Kamanda Mawazo ameuawa na Mfumo wa Jeshi la Polisi - Lema

Kamanda Mawazo ameuawa na Mfumo wa Jeshi la Polisi - Lema

Godbless J Lema

Arusha MP
Joined
Sep 28, 2013
Posts
92
Reaction score
2,205
Kamanda Mawazo ameuawa na Mfumo wa Jeshi la Polisi

Alikuwa kijana aliyeamini katika Mabadiliko, alitembea Nchi nzima kwa shida kujenga ufahamu kuhusu Ukweli, Haki na Usawa. Ameuwawa akiwa akitoka kwenye kazi za Chama chake, akavamiwa, akapigwa na baadae kufariki. Ni nani amefanya kitendo hiki?

Watu wengi mnalaumu Wanachama wa CCM kwani ndio waliofanya kazi hiyo, hapana, mnakosea. Mawazo ameuwawa na mfumo wa Serikali na Jeshi la polisi unaojali ukatili na uovu. Mauaji yataendelea sana, kwani wengi wamekishauwawa na kuumizwa bila Serikali kuchukua hatua.

Polisi wanaowajibika kwa utawala unaojali ukatili, ubaya, na uovu ni lazima watamsaidia Shetani kufanya kazi. Polisi wanaoshindwa kukamata wahalifu na na kuwajibisha wahalifu, wao ndio wanaosaidia Taifa hili kuingia Vitani, Matukio ya Green guard kuvamia na kujeruhi na hata kuua ni mengi katika Taifa hili, Wahalifu wanalindwa na sasa wana ujasiri wa kufanya wanavyotaka. Sioni siku nyingi za Amani Tanzania, magari ya kuwasha na silaha za moto zitashindwa kupambana na Umma uliojawa hasira na Uchungu, propaganda pia zitashidwa kutengeneza hali ya usalama, masikitiko yangu ni kuwa hali hii itamkuta kila Mtu aidha ni mwenye haki au ni asiye na haki. Usalama wa Nchi haujengwi na wingi wa silaha wala wingi wa Askari, Isipokuwa utawala unaojali Haki na Usawa.

Uhalifu wa namna hii katika Taifa hili unajengwa na Polisi walioshindwa kazi zao kwa kuzingatia Uadilifu na Sheria za kazi, Kamati za Siasa za Chama Tawala ndio zinatoa maelekezo ya utendaji wa Jeshi la Polisi. Kwa mfano hapa Arusha RPC ni mdau namba moja wa CCM na hivi karibuni katika vikao vyake vya kampeni ya kumsaidia mgombea Ubunge wa CCM alichokaa na Viongozi wa bodaboda alitoa maelekezo mabaya na ya uharibifu dhidi yangu, unafikiri nini? Ni lazima Vijana hawa kama watakosa Utu, wanaweza kufanya uhalifu mbaya sana kwangu, kwani anayepaswa kulinda amani ndiye anayesimamia Mipango mibaya ya uhalifu.

Mambo haya ni lazima yafike mwisho. Polisi mnapaswa kuwa na hekima sasa na mtambue kuwa hali ya Usalama Nchini haiko salama, Watoto wenu, Wazazi wenu, Wake zenu na familia zenu ziko Mitaani, Ukatili na Uonevu unapoongezeka kwa Watu wanyonge, ndivyo hivyo Watu hawa wanaanza kufikiria njia mbadala ya kujitetea, naona Binadamu wa Tanzania anaanza kuelekea huko.

Ni nani anafuata baada ya Mawazo? Ni vita ya kujilinda au kukubali kuwa Maiti kwa njia ya mapanga na vipigo? Tulitafakari jambo hili wote, kwani Utulivu huu tulionao hauna muda mrefu kutoweka na ndipo Nchi yetu itakuwa Nchi ya Ukiwa.

Moyo wangu umeumia na kuchoka sana nahitaji msaada zaidi, Ni Kijana rafiki mzuri niliyemuingiza kwenye Siasa, nilimpa Suruali, Mkanda, na Koti wakati ninampleka kumtambulisha kwa ajili ya kura za maoni kwenye Chama cha Tlp wakati huo, tuliishi wote na familia zetu zikapendana sana, hakuwahi kuwa mnafiki juu ya anachokipigania.

Mawazo umeuwawa? Kosa lako ni kuwa CHADEMA na kufanya Siasa? Mkuu wa Wilaya ya Geita atafurahi sasa, kwani alishawahi kutamani kuona maiti yako na leo ameshuhudia, Rafiki zako tunatafakari kwa kina na Uchungu mkubwa.

Ni heri Vita inayotafuta Haki na Usawa kuliko Amani inayopumbaza na kudhalilisha Utu wa Binadamu.

Nilikuwa nakupenda sana Mawazo.

Godbless Jonathan Lema
 
Waliofanya tuko hili wakamatwe Mara moja na sheria ichukue mkondo wake,
Kwani hakuna mwanadamu mwenye mamlaka ya kutoa uhai wa mwenzake.

Police fanyeni kazi yenu kwa weredi wenu na kwa kutumia intelijensia yenu kuwanasa wote waliohusika na tukio hilo.
Ili kuondoa mtazamo hasi juu ya jeshi letu lenye dhamana ya ulinzi wa raia na mali zao.

Siasa hizi za mauaji zikomeshwe Mara moja kuendelea kuzifumbua macho ni kulitumbukiza taifa letu kwenye machafuko.
Wananchi wote tuwe watulivu wakati jeshi la police likifanya kazi yake.
 
Maneno haya hameniumiza sana kwa kweli, nenda kamanda Mawazo Nenda.
 
Jamani Mbona hakuna anayeeleza kisa cha yeye kuvamiwa? Yeye kama mwananchi anaweza tenda kosa kwahiyo msikimbilie kwenye nafasi yake bila kueleza mkasa mzima.
 
Na nyie viongozi wa ukawa mmekaa kimya sana , toeni tamko kieleweke sio kulia lia kwenye social media,
 
Kamanda Mawazo kauawa na Polisi na inajulikana,najiuliza hivi hawa Polisi wetu ni Watanzania?na kama ni Watanzania wanapigania nini?nasema wazi watatumaliza wote ili wabaki wenyewe,lakini kabla hawajatumaliza haki itachukua mkondo wake na ndipo Taifa langu Tanzania litainuka kutoka kwenye mavumbi,Mungu M;laze pema Kaka yangu Kamanda Mawazo!
 
YATQKUWA KAMA YA MWandishi MWANGOSI NA DR ULIMBOKA CCM HOVYO KABISA LAZIMA NCHI INAHITAJI UKOMBOZI HUU NI UHUNI
 
Pumzika kwa Amani kamanda wako, watesi wako wote waliokutendea ubaya Mungu atawaonyesha peupe
 
Nasikitika kuona taifa langu kupoteza amani.tambua rwanda nao walianza hivo. Mda si mrefu uvumilivu utakoma ju ya uovu.
 
Kweli LEMA umenena! Nahisi nguvu kunipungua mwilini. Natafakari sana juu ya kodi yangu na kazi yake kwangu kuhusu usalama. Jeshi letu la ccm wamejisahau na kuwa nao chama cha siasa. Si jeshi la polisi tena bali ni la ccm. Ukitaka kuwajua ikosoe ccm watafik
 
Taarifa ya polis I unaiamini sana?? utasikia amepigwa na kitu kizito! aliyemteka Ulimboka ni mkenya, hakuna cha kusubiri taarifa ya polisi ,
 
Kamanda Mawazo kauawa na Polisi na inajulikana,najiuliza hivi hawa Polisi wetu ni Watanzania?na kama ni Watanzania wanapigania nini?nasema wazi watatumaliza wote ili wabaki wenyewe,lakini kabla hawajatumaliza haki itachukua mkondo wake na ndipo Taifa langu Tanzania litainuka kutoka kwenye mavumbi,Mungu M;laze pema Kaka yangu Kamanda Mawazo!

Ushahidi wa uongo sio mzur,uko dar huko umejifichavnyuma ya keybord unajiandikia tu unachohisi then anatoa ushuhuda,acheni siasa huu ni uhalifu kama uhalifu mwingine
 
Tunaomba kujua mazingira vizuri ya kuuawa huyu kamanda, taarifa ziko sahihi ila namna alivyouawa ndiyo hatujui. Je alitekwa?? Na alikuwa peke yake?? Muda gani??? Maeneo gani??? Hapa wahalifu lazima wapatikane tu na sheria ichukue mkondo wake.
 
Back
Top Bottom