Kamanda Mambosasa: Mwandishi Erick Kabendera anahojiwa uraia wake

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
Kamanda Mambosasa anasema:

Erick Kabandera alikamatwa nyumbani kwake baada ya kukataa wito halali wa Jeshi la Polisi

Awali aliandikiwa barua ya wito ajili ya mahojiano lakini alikaidi kutii wito halali wa Polisi

Jeshi la Polisi likimwita mtu kwa hiari akikaidi, sisi tunamwezesha atii

Baada ya kukamatwa tumesikia watu mbalimbali wakidai ametekwa. Niseme hajatekwa lakini kwa jeuri akawa amekaidi kutii wito.

Aliitwa kuhusiana na Utata wa Uraia wake. Kwa kushirikiana na Uhamiaji, tunafuatilia uhakika wa uraia wake pale atakapotoa vielelezo mbalimbali kuthibitisha uraia wake. Sasa tunaye, taratibu nyingine za kiupelelezi zinaendelea.

Hajatekwa, amekamatwa na tunaye Central Police.

Upelelezi unaendelea, tukikamilisha upelelezi matokeo ya upelelezi ni kupelekwa mahakamani

Kwakuwa alikaidi wito, hatukuwa na namna zaidi ya kumkamata na kumshikilia

=====

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUKAMATWA KWA ASKARI BANDIA ALIYEVALIA CHEO CHA MKAGUZI MSAIDIZI WA POLISI.

Jeshi la Polisi kanda maalum Dar es Salaam linamshikilia DAUDI RAMADHANI IDDY (23) mkazi wa Tabata Segerea kwa kujifanya ofisa wa Polisi, akiwa amevaa sare za Jeshi la Polisi na cheo cha mkaguzi msaidizi wa Polisi( Assistant Inspector).

Mnamo tarehe 19.07.2019 Jeshi la Polisi lilipata tarifa toka kwa askari wa Jeshi la kujenga taifa (JKT) makao makuu Mlalakuwa, kuwa kuna kijana mmoja amevaa sare za Jeshi la Polisi wana mashaka naye.

Makachero wa Jeshi la Polisi walifika makao makuu ya JKT Kumkamata na kufanya naye mahojiano,mtuhumiwa alikiri kujifanya yeye ni afisa wa Polisi na kufanya utapeli.

Pia alikiri kupitia mafunzo Jkt huko Mafinga mwaka 2006 na kujitolea kwa mujibu wa sheria katika kambi hiyo.

Mtuhumiwa alifanyiwa upekuzi na kupatikana na vifaa vifuatavyo;
1.sare moja ya Polisi aina ya kaki

2. vyeo vya(Cpl, Sgt na cheo cha mkaguzi msaidizi

3 pea moja inaya kombati Jungle green.

4.pingu moja.

5.kofia moja ya askari wa usalama barabarani.

6.radio ya upepo moja aina ya motorola.

7 mikanda miwili ya Jkt.

8.mkanda mmoja wa bendera wa Jeshi la Polisi, buti na viatu vya kawaida.

Upelelezi wa kina unaendelea na mtuhumiwa atapelekwa mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili.

KUKAMATWA KWA MWANDISHI WA HABARI.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linamshikilia ERICK KABENDERA, (39) mkazi wa Mbweni, Mwandishi wa habari, kwa mahojiano.

Mnamo tarehe 29/07/2019 mtuhumiwa alikamatwa nyumbani kwake na Jeshi la Polisi baada ya kukataa wito wa Jeshi la Polisi.

Aidha mwandishi huyo awali aliandikiwa barua ya wito kufika Polisi kwa ajili ya mahojiano lakini alikaidi wito huo.

Ndugu waandishi wa habari niseme utii wa sheria bila shuruti ni muhimu sana kuzingatiwa kwani ukishindwa kutii sheria inakuwa shuruti. Baada ya kukamatwa mwandishi huyo tumesikia taarifa mbalimbali zikisambaa kuwa mwandishi huyo ametekwa, niseme kuwa mwandishi huyo hajatekwa ila tumemkamata kwa mahojiano. Aidha mtuhumiwa huyo kuna mashaka makubwa kuhusiana na uraia wake tutakapobaini mara moja tutamkabidhi kwenye idaya ya uhamiaji ili kushughulika naye na ndiyo maana alikuwa akikaidi wito wa polisi na kujihami kuwa ametekwa.

LAZARO B. MAMBOSASA – SACP KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAM.
30.07.2019
 
Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam nchini Tanzania limesema litatoa taarifa inayomhusu Mwandishi wa habari za uchunguzi, Erick Kabendera ambaye alichukuliwa kwa nguvu na watu waliojitambulisha kwamba ni polisi nyumbani kwake nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam eneo la Mbweni.

Kabendera ambaye anaandikia magazeti ya ndani na nje ya Tanzania alichukuliwa jana jioni Jumatatu Julai 29, 2019 na watu hao walioieleza familia yake kwamba wanampeleka Kituo cha Polisi Oysterbay, Dar es Salaam.

Leo asubuhi Jumanne Julai 30, 2019, Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema atatoa taarifa kuhusiana na swala hilo saa saba mchana.

"Nitatoa taarifa rasmi saa saba mchana karibu Kanda Maalum kwa sasa siwezi kuzungumza chochote" amesema Mambosasa

-----
Mwandishi Erick Kabendera anashikilliwa kwa mahojiano. Tarehe 29/07 alikamatwa baada ya kukataa barua ya wito. Awali aliandikiwa akakaidi. Utii wa sheria bila shuruti ni muhimu. Kila mmoja anazingatia kutii sheria na witoPolisi tunapomuita akakaidi, tunamuwezesha atii.

Baada ya kukamatwa mwandishi huyo tumesikia taarifa mbalimbali wakiendelea kusema mwandishi huyo ametekwa. Niseme mwandishi huyo hakutekwa, ameitwa akakaidi.

Sababu ya kumuita ni kuhusiana na utata wa uraia wake. Jeshi la Polisi linashirikiana na Uhamiaji kuprove kama ni Mtanzania.

Yupo mikononi mwetu na yupo salama hakutekwa.Niwaambie tu kwamba usipofanya research huna sababu ya kusema. Kabendera Yupo kituo ninachokiongoza mimi. Kama unataka kumuona yupo Central

Niwaase watanzania, tufikie mahali tusikimbilie kwenye mitandao, mitandao inapotosha na inazua taharuki.Hawatuulizi, sisi tunaamua kukaa kimya waongee ili sisi tuje kutoa taarifa

Kukamatwa utaratibu ilifuatwa wa kumkamata Erick.
 
Mtandao wowote utakaovujisha siri za wateja au Kushirikiana na watekaji ni wa kuususia.Wamekiuka Sheria ya faragha
 
Aeleze kuna ugumu gani kufuata sheria ya kumkamata mtu - ama kwa mahojiano au kwa jinai iliyokwisha chunguzwa!
 
Dunia ya sasa huwezi teka MTU usijulikane,washamba tu ndo ufanya mambo ya kishamba.Ndumba haiwezi shindana na teknolojia
 
Back
Top Bottom