Kamata kamata ya Polisi na kunyimwa dhamana. Ushauri wa bure kwa Rais Magufuli

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,223
35,149
Kwako mheshimiwa,

Ninalazimika kukupa ushauri huu wa bure maana ninaamini unao washauri waliobobea kabisa ambao haiyumkini wanalipwa mapesa mengi kwa kwa ushauri wao kwako. Ninaandika haya kwako nikiamini unakubaliana nami kuwa hayuko mmoja aliye juu ya sheria wala juu ya katiba. Ambaye ati kuwa yeye ni mwenye haki ya kuvunja sheria na hivyo katiba kwa namna yoyote ile klasi cha kuathiri utangamano wa watu wengine wanaomzunguka. Ulichoapa mheshimiwa ilikuwa ni kulinda katiba kwa maana ya kwamba utamtumbua jipu yeyote ambaye si tu kuwa atavunja katiba bali hata yule ambaye angejaribu au kuonesha kuonyesha dalili za kukiuka haya uliyoyaridhia kuyalinda. Kuilinda kwako katiba kungetoa hakikisho kwa wote kuwa kusingekuwa na uonevu wa makusudi kwa mtu yeyote kutokea kokote kwa kisingizio chochote kile. Kwa hali hii maisha yangekuwa "Murua" kama wasemavyo Vodacom.

Sasa mheshimiwa nitanatumaini unazo habari kuwa kuna watu (polisi) wanazuka na kukamata watu, kuwaweka wengine ndani na kuwanyima dhamana. Kwako waliona vipi hili mheshimiwa? Hakika kwa misingi ya katiba tuliyonayo, hili si sahihi. Matukio ya namna hii yamekuwa yanajitokeza mara kwa mara pasipo na kukemewa tokea kwako. Katika hali ya kawaida kabisa kwa hakika hili si sawa.

Sote tumerithi utamaduni mwema sana tokea kwa mababu zetu. Sisi tu Watanzania ambao tumefunzwa kuwa sote ni ndugu. Pamoja na tofauti zetu ambalo ni jambo la afya tu, hatuwezi kukubaliana kufuata sheria na misingi imara iliyoko katika katiba ambayo kimsingi imewekwa na kuridhiwa na sisi sote kwa ujumla wetu?

Kama ilivyokuwa katika mchezo wowote uwe wa mpira wa miguu nk. sheria ni muhimu na zote lazima ziwe zinafahamika kabla ya mchezo pasipokuwa na shaka yoyote kwa kila mchezaji. Hali hii ni vivyo hivyo hata kwetu sisi katika maisha ya hapa duniani kabla ya kumrejea mola wetu huko kwenye makao ya milele.

Kwa nini basi mheshimiwa na sisi tusiachane na haya matamko tata yasiyokuwa na mashiko yoyote ya kisheria wala kikatiba yanayochipuka kila leo tokea kwa watu mbali mbali na hasa polisi tukajikita katika kufuata sheria na katiba pasipokuwa na kisingizio chochote?

Ndugu mheshimiwa ni wazi kuwa tukikubaliana kufuata katiba "Tutachapa kazi kweli kweli. Kama kila mmoja wetu atakuwa na uhakika wa sheria au utaratibu (katiba) ipi iliyo rasmi ambayo sisi sote yaani: wewe, polisi na raia kuwa hizi ndizo pekee zinazoongoza mahusiano yetu na wengine mbona nchi hii itakuwa ya mfano kama ilivyokuwa siku za nyuma tokea katika awamu zote nne zilizopita? Bila hilo sijui wewe mheshimiwa unaona vipi, lakini kwa mtazamo wa wazi, mbona tunakoelekea kutakuwa kuna giza nene lisilo na chembe ya matumaini?

Pasipo na kumung'unya maneno, mbona nchi hii tulikuwa tumeshapiga hatua sana katika utawala wa sheria (rule of law). Chonde chonde mheshimiwa Magufuli pamoja na kuwa hapa tulipo sasa hivi si pema sana, bado tunayo nafasi na tunaweza kurejea nyuma, tukajizatiti na kubadilisha muelekeo.

Vuta kumbukumbu mheshimiwa: "Mkiwa wizara ya ujenzi wewe na mheshimiwa Daktari Mwakyembe, Raisi mstaafu wa awamu ya pili aliwahi kuwashutumu hadharini kuwa "mu-wababe mno!".

Tulio wengi tungali na matumaini nawe kuwa utaliona hili katika mtizamo ule wa kiungwana ya kwamba kuteleza si kuanguka.

Tunayo nafasi kubwa kabisa ya kujenga nchi yetu katika hali iliyokuwa na utangamano. Sisi sote tu Watanzania na kwa umoja wetu tusikubali kuipeleka kusikokuwa na tija. Hebu tuone kuwa kila mmoja wetu yuko na haki na usawa wa msingi ya kufurahia maisha hapa duniani na pia katika kuchangia mstakabala wa nchi hii tuipendayo: kiuchumi na kimawazo kwa uhuru kabisa pasipo na hofu yoyote kwa mujibu wa katiba.

Ninaandika haya tukiwe tumeshudia wengi yaliowakuta ya kulindikwa ndani na kunyimwa dhamana katika hali za kushangaza iliyo kinyume cha katiba:

1. Pana wabunge wamekuwa wakikamatwa wananyimwa dhamana
2. Kuna madereva walikamatwa juzi juzi kwa makosa ya usalama barabarani mkoani Kagera wakanyimwa dhamana.
3.
4.
5.
.
.

.

.
.
100.
.
.
.

Matukio yamekuwa mengine mno hayatoi taswira nzuri ya nchi hii ambayo imekuwapo tokea enzi za wasisi wetu. Nimeachia pale wazi wengine nao wanaweza ongezea mifano halisi ambayo imetokea tangia awamo ya Tano imengia madarakani mheshimiwa.

Ni matumaini yangu utaiona nia njema iliyoko katika ushauri huu na labda ukatafakari na kuchukua hatua.

Mungu akubariki na Mungu aibariki Tanzania.
 
Kiongozi mkuu Wa chadema akiwaonya bavichaaa pamaoja na Lisu wao waache siasa za uanaharakati wanakomaa tu.

Acha wanyooshwe na kupigwa tu maana hamna namna.
 
Niliwahi kuudhuria msiba fulani zamani nikashangaa watu walikuwa wanapongezana kwa kifo cha aliyekufa kwenye msiba huo!
 
Sidhani kama busara ya andiko lako kuna atakayeiona muda huu, mwaka huu na ijayo
 
Tunaambiwa tutii sheria bila shuruti

Mada iko wazi: tuheshimu sheria na katiba. Kutii sheria bila shuruti ni wajibu ni wajibu wa kila mtu (raia, pokisi, nk). Vile vile kutoheshimu sheria au katiba kwa polisi kuwakandamiza wengine yakiwamo kuwakamata na kuwanyima dhamana kinyume cha sheria na katiba kufikia "si utii wa sheria bila shuruti -- huu ni utovu mkubwa aka jipu lililoiva sana linapaswa kutumbuliwa haraka si la kulea hata kidogo".

Kwa maana nyingine mkuu -- wanaotakiwa kutii sheria bila shuruti ni watu wote wakiwamo polisi pia.

Au wewe huoni hivyo?

Nchi hii itajengwa na sisi sote. Hebu isifike mahali wengine wakadhani wao ni bora zaidi. Sisi sote tu sawa mbele ya sheria na katiba mkuu. Hakuna aliye juu ya hapo.
 
Bila moto huu hawa vibendera hawata kuwa na heshima.

Kwanza naona bado bado sanasana zaidi
Mijitu ilimtukana sana Jk
Sasa mazoea mabaya Magu sio Jk

Bila kupotezwa watu hatuta heshimiana
 
Kiongozi mkuu Wa chadema akiwaonya bavichaaa pamaoja na Lisu wao waache siasa za uanaharakati wanakomaa tu.

Acha wanyooshwe na kupigwa tu maana hamna namna.

Unafurahia ukidhani wanakomeshwa wapinzani, jambo likizoeleka ubadilika na kuwa sheria siku moja Mungu atayaruhusu yaje kwako ndipo utakapojutia kushabikia uvunjifu wa sheria unaofanyika sasa.
 
Bila moto huu hawa vibendera hawata kuwa na heshima.

Kwanza naona bado bado sanasana zaidi
Mijitu ilimtukana sana Jk
Sasa mazoea mabaya Magu sio Jk

Bila kupotezwa watu hatuta heshimiana

Kwahiyo tumuombe Mungu asaidie wapotezwe watu wa familia yako? maana hakuna ujinga wa hali ya juu kama wako wa kufurahia watanzania kupotezwa kwa maslahi za kisiasa..siku zote siasa ni kupingana
 
Mada iko wazi: tuheshimu sheria na katiba. Kutii sheria bila shuruti ni wajibu ni wajibu wa kila mtu (raia, pokisi, nk). Vile vile kutoheshimu sheria au katiba kwa polisi kuwakandamiza wengine yakiwamo kuwakamata na kuwanyima dhamana kinyume cha sheria na katiba kufikia "si utii wa sheria bila shuruti -- huu ni utovu mkubwa aka jipu lililoiva sana linapaswa kutumbuliwa haraka si la kulea hata kidogo".

Kwa maana nyingine mkuu -- wanaotakiwa kutii sheria bila shuruti ni watu wote wakiwamo polisi pia.

Au wewe huoni hivyo?

Nchi hii itajengwa na sisi sote. Hebu isifike mahali wengine wakadhani wao ni bora zaidi. Sisi sote tu sawa mbele ya sheria na katiba mkuu. Hakuna aliye juu ya hapo.

Vipi wale wanaovunja sheria bila shuruti? maana kuzia watu wasifanye mikutano iliyohalalishwa na katiba ni kuvunja sheria bila shuruti
 
Jana difenda za polisi zimezunguka sana n'a kuwakamata mpka wauza kahawa.......
Watu wanebebwa ......
Kuna jamaa mmoja ana Jina maarufu Kama la rais wanamuita magu naye....alafu ni gamba
Wazeee wakamdandia nayeye hadi kuchezea kichapo....kalala obay katoka leo,
Nyie buku7 msishabikie uonevu yakiwakuta mtabaki kulilia
 
Bila moto huu hawa vibendera hawata kuwa na heshima.

Kwanza naona bado bado sanasana zaidi
Mijitu ilimtukana sana Jk
Sasa mazoea mabaya Magu sio Jk

Bila kupotezwa watu hatuta heshimiana[/
QUOTE]
We utaingia kwenye 18 sijui utawambia oh mm ccm ili wakuachie
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom