Kamanda Muliro: Malisa GJ, Boniface Jacob wakamatwe kwa tuhuma za kupotosha taarifa za kifo cha Robart Mushi

Tangu Lini Mochwari za Polisi zikaanza kutunza Maiti za Raia waliokufa kwa ajali ? Huyu Muliro hana hata haya kusimama mbele ye Media na kuwahadaa wananchi ?
 
Labda walitaka kuufanya uwe cadaver ( dead human body used in scientific and medical research).

Bure kabisa Hawa jamaa yaani wamekaa na maiti karibu week 2 bila kutoa taarifa wanaona sawa tu.
 
Eti Amana mochwari ilijaa wakampeleka Hospitali ya Jeshi la Polisi ??? Kwa nini hakupelekwa mUhimbili au hospitali ya Temeke ???
Hii kesi nyepesi sana kwa ex mayor Jacob

Inafikirisha sana ,halafu kumbuka kwamba ndugu walitoa taarifa vituo vya polisi na pia walizunguka hospital kubwa kubwa mochwari ,lakini polisi wala hawakukumbuka kusema kwamba waje kuangalia mwili pindi ndugu walivyotoa taarifa ,zimepita karibia wiki mbili ndiyo wanakuja kusema.
 
Napata ukakasi kama Amana ilijaa nimaiti ngapi ziliamishiwa hospitali ya polisi siku hiyo au alikufa Robert tuu kama Kuna mwingine watuambie na wao walipekwa huko au muhimbili hata lugaro!
 
Nafikiri Kamanda Muliro anapaswa kuona aibu kuzungumzia baadhi ya Mambo yanayolichafua Jeshi la Polisi kama tukio hili. Wakati mwingine kukaa kimya ni busara na hekima zaidi kuliko kutoa taarifa ambayo inazua utata mkubwa ktk jamii sambamba kukuondolea credibility ktk jamii hiyo.
 
Ila ukisikiliza maelezo ya Kamanda Muliro, kuna namna Jacob kakosea. Inaonyesha kuwa hata ndugu zake na huyo Marehemu wamekubaliana na maelezo ya Polisi.
Ndugu wepi hao wanaokubaliana na maelezo ya Polisi???
Tukubali tu ukweli kwamba tukio hili lina ukakasi na utata mkubwa sana. Kwa vyovyote itakavyokuwa Jeshi la Polisi haliwezi kukwepa kuhusishwa moja kwa moja na Kifo cha huyu mtu kwa sababu maiti ya huyo mtu 'imekutwa ndani mwao.' Ukikamatwa na ngozi lazima ueleze nyama iko wapi au nyama kala nani!
 
Inasikitisha Serikali kutumia kodi zetu Kumsafirisha Malisa G.J hadi Moshi kwenda kufanya Upekuzi.

Yaani Polisi wanafikiria wakienda moshi watapata ushahidi wowote? Kama ndugu wanajua polisi wanakuja si watatoa kila kitu wabakize makochi na vitanda tu ndani?
 
Na wanajua baba yake Malisa GJ ni Inspekta mstaafu anajua figisu zao zote.
 
Na wanajua baba yake Malisa GJ ni Inspekta mstaafu anajua figisu zao zote.

Kabisa yaani sijajua wamewaza nini kuchoma mafuta hadi Moshi labda wanafanya tour na kulamba Over Time tu.,,nina uhakika 100% hawakuti chochote huko.

Ila Boniface mafia wamemuibukia saa saba usiku lakini walimkosa hahaaaa
 
Imekuaje tena huko mkuu hebu tuhabarishe
 
Baada ya polisi kumuua Mushi, walienda kuuhifadhi mwili wake kwenye mochwari ya polisi kwa sababu walipompeleka Amana madaktari waliwaomba PF3 wakashindwa kutoa. Na wasingeweza kutoa PF3 kwa kuwa ni wao wenyewe waliomuua. Hivyo, wakaona isiwe tabu wakapeleka mwili kwenye mochwari ya polisi ambayo haina maswali mengi.

Wakati ndugu wanatafuta mwili wa ndugu yao, polisi waliuficha na kukaa kimya kwa kuwa bado walikuwa hawajamaliza kutunga uwongo. Baada ya kumaliza kutunga uwongo ndipo wakasema mwili wanao wao.

Mungu hadhihakiwi. Jiwe alikuwa anauawa watu na kuwafunga kwenye viroba anaenda kutupa baharini. Alimkosakosa Tundu Lissu hivi sasa natembea kwa kuchechemea huku akiwa amejaa vyuma mwili mzima. Hata General Bokasa na madikteta wengine kama Idd Amini na Foday Sanko, waliua mamilioni ya raia wasiokuwa na hatia lakini leo hii wapo kaburini wameoza imebaki mifupa tupu. Na hata huenda mifupa mingine imeoza limebaki fuvu tu.

Hawa polisi wanaowaua raia na kisha kutunga uwongo na kuuhadaa umma, nao kiama chao kinakuja na watakuja kufa vifo vibaya sana. Mungu hadhihakiwi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…