nema) allows manufacture of primary plastic packaging materials for industrial use but has maintained that secondary use is prohibited, with punitive penalties imposed.

Uganda has since invited Kenyan plastic companies to their country, promising to give them land and to fast-track licensing procedures. Investors and workers who will be assisted to acquire permits will be at liberty to repatriate the profits and earnings.

Mr Kibet said that while Kenya’s exports grew by a paltry 1.3 per cent, there was a need to safeguard the gains made while looking for other means to increase the earnings by about 15 per cent annually until 2030.

This would reduce the export-import imbalance by 50 per cent, he said.

“Kenya is jealously safeguarding its export markets. We are open to suggestions on how the plastics-for-export packaging companies can resume operations once proper mechanisms are found. We could turn them into export processing zones and deliberately deny them a local market option, or order them to move into special economic zones targeting the export market,” he said.
 
Itakuwa wenye viwanda wanatembeza mlungula wasifungiwe biashara hyo
Mkuu unaonaje tukianza ku produce mifuko ya karatasi sasa na Sisi tufungue ka kiwanda

Ova
Hizi rushwa ndio zinaangamiza afya za waTanzania, we can do away with plastic bags
 
Back
Top Bottom