Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,495
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Suleiman Kova amesema marafiki wengi wa viongozi si marafiki wa kweli bali ni marafiki wa zile nafasi walizonazo.
Kamanda Kova alisema hayo katika uzinduzi wa Chuo Cha Fursa (APEC) kilichopo maeneo ya Ukonga, mwishoni mwa wiki ambapo mkurugenzi wa chuo hicho alimualika kuhudhuria hafla hiyo.
“Mkurugenzi wa APEC, Respicius Timanywa, alikuja ofisini kwangu mwaka 2010 akitaka ushauri na kupata maelekezo kuhusu mtaala wa kufundishia bodaboda, tuliandaa pamoja naye, leo amenikumbuka kanialika katika uzinduzi wa chuo,” alisema Kamanda Kova.
Aliongeza “Ni watu wachache sana wanaoweza kukumbuka, wengi ni marafiki wa kiti chako sio wewe, ukitoka katika kiti ukimpigia simu hapokei na mwingine anaitika kisha anazima kabisa.”
Aidha Kamanda huyo alisema kwa sasa anajishughulisha na kutoa ushauri wa masuala ya maafa, majanga na uokoaji.
Source: Bongo 5