Kama wewe ni mwanaume kuna mambo hupaswi kumuita fundi

Unasemeje

JF-Expert Member
Apr 29, 2021
249
915
Mwanaume kuna mambo hupaswi kufanyiwa na fundi;

1. Kubadili bulb: Yaani taa inaungua, wewe na mke wako mnaona suluhu ni kumwita fundi.

2. Kufunga screen ukutani: Acha uzembe, hilo ni jukumu lako, install app yoyote ya pima maji itakusaidia kunyoosha ili TV isipinde, kuna mtu anafunga TV inapinda utadhani kalazimishwa.

3. Kufunga dish: Unapigwaje pesa kizembe kufunga dish la ku band? Nunua sat finder ya dollar 7 tu zile manual itakusaidia hata ukiwa pekeyako unafunga, ikitokea changamoto yoyote unafix, sio wewe na mke wako mnaita fundi kwa case ya kijinga kama hii.

4. Kufyeka nyasi kuzunguka nyumba yako: Usijifanye uko busy sana mtoto wa kiume wewe, weekend itumie kurekebisha mazingira ya nyumba yako, fyeka, pogoa miti, reki nyasi nk.

5. Kuzibua sink la jikoni: Mke anakwambia baby sinki limeziba wewe akili yako inakutuma kwa fundi, alaah!

6. Kufix matatizo madogo madogo ya umeme: Matatizo kama kubadili fuse, kurekebisha extension, kubadili socket nayo mpaka uite fundi? Sasa topic ya Electricity ulijifunza ili iweje?

7. Kufunga mapazia: Unataka fundi aje chumbani kwako apande juu ya kitanda chako kukuwekea mapazia?

8. Kubadili oil kwenye gari lako na kufanya service ndogo ndogo: Ingia youtube jifunze acha uzembe wewe, ndomaana likitambi linaota sababu ya uzembe.

9. Kuosha gari hata mara 1 kwa mwezi: Fanya hivi watoto waige.

10. Kuendesha vyombo vya moto: Hakikisha unajua kuendesha gari na pikipiki, ikibidi uwe na leseni hata kama haumiliki hivyo vyombo.

NB: Mwanaume unapaswa kumiliki toolbox nyumbani kwako bila kusahau ngazi na vitendea kazi vingine.

Mfanye mke wako aone kuna mwanaume, usiwe mlegevu ukasingizia huna muda kumbe huna maarifa.

Unapomlipa fundi jua kuwa unalipia gharama ya ujinga wako, hakikisha fundi anakuja kwa suala ambalo hata yeye akija atahangaika.
 
mimi ninaekaa nyumba ya kupanga kwahiyo kila ninipohama naamia na ngazi yangu??

bro swala la kuweka taa nakubaliana na wewe ila kuhusu mambo ya fuse extension sijui imefanya nini ita fundi, usifanye mtu kwenye neutral akaweka live

bro unajua namna ya kufunga dish wewe una mashine ya kufungia wewe ili upate signal na quality?? labda Startimes ila sio Azam na DSTV au ndo kisa dish la jirani limeelekea mbagala na wewe ufanye hivyo hivy? ita fundi

bro huu uzi unawahusu watu wa maisha gani?? wengine hayo masink unayosemea tunayaona kwenye muv na public toilets tu

kuosha gari 🤣🤣🤣 gari ipi wakati gari zetu ni mwendo wa mateka

mwisho wa yote mwanaume kuwa na hela tu basi hayo mengine yatajifanya yenyewe automatically
 
mimi ninaekaa nyumba ya kupanga kwahiyo kila ninipohama naamia na ngazi yangu??

bro swala la kuweka taa nakubaliana na wewe ila kuhusu mambo ya fuse extension sijui imefanya nini ita fundi

bro unajua namna ya kufunga dish wewe una mashine ya kufungia wewe ili upate signal na quality?? labda Startimes ila sio Azam na DSTV au ndo kisa dish la jirani limeelekea mbagala na wewe ufanye hivyo hivy? ita fundi

bro huu uzi unawahusu watu wa maisha gani?? wengine hayo masink unayosemea tunayaona kwenye muv na public toilets tu

kuosha gari gari ipi wakati gari zetu ni mwendo wa mateka

Chagua yanayoenda na maisha na hali yako….. don’t complicate
 
Kwan Kuna kidume hakiwezi kufanya hizo ishu.

Kipindi hcho nliwahi kujikuta fundi Dishi lolote lile. Na kaz ilienda vzr tu jpo skua najua nachokifanya ni brabra tu mara waah kinawaka nachukua pesa angu huyooo.
Plus kutengeneza extension zilizo ungua SI haba unaishi mjini.
 
Kuna vitu ukiweka uanaume mbele itakuja kukugharim Maisha au viungo.

Maswala ya kuhangaika na ngazi bahati mbaya iteguke uvunje kiuno wakati mafundi wa kuwapa buku wajirisk wao wenyewe wapo.

Kama MWANAUME unatakiwa uwe na panga au rungu ndani.

Mbili hata kama hakuna kitu jitahidi uwe unatoka usiku na tochi kuangalia usalama.

Tatu, kama mwanaume hakikisha kitanda kinalegea nati.

Hayo maswala ya kufunga bulb mara kuosha gari ni kazi ambazo hata Mkeo anaweza fanya.
 
Back
Top Bottom