Kamanda Sirro awajibu waliosusia maiti ya kijana aliyeuawa akihisiwa kuwa jambazi

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
20,382
24,936
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limetolea ufafanuzi malalamiko yaliyotolewa na ndugu za kijana aliyeuliwa na jeshi hilo kwa tuhuma za ujambazi wiki moja iliyopita akidaiwa kujaribu kumpora askari silaha.

Kamishna Simon SirroKamanda wa jeshi hilo Kamishna Simon Sirro amewataka ndugu wa marehemu huyo wakatembelee eneo la tukio kusikia wananchi wanasema nini kuhusiana na kitendo cha kijana huyo ambaye aliuawa na polisi baada ya wenzake kukimbia kusiko julikana.

Amesema katika eneo la tukio palikuwa gari la kubebea fedha lililokuwa likisambaza fedha katika mashine za ATM za CRDB kiasi cha Tsh. 320, 000,00 ambapo mtuhumiwa huyo kwa kushirikiana na wenzake alidaiwa kutaka kufanya tukio la uvamizi katika gari hilo, kabla ya askari kumuwahi na kumuua.

Tangu kutokea kwa tukio hilo, ndugu wa marehemu huyo wamegoma kuchukua mwili wake kwa ajili ya maziko wakidai kuwa ndugu yao ambaye pia alikuwa ni mwanafunzi wa UDSM hakuwa muhalifu, huku wakitaka jeshi hilo liombe radhi kwa kudai kuwa ndugu yao alikuwa mhalifu.

Chanzo :EATV

Kumjua mtu kama jambazi nayo kazi si mchezo.

Hapa mtaani kulikua na jamaa amehamia yeye na familia yake, mtu wa makamo, kama miaka 45 hivi jamaa alikua mhaya kitambi cha kizushi nini na mvi kwa mbali.

Siku fulani tupo na gym master (alishiriki hadi mashindano, the guy was huge) dirishani kwa jamaa, gym master akawa anatukana. Yule jamaa akachungulia dirishani akauliza nani anatukana huyo, gym master kwa kujiamini "Mimi hapa" yule jamaa akatoka na taulo akasema ondokeni dirishani kwangu.
Gym master akasema hatutoki kama unaweza tupige, yule jamaa akaingia ndani akatoka na bukta.

Zikaanza kupangwa, gym master alipigika vibaya mno. Akaona haiwezekani akaenda kumleta rafiki yake, wakapigwa wote.

Siku hiyo tupo gym akatuambia kakutana na jamaa bar Mwenge akanunuliwa bia halafu akamwambia yeye siyo wa kawaida atampoteza bure. Watu tukahisi jamaa usalama.

Mpaka tunakuja kujua kua jamaa jambazi ni baada ya kupiga tukio akauawa na askari, ishu ikaonyeshwa kwenye tv. Ndiyo tukajua kumbe alivyosema mtu mbaya alimaanisha nini.
 
Nchi yetu ingekua na mfumo wa kamera barabarani na maeneo yanayokua na mikusanyiko bila kusahau maeneo maalum km bank, vituo vya mafuta n.k and ngekua rahisi kubaini nani msema kweli. Kwasasa ni kukandamizana tu, bora liende.

Ingawa haki ya mtu haipotei Ila akishapoteza uhai ni km imepotea pia.
 
Ni ujinga kwa familia kushikilia msimamo kuwa ndugu yao sio mhalifu ukiwa wao hawana utaalamu wa kumgundua mhalifu.
Sio lazima jambazi awe mvuta bange, pombe, mkorofi n.k.
Mtu anaweza akawa ajambazi lakini familia isijue chochote tena anaweza kuwa ni mtu wa heshima sana nyumbani.

Haya mambo mengine tusitetee hovyo, hivi kama hawakuwa majambazi kwanini wenzake walikimbia??
Wangeuwawa polisi badala yake je tungesema kuwa police hawana weledi na kazi yao??

Ni kwanini siku hizi wahalifu wanatetewa sana??
Zingeibiwa hizo pesa mngesemaje??

Huu ujinga utatufikisha pabaya sana huu.
 
Kumjua mtu kama jambazi nayo kazi si mchezo.

Hapa mtaani kulikua na jamaa amehamia yeye na familia yake, mtu wa makamo, kama miaka 45 hivi jamaa alikua mhaya kitambi cha kizushi nini na mvi kwa mbali.

Siku fulani tupo na gym master (alishiriki hadi mashindano, the guy was huge) dirishani kwa jamaa, gym master akawa anatukana. Yule jamaa akachungulia dirishani akauliza nani anatukana huyo, gym master kwa kujiamini "Mimi hapa" yule jamaa akatoka na taulo akasema ondokeni dirishani kwangu.
Gym master akasema hatutoki kama unaweza tupige, yule jamaa akaingia ndani akatoka na bukta.

Zikaanza kupangwa, gym master alipigika vibaya mno. Akaona haiwezekani akaenda kumleta rafiki yake, wakapigwa wote.

Siku hiyo tupo gym akatuambia kakutana na jamaa bar Mwenge akamnunuliwa bia halafu akamwambia yeye siyo wa kawaida atampoteza bure. Watu tukahisi jamaa usalama.

Mpaka tunakuja kujua kua jamaa jambazi ni baada ya kupiga tukio akauawa na askari, ishu ikaonyeshwa kwenye tv. Ndiyo tukajua kumbe alivyosema mtu mbaya alimaanisha nini.
Master fake huyo
 
Hahaaaaa gym master na Rafiki yake kipigo
 
Hyo kauli nenda kamwambie kamanda Sirro. Kutetea majambazi ni kazi ngumu sana.
Kama nape na malima walitolewa silaha,unadhani wewe ukiuliwa bahatimbaya itaitwaje?polisi juzi wametoa listi ya majambazi waliouwa polisi,swali hao vijana 50 waliowawa hadi sasa nao ni kwanini? Tukikubali ujinga huu tutaendelea kuokota maiti nyingi mtoni tukisema ni wakimbizi, polisi hivi sasa wamevuka mpaka akiambia toa hela wewe mpe tu ukibisha anaweza kukupiga risasi na kusema ulikuwa unataka kumpora silaha,kuna kitu kinaitwa extrajudicial killings tukiruhusu kwa watu wenye dola hamna atakaekuwa salama.
 
Kumjua mtu kama jambazi nayo kazi si mchezo.

Hapa mtaani kulikua na jamaa amehamia yeye na familia yake, mtu wa makamo, kama miaka 45 hivi jamaa alikua mhaya kitambi cha kizushi nini na mvi kwa mbali.

Siku fulani tupo na gym master (alishiriki hadi mashindano, the guy was huge) dirishani kwa jamaa, gym master akawa anatukana. Yule jamaa akachungulia dirishani akauliza nani anatukana huyo, gym master kwa kujiamini "Mimi hapa" yule jamaa akatoka na taulo akasema ondokeni dirishani kwangu.
Gym master akasema hatutoki kama unaweza tupige, yule jamaa akaingia ndani akatoka na bukta.

Zikaanza kupangwa, gym master alipigika vibaya mno. Akaona haiwezekani akaenda kumleta rafiki yake, wakapigwa wote.

Siku hiyo tupo gym akatuambia kakutana na jamaa bar Mwenge akamnunuliwa bia halafu akamwambia yeye siyo wa kawaida atampoteza bure. Watu tukahisi jamaa usalama.

Mpaka tunakuja kujua kua jamaa jambazi ni baada ya kupiga tukio akauawa na askari, ishu ikaonyeshwa kwenye tv. Ndiyo tukajua kumbe alivyosema mtu mbaya alimaanisha nini.
Kama sijakosea ilikuwa 2008 kinondoni mkwajuni ilikuwa siku ya ijumaa jamaa mmoja alikuwa mwanafunzi wa kidato cha sita anatembea pembezoni ya barabara akimshika mkono mdogo wake cha kushangaza polisi walimpiga risasi na akafa hapo hapo wakisema ni jambazi ,na magazeti yote kesho yake yakamwandika ni jambazi ila familia yake waliweka ngumu polisi baadae wakaomba msamaha na magazeti yakamsafisha siku iliyofuata lakini ilikuwa too late ,

Roho yake iliondoka kimakosa
 
Back
Top Bottom