Kama washauri wenyewe wa Chadema ndio hawa...

Kama washauri wenyewe wa Chadema ndio hawa...

Mzalendo_Mwandamizi

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2007
Posts
1,116
Reaction score
4,773
Chadema imepoteza wabunge wawili ndani ya takriban masaa 48. Kila anayefuatilia kwa karibu matukio haya anaifahamu drill: CCM watakaa pembeni wakiwa na kicheko kikubwa huku "waasi" kutoka Chadema wakifanya kazi ya kukaanga chama hicho kikuu cha upinzani. Then Chadema watakuja na script Ileile "acha waondoke. Chama bado imara." Baada ya hapo, maisha yanaendelea kana kwamba hakuna kilichotokea.

Ni rahisi kuilaumu CCM kwamba inatumia mbinu chafu "kulazimisha" wabunge na madiwani wa Chadema kujiunga na chama hicho tawala. Hilo la mbinu chafu ni kweli, na ni chafu kwelikweli. Kwa kifupi, nyenzo muhimu inayowezesha hamahama hiyo ni ile "ya Putin kwa Trump" yaani KOMPROMAT. Ileile ambayo JIWE anafanyiwa na "Mtu Mrefu Paulo." Yawezekana kabisa kuwa mbinu hii ambayo ni maarufu sana katika "sistema" huko Russia ikihusisha mashushushu, inaweza kuwa ni "msaada wa kiutawala" kwa Jiwe kutoka kwa "Mtu Mrefu Paulo."

Uzuri wa "kompromat" ni kwamba it usually works, tena kwa ufanisi. Fanikiwa kupata compromising info kuhusu mlengwa, basi huyo anakuwa mtumwa wako wa kudumu. Labda kuna siku nitapata wasaa wa kueleza hili kiundani ila ninachoweza kueleza kwa sasa ni kwamba hamahama hii inaambatana na udhalilishaji mkubwa ambao baadaye hutumika kwenye "kompromat."

Lakini Chadema haiwezi kukwepa lawama kwa haya yanayoisibu. Wakati flani, chama hicho kilikuwa na Idara ya intelijensia iliyokuwa hodari mno, yayumkinika kusema "hodari karibu au hata zaidi ya TISS." Hii ilikuwa Chadema ya enzi za kina Dokta Slaa. Ilikuwa both defensive and offensive. Defensive kwa namna ilivyoweza kubaini hujuma mbalimbali dhidi ya chama from CCM na kitengo. Offensive kwa namna ilivyoweza kujipenyeza serikalini na hata TISS na ndio maana iliwezekana kuibua skandali mbalimbali kama EPA, Richmond, nk.

Ninaweza kusema bila kusita kuwa laiti ingekuwa zama hizo, hawa wanaohama wangejulikana kabla hawajafanya "surprises" hizi za mfululizo. Kusema "ah huyu alikuwa mzigo" ilhali hamkumtimua mpaka akawakimbia ni utoto wa kisiasa. Kudai "acha waende" ilhali hatuambiwi kuwa "huyu na yule kamwe hawawezi kuhama" ni mzaha.

Kwa uelewa wangu, kuna wabunge wengine kadhaa wapo njiani kuhama. Na kama unadhani hizi ni porojo tu, zingatia "ubashiri" wangu huu nilioutoa majuzi na umetimia

Chadema kuilaumu CCM kwa mbinu chafu ni sawa na Yanga kuilaumu Simba kwa hujuma. Iwe kwa njia halali au zisizo halali, jukumu la kujikinga na hujuma za adui haliwezi kutegemea huruma ya adui. Kwamba "tuzembee, akitudhuru tumlaumu." Who cares?

Talking of mapungufu ya kiintelijensia ndani ya Chadema, nimekutana na bandiko la mmoja wa "think tanks" za chama hicho, Bwana Yericko. Let's be honest, kama "washauri wa kiintelijensia" wa Chadema ndio wa aina hii, basi mustakabali wa chama hicho upo hatarini. Hebu angalia bandiko hili hapa chini la Bwana Yericko kisha rejea bandiko halisi "aliloiba" huko Facebook.

Bandiko la Yericko ni hili hapa Kama nitasafiri kwa ndege moja na Polepole na Lugola nitaomba niwaelekeze haya:

Bandiko aliloiba kutoka kwa Mheshimiwa Ismail Jussa ni hili hapa Ismail Jussa

Labda hili halihusiani na "mapungufu" ya Chadema lakini nonetheless halileti picha nzuri, especially katika kipindi hiki ambapo chama hicho kikuu cha upinzani kinapitia kipindi kigumu.

Screenshot_20180731-022533.jpg
Screenshot_20180731-022551.jpg
Screenshot_20180731-022653.jpg
Screenshot_20180731-022712.jpg
Screenshot_20180731-022727.jpg
Screenshot_20180731-022741.jpg
Screenshot_20180731-021357_Chrome%20Beta.jpg
Screenshot_20180731-021415_Chrome%20Beta.jpg
Screenshot_20180731-021429_Chrome%20Beta.jpg
Screenshot_20180731-021445_Chrome%20Beta.jpg
Screenshot_20180731-021503_Chrome%20Beta.jpg
Screenshot_20180731-021518_Chrome%20Beta.jpg
 
Kupata taarifa kwa TISS ya sasa not easy like that braza. Kitengo kwa sasa kina endeshwa kwa weledi na uzalendo. Wataishia kupata tetesi zisizo na uhalisia. Weewe unasikia hata siku izi Siri za vikao vya state house au vikao vikuu vya chama zinavuja kama zamani. Mambo yamebadilika sana na kiukweli nimeiamini ule msemo kuwa mtu mmoja anaweza kubadilisha mambo kabisa.
 
Hakuna siasa chafu,nakumbuka 2013-2015 chadema ilipokea wana ccm wengi sana...hizo hazikuwa siasa chafu za chadema wala chadema haikununua mtu...
Nina uhakika leo hakuna anayenunuliwa...Ila watu hawaoni mwelekeo wao,hawaoni kesho yao....
Wapo wengi wanatamani kuondoka....Ila hawajui njia yakupita....

Siyo jambo lakufurahisha....Mbowe hajawahi kuwa kiongozi makini....
 
Chahali analysis yako ni very poor! Nilikuwa nakuamini sana katika haya mambo. Kumbe na wewe ni wale wale. Unasahau kuwa CDM is dealing with a BRUTAL DICTATOR in all senses. How do you deal with someone using a gun, police, army to silence opossition and not HOJA kupambana na upinzania? Unapambanaje na Dikiteita ambaye hata vikao vya ndani amevikataza, viongozi wote wanabambikiwa kesi? Mahakama compromised??? (kwa kiasi fulani CJ aliingilia siasa kidogo) .Ruhusu CDM iende kwa watu iwahubirie kinachoendelea uone kama haitaungwa mkono. Unapambanaje na Idd Amin, Kim Jong Un , Kagame ,,, (Diane Rwigima) , Museveni and the like. Nadhani umenielewa Evarist Chahali

Mpinzania wa Kagame ashitakiwa kwa kosa la uasi

By Rashid Bugi -

1533006334168.png

Mkosoaji mkubwa wa rais wa Rwanda Paul Kagame, Diane Rwigara ameshtakiwa kwa kuchochea uasi dhidi ya serikali.

Ameshtakiwa pamoja na mama yake mzazi aitwae Adeline Rwigara na dada yake Anne Rwigara.
Diane Rwigara aluzuiwa kuwania urais wa mwezi Agosti nchini Rwanda ambapo rais Kagame alishinda kwa kishindo.
Rais wa sasa Paul Kahame alishinda uchaguzi huo kwa asilimia 99, na kupelekea madai kuwa kuikuwa na udanganyifu madai yalipingwa na mamlaka ya nchi hiyo.
Diane Rwigara pia ameshtakiwa kwa kubuni stakabadhi bandia.
Wachunguzi wanadai kuwa Bi Rwigara alivunja sheria za uchaguzi kwa kukusanya sahihi bandia kuunga mkono ugombeaji wake.
Haijulikani ni kitu gani kilichangia afunguliwe mashtaka ya kuchochea uasi nchini humo pamona na ndugu zake.
 
Last edited:

Zinawezekana sana. Unadhani operatives wote wa TISS wanapenda yanayoendelea? Hata na wao pia wanafamilia, wanaishi uraiani kama sisi.
Kama una bisha, Mange anapataje habari za humo ndani? Lissu alikuwa anazipataje?

Sema tu sasa hiv chama hakina watu wenye ushawishi tena. So wale operative wa TISS hawana imani kabisa nao hata kama wakiwavujishia habari.
 
View attachment 823222

Umeelewa kilichoandikwa na Chahali lakini? I'm afraid you're too emotional and out of the topic
 
Sometimes huwa najiuliza! Kununuliwa? Basi kama ni kununuliwa, it's too much and no justification!!

Kwangu naona ni ujinga kwa CHADEMA kuwashutumu Wabunge wake kwamba wananunuliwa! Naona ujinga kwa sababu, hiyo biashara itakuwa ina-confirm only one thing kwamba: CHADEMA nayo imejaa a bunch of cheap politicians with price tags!

Hili ni jambo la aibu lisilofaa kuongelewa kwa mikogo!!

Endapo CHADEMA wangeshinda 2015, hawa akina Waitara wangekuwa ndo mawaziri wetu!

So, endapo leo hii CHADEMA inatuambia Wabunge wake wananunuliwa na CCM, sasa baada ya kuwa mawaziri wangeshindwa vp kununuliwa na mabepari ya kimataifa yanayotafuta money making deals in Tanzania?! Tuna oil and gas hivi sasa! Ni very corrupt industry duniani!

Lakini linapokuja suala la kompromat; tufanye kusikia tu! Hiyo ni habari nyingine! Kila mtu ana kitu ambacho asingependa kifahamike! Na wataalamu wakikukusudia; hata kama upo clean; unaweza kuwa setup!

Kwenye kompromat hakuna ujanja; yakikukuta; usishangae kukuta hata radicals kama akina Sugu na Lissu; ukakuta kesho wanaanza kuimba nyimbo za CCM!

Hata kama Evarist Chahali anaweza asiwe sahihi, but we've to think of this possibility as well!

Malcom Lumumba, JokaKuu
 
Last edited by a moderator:
Si ndio wewe unajuaga kila kitu na kupayuka kwa maandishi...
Eeeeeh leo naona usingizi uliukosa..
Jilaumu na nyie mnaopiga porojo mitandaoni.. kuwa wasemaji wa Chama.. na wao kuamua kuwaachia uwanja huku wenyewe wanachojali ni matumbo yao kwanza.
Kila mkiandika ni kudakia yanayofanya na CCM.. eeeh
Wewe lini umewahi kuandika juu ya nchama chako tu hata angalau kuhamasisha?
Ukila ukilala CCM.. wewe moyo upo CCM na mwili Chadema.. eeeeeeh
Kumbe u bomu unalia lia leo ha ha haaaa

HAWANUNULIWI.. WANAKIMBIA UOZO, CHAMA KILICHOJICHIMBIA SHIMO LA FUTI SITA NA KUDUMBUKIA WENYEWE..
 
Hakuna siasa chafu,nakumbuka 2013-2015 chadema ilipokea wana ccm wengi sana...hizo hazikuwa siasa chafu za chadema wala chadema haikununua mtu...
Nina uhakika leo hakuna anayenunuliwa...Ila watu hawaoni mwelekeo wao,hawaoni kesho yao....
Wapo wengi wanatamani kuondoka....Ila hawajui njia yakupita....

Siyo jambo lakufurahisha....Mbowe hajawahi kuwa kiongozi makini....
Vipi kesho yako! Ushaiona?
 
Kupata taarifa kwa TISS ya sasa not easy like that braza. Kitengo kwa sasa kina endeshwa kwa weledi na uzalendo. Wataishia kupata tetesi zisizo na uhalisia. Weewe unasikia hata siku izi Siri za vikao vya state house au vikao vikuu vya chama zinavuja kama zamani. Mambo yamebadilika sana na kiukweli nimeiamini ule msemo kuwa mtu mmoja anaweza kubadilisha mambo kabisa.
Broo Da Mange anazipata frsh tuuu
 
Chahali kachambua vizuri sana, kitengo cha intelijensia CHADEMA kimepwaya. Jamaaa aliona nunua nunua inamaliza pesa na haina tija so hii ya kuwa na habari fulani mbaya au hata 'kutengeneza habari mbaya'ya adui yako ikawa ndio silaha yako ya kumfanya afuate matakwa yako la sivyo utaitoa naona inafanya kazi vizuri mno.CHADEMA wasipoifanyia kazi na kuweka vikao vya kimkakati nakwambia wabunge wake wengi watajiuzulu na kurudi chama dola ili kulinda heshima zao na mambo mengine.Hii njia hata mzee wa kupenda kuvua kule "moscowu" naona imemletea neema kubwa mno ndio maana jamaa wa kuandika kwa herufi kubwa kwa "Iraniani presidenti" yupo yupo tu. Nilipoumia zaidi ni hapa Chahali aliposema "ni kwamba hamahama hii inaambatana na udhalilishaji mkubwa ambao baadaye hutumika kwenye "kompromat." "
 
Last edited:
Sema wanao hama ikifika 2025 wataiama CCM sababu haziishi kwa kuwa ni ugonjwa wao ulojaa ulafi na njaa
 
Umeelewa kilichoandikwa na Chahali lakini? I'm afraid you're too emotional and out of the topic
Nimemuelewa vizuri. Kuna lawama anazitupa kwa CDM , anasahau political situation ya sasa. Nawewe hujanijibu viswali vidogo nilivyouliza, ila umekuwa emotional vile vile. Labda kama Chahali anailamu CDM/viongozi wake kwa kuogopa risasi, vifungo, vipigo then he is right! Huu ni wakati mgumu sana, sawa na Rwanda! Ukisema tu unapotea, who dares? Mbowe anajaribu lkn maisha yake wakati wowote yatatoweka. Wangapi wa kuwa na ujasiri huo? soma hili la Lisu
Lissu ajibu shutuma za Ruzuku, athibitisha bila Mbowe kuchanganya na zake hakuna kinachofanyika, wanao hama waende
 
Zinawezekana sana. Unadhani operatives wote wa TISS wanapenda yanayoendelea? Hata na wao pia wanafamilia, wanaishi uraiani kama sisi.
Kama una bisha, Mange anapataje habari za humo ndani? Lissu alikuwa anazipataje?

Sema tu sasa hiv chama hakina watu wenye ushawishi tena. So wale operative wa TISS hawana imani kabisa nao hata kama wakiwavujishia habari.
A big NO! Unasahau kuwa enzi ulizozitaja zilikuwa na democrasia kwa kiasi fulani. Maisha ya watu hayakuwa hatarini kama ilivyo sasa. sasa ni full swing dictatorship! Kuna risk kubwa ya maisha tofauti na zamani. Kilaupande unaogopa KIFO, si TISS si CDM. Ya Lisu ni funzo la kulitilia maanani kabla hujafanya lolote. Mange ni rahisi maana ukimrushia umemaliza kazi hakuna leakage kama ukifanya hapa. Ungelitegemea Waitara kufanya haya?
 
Last edited:
Sometimes huwa najiuliza! Kununuliwa? Basi kama ni kununuliwa, it's too much and no justification!!

Kwangu naona ni ujinga kwa CHADEMA kuwashutumu Wabunge wake kwamba wananunuliwa! Naona ujinga kwa sababu, hiyo biashara itakuwa ina-confirm only one thing kwamba: CHADEMA nayo imejaa a bunch of cheap politicians with price tags!

Hili ni jambo la aibu lisilofaa kuongelewa kwa mikogo!!

Endapo CHADEMA wangeshinda 2015, hawa akina Waitara wangekuwa ndo mawaziri wetu!

So, endapo leo hii CHADEMA inatuambia Wabunge wake wananunuliwa na CCM, sasa baada ya kuwa mawaziri wangeshindwa vp kununuliwa na mabepari ya kimataifa yanayotafuta money making deals in Tanzania?! Tuna oil and gas hivi sasa! Ni very corrupt industry duniani!

Lakini linapokuja suala la kompromat; tufanye kusikia tu! Hiyo ni habari nyingine! Kila mtu ana kitu ambacho asingependa kifahamike! Na wataalamu wakikukusudia; hata kama upo clean; unaweza kuwa setup!

Kwenye kompromat hakuna ujanja; yakikukuta; usishangae kukuta hata radicals kama akina Sugu na Lissu; ukakuta kesho wanaanza kuimba nyimbo za CCM!

Hata kama Evarist Chahali anaweza asiwe sahihi, but we've to think of this possibility as well!

Malcom Lumumba, JokaKuu
Unasahau kuwa kwa sasa haya hayaonekani CCM kwa vile kuna mkate kule. Unaamini say CDM au chama chochote mbali na CCM kikiwa madarakani wakahubiri ujinga huu wa kununua watu, walio sasa CCM hawatatoka? Hawatanunuliwa? Tafakari zaidi, usiishie karibu!
 
Back
Top Bottom