nkongu ndasu
JF-Expert Member
- Jan 19, 2013
- 22,532
- 6,613
kwa sasa hatuna kiongozi yeyote wa kukemea huu uvunjaji wa katiba unaoendelea. r.i.p mwalimu nyerere...
Umh.... Haya bhana. Hii ni fasihi simulizi au andishi?Niliwahi kuudhuria msiba fulani zamani nikashangaa watu walikuwa wanapongezana kwa kifo cha aliyekufa kwenye msiba huo!
Nani amemtukana Magufuli?Bila moto huu hawa vibendera hawata kuwa na heshima.
Kwanza naona bado bado sanasana zaidi
Mijitu ilimtukana sana Jk
Sasa mazoea mabaya Magu sio Jk
Bila kupotezwa watu hatuta heshimiana
Kwa hali ilivyo sasa, ili kupiga hatua za maendeleo katika nchi yetu ni lazima kwanza rais awadhibiti wote wanaojaribu kuhatarisha hali ya usalama kwa matamko yasiyo na tija kwa maendeleo ya nchi yetu. Ifike mahala tuwe wakweli katika hili. Watu hawa wamekuwa hawana jema, kazi yao kubwa ni kupinga kila jambo linalofanywa na mheshimiwa rais Magufuli. Zaidi ya hayo wamekuwa wakitoa lugha za matusi na kejeli. Mtu waliyemwita fisadi kwa vinywa vyao leo hii kwao amekuwa mtakatifu, je watu hawa tuwaweke kwenye kundi gani? UFISADI ulipokuwa umeshamiri katika nchi hii walikaa kimya bila kuleta fyoko fyoko wala katangaza maandamano. Leo mheshimiwa rais Magufuli amejitahidi kwa kiasi kikubwa kupiga vita ufisadi, wao wanaanza kuleta fujo, kejeli na matusi. Je, watu hawa wana uchungu wowote juu ya nchi yetu? Mimi naona bado rais ana huruma ndiyo maana wanarudia rudia kutoa kauli za kuudhi. MHESHIMIWA RAIS MAGUFULI, NAOMBA UCHUKUE HATUA KALI ZAIDI DHIDI YA WATU WANAOTAKA KUFIFISHA JUHUDI ZAKO KATIKA KUIJENGA NCHI YETU. MUNGU IBARIKI TANZANIA, MBARIKI RAIS MAGUFULI NA VIONGOZI WOTE WA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. AMINA.
Walioleta hiyo kauli mbiu hawalijui hilo wakiamini wao sheria haziwahusuMada iko wazi: tuheshimu sheria na katiba. Kutii sheria bila shuruti ni wajibu ni wajibu wa kila mtu (raia, pokisi, nk). Vile vile kutoheshimu sheria au katiba kwa polisi kuwakandamiza wengine yakiwamo kuwakamata na kuwanyima dhamana kinyume cha sheria na katiba kufikia "si utii wa sheria bila shuruti -- huu ni utovu mkubwa aka jipu lililoiva sana linapaswa kutumbuliwa haraka si la kulea hata kidogo".
Kwa maana nyingine mkuu -- wanaotakiwa kutii sheria bila shuruti ni watu wote wakiwamo polisi pia.
Au wewe huoni hivyo?
Nchi hii itajengwa na sisi sote. Hebu isifike mahali wengine wakadhani wao ni bora zaidi. Sisi sote tu sawa mbele ya sheria na katiba mkuu. Hakuna aliye juu ya hapo.