Kamati Kuu ya CHADEMA yakutana Igunga

ombi langu kwa chadema ni kila kituo msimamizi msije mkatuambia kituo X hakikuwa na msimamizi na ningependa muwape semina ya kutosha sina wasiwasi kwa hilo yuko kama G. Lema..
 
Kwanini CUF wasiungane na CCM kumsimamisha mgombea wao mmoja? au wewe hujui kuwa CUF na CCM lao ni moja?
Mkuu,
wala usihangaishe kichwa, huyu mwenzetu sometimes ni very controversial.

Umesababisha nikumbuke utata wa misimamo yake tangu alipokuwa akituelezea habari za mgomo wao UD siku za nyuma.

Maelezo yake mengi yalikuwa ndivyo sivyo!! huyu ndugu ni lukewarm
Muhimu kwa wapambanaji ni kusonga mbele tuu.
 
Kamati kuu ya chama cha chadema kuweni makini na mamluki wa chama tawala,Kumbuka ktk msafara wa mamba na kenge wapo.
 

Hongera dada Regia,nawaombea mfike salama,Igunga yetu, lakini huyu Shibuda tunamfanyaje jamani?

Naomba wembe ulitumika kuwanyoa madiwani utumike upande wa pili ukiwa na makali zaidi ya madiwani kumng'oa huyu kibaraka wa CCM, CHADEMA FOR CHANGE.
 
<br />
<br />
Naunga mkono maelezo yako 100%,na ikumbukwe kua huyu bwana Shibuda ni rahisi sana hata kutoa siri za Chama huko tuendako eg.chukulia karibu tunaelekea uchaguzi na akajaribu kuvujisha SIRI za Chama hamuoni kua atakua ametuharibia sana? mtu gani huyu hataki kuendana na Philosophy ya Chama?

Jana nimekeleka sana na ameniumiza sana na huko Igunga kuweni makini na watu wanaofanana na huyu kiruka njia,nina hasira sana na maisha haya tunayoishi.
 

Hapo kwenye red. Kwa mujibu wa Katiba, Mbunge ana kinga ya ajabu sana kwa lolote atakaloongea AKIWA KWENYE VIKAO RASMI NDANI YA UKUMBI WA BUNGE.

Hakuna mamlaka yoyote, hata Mahakama ya Rufaa, yenye uwezo wa kumhoji Mbunge kwa kauli zake "ndani ya Bunge". Labda kwa kujua hilo, ndio maana Shibuda anafanya mizaha anayoifanya.
 
Thanx dada Regia nakutakieni cc njema na mungu awaongoze mtuletee mbunge wa Igunga
 
Kwa hiyo hata ukimtukana rais matusi ya nguoni bungeni hansad inakulinda........labda mimi sielewi.
 
Kwa hiyo hata ukimtukana rais matusi ya nguoni bungeni hansad inakulinda........labda mimi sielewi.

Kuna taratibu zake na hatua zinachukuliwa humo humo ndani ya Bunge na si nje ya hapo. Ndio maana Spika/Mwenyekiti wakati wote hachezi mbali na kauli za wabunge wanapochangia kuhakikisha hakuna ukiukwaji wa Kanuni za Bunge ikiwamo hilo la kutukana.

Ndio maana utasikia "futa kauli", "lete ushahidi", n.k.
 
Ahsante kwa taarifa mpiganaji wetu.zingatieni kua magamba ni wazuri sn katika rafu na rushwa katika uchaguzi na ni vema mkumbuke kua cuf hawaipendi cdm na wapo tayari kuwasaport ilimradi cdm ikose ushindi.

Hivyo nashauri makamanda muwe makini na mumtumie sn huyo diwani wetu wa hapo igunga.
 
Asante kwa taarifa tunaiamini kamati kuu itamteua m2 makini atakae toa ushindi wa kishindo. Naamini kuanzia kesho Igunga itafunikwa na VAZI LA TAIFA (magwanda)
 
Nyie mnaolazimisha CDM iungane na CUF kwanini CUF wasiungane na CCM halafu mtuambie ni wapi wapinzani waliungana wakashinda,
kama ni kugawana kura hata CCM itagawana na CUF maana CDM wanaenda bila kuwa na kura hata moja, ngoja niwape mahesabu yatavyokuwa,

Uchaguzi uliopita CCM walipa kura 35,000 safari hii watapata nusu ya hizo nusu iliyobaki itakwenda Chadema yaani 17,500.
CUF walipata kura 11,000 safari hii hata nusu yake hawapati basi tuwape nusu 5,500 na nusu iliyobaki itakwenda Chadema yaani 5,500.
Final results
Chadema kura 17,500 + 5,500 = 23,000.
CCM kura 35,000/2 = 17,500.
CUF kura 11,000/2 = 5,500.
 
Nadhani swali lako limejibiwa vizuri na Mwita Maranya.....
 
Mheshimiwa Regia nakubali CDM mko serious lakini jambo dogo tu huwa tunamalizwa na CCM, mimi ni mzaliwa wa igunga na nimeishi igunga muda mrefu sana kwahiyo nafuatilia kwa karibu mchakato wa igunga tangu kujiuzulu kwa rostam, nawajua wafuasi wa CCM na CDM. weakness ya CDM Igunga hakuna uongozi imara wa CDM, nasema hivyo kwasababu mwenyekiti wa wilaya Majimoto, Kashindye na Pili mnene (amekuwa mwenyekiti wa wanawake wa chadema wilaya tangu kujiuzulu kwa rostam kabla ya hapo alikuwa ccm) walikuwa wakala wa rostam uchaguzi wa 2010.

Majimoto alijitoa kugombea ubunge kwa kupewa fungu na rostam, Kashindye alteuliwa kuhamasisha kura za uraisi kwa jakaya kwa kauli mbiu aliyokuwa anawambia wanaigunga vijijini kuwa DR. SLAA ni fisadi wa mapenzi ili wanawake wasimpigie kura. Pili Mnene amejengewa nyumba na rostam na mpaka sasa anasomesha mtoto wake chuo kikuu. Mheshimiwa diwani wetu wa chadema kwenye vikao vya council anapokea posho anayotoa RA ili kuweza vikao vya madiwani vipitishe matakwa yake kwa remote wakati yeye anakula raha jijini.

Sasa kabla ya kupitisha mgombea wenu kesho mheshimiwa kashindye muhakikishe mmesafisha jambo hilo kwani walimu wote wanajuwa kuwa alikuwa kibaraka wa rostam kufanya kampeni za ccm 2010 sasa wapiga kura wenu watakuwa na imani nae vipi kwasababu wanamtambua kama CCM na kwataarifa nilizo nazo hadi sasa wamekorofishana na DC igunga kwa kuwa wanajuwa kilichofanyika mwaka jana. Na siku chache baada ya kujiuzulu RA, Bashe alivyokuja igunga alimtumia Kashindye kuwapelekea wenyeviti wa kata salamu kutoka kwa rostam na kuwajulisha kuwa yupo nao pamoja fungu alilopewa alimficha boss wake DC na badala yake akatumia gari la ukaguzi na mafuta ya serikali bila kumgawia boss wake fungu.

TUPO NJIA PANDA wanaigunga kwa maana kwamba tutapata bora mbunge kwa maslahi yake mbunge na kuongeza fungu la posho kwenye chama au tunapata mbunge ili kuweza kuwatumikia wanaigunga? NITOE NJIA PANDA KESHO
 

chadema wanayo nafasi ya kushinda ila wako mtegoni mpaka sasa, CUF msijisumbue sana bora muwaunge mkono ccm kwani Dr. Kafumu ameyavulia nguo maji na hana budi kuyaoga mpaka ameacha budget ya wizara yake haijapita yupo kwenye mchakato. DANGER, mzimu wa rostam unasumbua igunga bado.
 
Unaongea sana kama kasuku kila kitu wewe unakijua ah waache wana Igunga wachague wanayemtaka kwani tatizo lako nini mbona unaumia sana kuna nini, kwani kuhama chama ni dhambi kwa taarifa yako karibu asilimia 80 ya wapinzani walikuwa CCM hata hao unaowaona viongozi wa CDM walikuwa huko huko.
 

Dada yangu Mh. Regia Mtema naandika huku nikibubujikwa na machozi ya furaha hasa baada ya kuniakikishia ushindi huko Igunga, sidhani kama kuna Mwanaigunga anayewaza kuwachagua CCCM, matatizo yaliyopo katika nchi hii hayawezi kutatuliwa na CCM tena na hilo Igunga wanalijua fika hivyo tunategemea kumsimamisha mtu ambaye atawatendea haki wanaigunga maana ni lazima tu CDM inashinda hiyo haina ubishi.

Hongera sana Mh. Regia kazi yako inaonekana, wakabeni koo hao Magamba.
 
Naskia NAPE yupo nyumbani kwa Mkurugenzi wa usimamizi wa uchaguzi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Igunga.

Lengo ni kupanga mkakati wa kuiba kura na kumtangaza mgombea wa CCM kwamba ndiye atakuwa mshindi siku ya kutangaza matokeo.
 
Tumbili, ccm hadi sasa wanajenga mazingira ya kuiba kura maana wanaamisha watendaji wanaoonekana kutopokea maelelekezo yao au wasio tayari kuwa remoted kutoka juu, amini nawaambia kuwa kuna uwezekano mkubwa saaaana wa kumwamisha mkurugenzi mtendaji wa wilaya ndugu Protas Magayane kabla ya uchaguzi huu mdogo.

Juzi kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa ilikutana kuweka mikakati ya ccm kubaki na jimbo na amri kutoka kwa Jk ni kuwa hata kwa kupindua matokeo halali wafanye kwa gharama yoyote ilimladi jimbo libaki ccm!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…