Balungi
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 234
- 162
Wananchi wa wilaya ya Newala hawana amani kufuatia kukamatwa ovyo na watendaji wa serikali za vijiji wakishirikiana na jeshi la polisi kwa nyumba ambazo hazina vyoo vya kudumu.
Zoezi hili linaendeshwa kwa madai kuwa, kila nyumba inatakiwa kuwa na choo cha kudumu hata kama una choo cha kawaida cha kudumu lakini wao wanataka choo kilichojengwa kwa matofali ya saruji bila kuzingatia uwezo wa mtu.
Hakuna muda uliotolewa kwa ajili ya utekelezaji wa kujenga vyoo, na kama ukikutwa hauna aina hiyo ya choo unapigwa faini Tsh. 50,000/= papo hapo, na wanasema hiyo ni kwa ajili ya kukusanya fedha kwa ajili ya maendendelo.
Inashangaza sana, kama ni hivyo kwa nini wasikusanye pesa tu kwa mtindo mwingine kwani ni lazima wajifiche kwenye vyoo vya kudumu?