Kamanda Kova, Je Kundi la Al shabaab limekufa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamanda Kova, Je Kundi la Al shabaab limekufa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Patriote, Dec 9, 2011.

 1. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #1
  Dec 9, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Wahenga walisema njia ya Muongo ni fupi, yapata wiki mbili zilizopita wakati wanaharakati wakiwa na mpango wa kuandamana kupinga malipo kwa Mafisadi wa Dowans. Kamanda Kova alituambia kuwa serikali ilisitisha maandamano yale kwa sababu ya matishio ya Al-shabaab.

  Jana/Leo hii wakati Tanganyika inaadhimisha miaka hamsini ya uhuru hatujamsikia Kova wala Serikali ikizuia wananchi kufanya mikusanyiko sehemu mbalimbali ambako maadhimisho hayo yanafanyika. Je Kova na wenzake waliwasiliana na Al shabaab kuwa leo wasifanye milipuko???je Serikali inamahusiano ya Al Shabaab na ndo mana waliweza kujua kuwa siku ya maandamano ya Dowans wangelipua watu na leo wasingelipua watu????

  Kimsingi Kova alifanikiwa kutumia madaraka yake vibaya na kuamua kuzuia haki ya msingi ya raia kuandamani na kudai haki yao tena kwa sababu ambazo naweza kuziita ni za kijinga na zakitoto kwa mtu mzima kama yeye kuzitumia.Kimsingi alijidhalilisha kwa kujamba mawazo mbele la umma. Nionavyo mimi Kova amejipambanua kuwa ni mmoja wa wanachama wa Genge la Mafisadi wanaoitafuna nchi na ndio maana alijitahidi kuzima maandamano yale hata kwa kutoa sababu za kijinga ili kuwafurahisha mafisadi na mabosi wake kwa gharama ya haki za wananchi.

  Hivi kwanini tusifikirie kuweka utaratibu wa namna ya kuwajibisha viongozi wanaotumikia Mafisadi badala ya Wananchi wanaowalipa mishahara kupitia kodi zao???
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Dec 9, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  A million dollar question that is begging for an elaborated answer that staggers on hinges of infringement of constitutional fundamental human rights of speech, assembly and association in Tanzania.

  Why the selective administration of order and justice like this in our country?
   
 3. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #3
  Dec 9, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,312
  Likes Received: 5,599
  Trophy Points: 280
  Hujui Kova na Mwema ni makada wa magamba??na wana kadi??subiri wakimaliza madaraka yao uone wakigombe aubunge na kusema walikuwa wanachama hai....tokea 1977!!utashangaa
   
 4. M

  Magarinza Senior Member

  #4
  Dec 9, 2011
  Joined: May 9, 2008
  Messages: 122
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kova ni mpuuzi m1 tu ivi anayeshiriki kikamilifu kufanya siasa uchwala.
   
 5. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #5
  Dec 9, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,269
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  watakuja na majibu mepesi sana.. Utawasikia

  1. Tishio halikuwa kubwa sana
  2. Tulituma vijana kuimarisha usalama
  3. Alshabaab walikuwa likizo
  4. Alshabaab walienda show ya viduku
   
 6. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #6
  Dec 9, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  CCM na Al-Shabaab ni kitu kimoja kumbuka taarifa ya mwakyembe ambayo kimsingi mpaka leo si mwema wala mkama wameshatoa maelezo ya kukanusha kujihusisha na kundi hilo...
   
 7. King2

  King2 JF-Expert Member

  #7
  Dec 9, 2011
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 1,289
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Unamaanisha mr. MIKENGEZA.
   
 8. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #8
  Dec 9, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Haa haa haa, kweli hawa viongoz wetu wanadhani wao ndo wanafikiria kuliko mwananchi wote.Na ndiyo maana wakishafikiria kwa uwezo wao wote tena baada ya kupewa ushauri na wasaidizi wao, wanapanda majukwaani na kututangazia upupu kwa kudhani kuwa wananchi hatuna fikra na uelewa. Kumbe wao ndio viazi kbs, ila JK inaonekana anawakubali sana, nadhan itakuwa anawaelewa au nayet ana mawazo kama yao. Dah kwa kweli sipo proud kabisa of my country chini ya utawala wa hawa wezi, mafidasi na shallow thinkers.
   
 9. only83

  only83 JF-Expert Member

  #9
  Dec 9, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Al-shabab hawafanyi mashambulizi kwa viongozi wa CCM na serikali yake maana ni kama maji na samaki..alshabab na CDM ni kama petroli na maji......
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Dec 9, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  yawezekana kabisa kova ni aishababu ndio maana anajua lini watatishia

  Mrangi anatia aibu sana yule
   
 11. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #11
  Dec 9, 2011
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Al-Shabaab huwa hawagusi kabisa kwenye mikusanyiko yenye watu waliovaa nguo za kijani mkubwa
   
 12. mpinga shetani

  mpinga shetani JF-Expert Member

  #12
  Dec 9, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 3,268
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  hivi hamkuona tulivyojaza vifaru pale stadium? ilikuwa ni kujikinga na Al ... Al ... eh, Al nini tena?
   
 13. N

  Ngoiva JF-Expert Member

  #13
  Dec 9, 2011
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 236
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  teh teh teh! Juzi kova kafungua ghala na kuchukua risasi 240 na bunduki 5 za kiviti, kama kawaida press conference, ''tumewakata majambazi 12 sugu wa drs. Jamani saikolojia za kitoto. Eti kuthibiti uhalifu kipindi hiki cha kusheshekea miaka 50.
   
 14. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #14
  Dec 9, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  NINI SIRI YA UTAJIRI WA KUPINDUKIA WA MA-IGP WETU WA ENZI ZA VYAMA VINGI HIZI UNAOKINZANA KABISA NA HLE YA WENZAO KATIKA CHEO HICHO HICHO LAKINI ENZI ZA CHAMA KIMOJA TANZANIA?

  Duh, mkuu umenikumbusha mbaali sana kuhusu zile sanaa za msanii maarufu nchini enzi hizo kwa jina la Omar Mahita.

  Kama kuna mtu alituchezea akili nchi hii na kutufanya tukichukie kabisa Chama Cha Wananchi CUF (licha ya kuwemo Mtambo wa enzi hizo - Prof Lipumba), mtu huyo ni yule Kada wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro Alhaji Omar Mahita, ambaye hivi sasa ni tajiri wa kupindukia akiendesha biashara ya msururu wa mabasi ya BUFFALO kote nchini eti alizozinunua KWA MSHAHARA TU WA KI-POLISI hata kabla ya kustaafu na kupewa kiinua mgongo.

  Ndio, ni hizi hizi janja za Kova alizokua nazo huko Rungwe, Chunya na Tunduma huko ndizo hizo ambazo hata naye Alhaji alizitumia kukiua kabisa CUF huku bara.

  Basi mambo yakawa vurugu tu fujo tu mara leo aibuke na mitoroli ya mapanga yaliopakwa TOMATO SAUCE na kutuaminisha kwamba CUF ni chama cha fujo na kwamba kinachinja watu, mara kesho CUF Ngangari na yeye Ngunguri - basi ikawa ni sinema tuuuu hadi anapomaliza mchezo akiwa tajiri kuliko hata Ndg Regnald Mengi mfanyabiashara aliyeagana na usingizi mwanana siku nyingi ili apate tu kugema kile tu kilicho chake ki-halali.

  Wanabodi, kumbukumbu zangu hizo zinatufikisha hadi kwenye swala mama la: INAAKUA VIPI MA-IGP WA JESHI LA POLISI ENZI HIZI ZA VYAMA VINGI HUSTAAFU WAKIWA NA MALI KUZIDI KI-PATO CHAO MARA 100 ZAIDI UKILINGANISHA NA WENZAO WALIOWAHI KUSHIKA WADHIFA KAMA HUO HUO LAKINI CHINI YA CHAMA KIMOJA??

  Mzee Jenerali Ulimwengu, Saed Kubenea, na Steven Chuwa na Maggid Mjengwa mpo hadi hapo?????????????? Kwa kuweka tu sawa rekodi, IGP Mstaafu (enzi za chama kimoja) Mzee Mgaya ni mtu wa kawaida kabisa kule Msasani tena kwa kujibidisha kwa tu ili asiadhirike na maishi kaamua kuwa Mlinzi Mkuu wa kampuni tu ya Ulinzi iliokua Group Four pale Masaki kwa maana ya kuwa mjumbe wa bodi tu ili mkono uende kinywani.

  Je, hawa wenzake akina Omaari Mahita na wengine wanaoendelea kushika wadhifa huo ni kwamba wamegundua mgodi gani pale Wizara yetu ya Mambo ya Ndani mpaka watajirike kuliko hta waziri mwenye dhamana?

  Au bidha wanayoiuza pale ndio hizi hizi ya 'NIKINGE VEMA NA HAO AKINA HAJJI DUNI NA KAMANDA LEMA' na baadaye nitakutupia jicho kukufanya ADADI RAAJAB Ubalozini au tukamalizana kabisa Cash Cash mkononi kama huna talanta ya mambo hayo ya kidiplomasi kama Omari Mahita??????


   
 15. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #15
  Dec 9, 2011
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Al Shabab na CCM ni ndugu moja. Kwanini serikali ya Tanzania haijapeleka majeshi yetu somalia kusaidiana na majeshi ya Kenya + Uganda kupigana na Al-Shabab?. Kuna vijana wa ki-tanzania walishikwa huko Somalia wakiwa ni wapiganaji wa Al-Shabab na wakarudishwa Tanzania, je wamechukuliwa hatua gani na serikali tawala?. Kuna kambi za kuandikisha na kutoa mafunzo kwa vijana hawa wa Al-shabab hapa Tanzania na serikali inalijua hilo.
   
 16. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #16
  Dec 9, 2011
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,638
  Likes Received: 2,872
  Trophy Points: 280
  Aliwahi kusema al-shabab wanawatarget zaidi wanaharakati !!
   
Loading...