Kamata kamata ya Polisi kipindi hiki inalichafua Taifa

Kamata kamata ya Polisi kipindi hiki inalichafua Taifa

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
761
Reaction score
6,985
Mimi Ni mwalimu mstaafu, enzi tunasoma tulikuwa tunafundishwa zaidi kufahamu saikologia ya mwanafunzi. Mfano, ukiwa unafundisha ukabaini yapo Mambo usiyoyajua kitaalamu lakini unaamini wapo wanafunzi wanayafahamu unaelekezwa kutumia mfumo wa mswali na kupitia hayo maswali wewe utajifunza na wanafunzi watajifunza kisha utatumia majibu hayo kwenda kutafuta ukweli nakurejea darasana kipindi kinachofuata ukiwa na majibu sahihi ili ujenge uelewa wa pamoja.

Taifa linapokuwa kwenye msiba mkubwa Kama huu vyombo vingi vya habari vinatusema huku vyombo vya magharibi vikitusema kwa Yale mabaya kuliko mazuri yanayotokea. Kwa saikologia ndogo tu hiki siyo kipindi Cha Polisi kutumia nguvu kupambana na watu ambao ukiwaacha hawana madhara.

Msiba una tafsiri na tamaduni nyingi kiafrika, Kwanza ni Jambo la uzuni lakini kwa wengine ni Jambo la furaha hasa pale wanapokumbuka kuwa hii Ni kazi ya Mungu. Ukienda uchagani maiti usafirishwa kwenye gari lililojaa pombe maana yake safari uambatana na ulevi na mlevi siku zote hana kuuzunika yeye kila kitu ni furaha.

Ukienda mara watu wanacheza ngoma kwenye msiba , kadhalika na hapa kwetu Bukoba ambapo mzee anapofariki wajukuu ucheza ngoma. Hizi zote nitamadumu zilizowekwa kusaulisha machungu nakuwaaminisha kwamba maisha yanaendelea.

Kama tunazotamaduni hizi na Kama tunakubali uwepo wa vyama vingi Basi tuache kupambana na wanaoshangilia adharani kwani wapo viongozi wengi wanalewa sirini kwa starehe zao na wengine wapo kwenye vikao mbalimbali yamkini hata vyakitaifa kipindi hiki.....tuwapotezee walevi na wengine wengi maana kuwakamata nikuwapa Mataifa yenye wivu na wapinzani agenda yakutukosoa kwenye utawala wa awamu ya sita.

Lakini pia kitendo mnachokifanya kinamchafua Rais aliyepo madarakani kwa sababu naamini ajawatuma kuyafanya hayo.
 
Back
Top Bottom