Code zenu tunazijua wakuu na hamuwezi kufunguka maana tayari mmejawa woga kuhusu hatua inayofuata
Wananchi wamechoka ujinga unaoendelea
-------------
Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mkoani Morogoro leo Oktoba 18, 2025, yamefanya mazoezi ya pamoja yenye lengo la kuimarisha mshikamano, ushirikiano na utayari wa kulinda usalama wa wananchi na mali zao
Akizungumza wakati wa mazoezi hayo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama, amesema mazoezi hayo ni sehemu ya maandalizi ya kawaida na yanalenga kuongeza ufanisi wa vyombo vya ulinzi na usalama, siyo kuwatisha wananchi kama ambavyo baadhi ya watu wanavyodhani
Ameongeza kuwa ni muhimu kwa jamii kuelewa kuwa kuwepo kwa mazoezi hayo ni ishara ya utayari wa vyombo hivyo katika kukabiliana na changamoto za kiusalama, hususan kuelekea kipindi cha Uchaguzi Mkuu
Baadhi ya washiriki wameeleza kuwa mazoezi hayo yanasaidia pia katika kuimarisha afya ya miili yao, kuleta mshikamano miongoni mwa vikosi mbalimbali na kujenga ushirikiano imara, unaohitajika katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku
Soma pia GE2025 - Jeshi la polisi na vyombo vya ulinzi Morogoro limefanya mazoezi ya pamoja kuimarisha ushirikiano na usalama kwa jamii
Chanzo: Jambo TV