Kata ya Buyuni – Mtaa wa Nyeburu, Barabara ya Mchimbo (Maarufu Kwa Baba Esther)
Sisi wananchi wa Kata ya Buyuni, Mtaa wa Nyeburu, tunapenda kuwasilisha taarifa ya kero inayotusumbua kwa muda mrefu katika eneo letu, hususan barabara ya Mchimbo maarufu kwa jina la Kwa Baba Esther.
Eneo hili limekuwa chanzo cha usumbufu na vitendo visivyofaa, ikiwemo:
1. Uvutaji wa bangi hadharani.
2. Kukusanyika vijana wadogo, wakiwemo waendesha bodaboda ambao wengi hawajafikia umri wa kuendesha vyombo vya moto.
3. Kutukana matusi makubwa, kupiga muziki kwa sauti kubwa kupitia pikipiki bila kujali muda wa usiku au mchana.
4. Vurugu na ugomvi unaohusisha visu.
5. Michezo ya kamari mbalimbali.
6. Watoto wadogo na wanafunzi kushinda wakicheza PlayStation na kamari ya Dubwi uliowekwa katika eneo hilo, hali inayowaathiri kitaaluma na kimaadili.
Wananchi wa eneo hili tayari waliwahi kutoa taarifa kwa mjumbe wa mtaa pamoja na kuwasiliana na askari kata wa Buyuni, lakini hadi sasa hakuna hatua yoyote madhubuti iliyochukuliwa.
Kwa kuwa hali hii inazidi kuhatarisha amani, maadili na usalama wa jamii, wananchi tunaendelea kusisitiza kuwa tatizo hili lichukuliwe hatua haraka ili kurejesha utulivu na ustawi wa eneo letu.