Kama wanaona ishu ni LOWASA basi UKAWA Wekeni JIWE ligombee urais ,tutachagua hilo hilo

nyuli

Senior Member
Sep 7, 2012
128
95
Huduma za Afya mbovu,Ajira hakuna,Umeme leo mwezi wa tatu huu shida tupu.Harafu mtu leo anasimama jukwaani na ahadi zile zile baada ya kupewa uaminifu na wananchi na kutawala nchi hii miaka hamsini matokeo yake nchi imeachwa katika hali hii ya kusikitisha
wananchi tunaonekana wajinga.

Wakati mimi biashara yangu inadoda umeme hakuna.bila shaka nyie viongozi mnaotutukana sisi wapumbavu na malofa mnapigwa na kiyoyozi huko wakati sisi watoto wetu wanashindaa njaa sababu huduma ya nishati ya umeme mnakata miezi mitatu sasa tena hamtoi taarifa kama kuna mgao au la.Mnacho jua sisi Watanzania ni watu wapumbavu utulivu wetu na mabaya yote haya mnayo tufanyia harafu bado mnaleta propaganda za kuzingizia watu mafisadi ninyi jema lipi mlilo tutendea?


Cha ajabu chama hicho hicho ambacho kimetuacha katika dimbwi la dhiki leo tena kinakuja bila aibu na kinaniahidi eti kutakua na neema ndani ya miaka mitano ijayo kama nikikipa ridhaa!SO WONDERFUL!!!

I say NEVER and NEVER AGAIN!Hivi hata dhamira zenu haziwasuti kwamba Watanzania wameteseka vya kutosha angalau sasa muwaache huru?

Mi nadhani hizi propaganda za kuhangaika na upandikizaji wa chuki dhidi ya viongozi ambao wapo katika upande unaoelekea kuung'oa utawala huu ulio jisahau madarakani ni kupoteza muda wenu na rasimali zenu bure!

Kwa sababu toka Dr.Mihogo aanze kubwabwaja fitina zake katika vyombo vya habari sijumuona japo hata jirani yangu aliyekuwa UKAWA akahamia ama kurudi upande wa chama cha kikoloni.Zaidi zaidi nacho kiona ni kuchochea hasira za wanamabadiliko katika kwenda kutoa adhabu takatifu tarehe 25/10/2015.

Badala ya kuhangaika kupandikiza chuki kwa nini msiboreshe maisha yetu,Afya,Umeme Ajira?Hivi mngeyafanya hayo leo mngekua mna haja ya kufanya siasa chafu?

Pia nawaasa vijana wenzangu ambao mnacheza sana na hasira za wananchi wenye maumivu ya maisha magumu,waliochoshwa na ahadi hewa Leo hii mnaanza kuigiza uanachama na kuanza kuandamana na kujifanya mkipinga viongozi wa mabadiliko;mtakuja kufa bure,acheni unafiki,msiige hao wanafiki wakubwa kwani wao wanalindwa na walinzi zaidi yakumi, wewe unafanya unafiki harafu huna mlinzi hata mmoja utakuja kupata kilema cha bure.

Hili nimelisema makusudi kwani baada ya kuiona video ya vijana walio pandikizwa kua wao ni UKAWA na kuanza kuwapinga viongozi wa juu wa Mabadiliko wamepata kipigo cha mbwa mwizi kutoka kwa raia,ndo maana nasema acheni kuzichokonoa hasira za Watanzania Waacheni hasira zao wakamalizie katika sanduku la kura wasije wakawatoa uhai wenu bure kwa maigizo yenu hayo ya kipumbavu ambayo mnafanya kwa kupewa kiasi kidogo tu cha fedha.


Watanzania wamebadilika Propaganda za kinafiki hazita saidia,ni bora kutulia tu,na kuwaacha watu wafanye maamuzi yao kwa busara na kwa amani.

Kama ulipewa miaka hamsini ya kusumshawishi mtanzania huyu mpole na mnyonge ukashindwa.Leo hii ameamua kukukataa unajifanya eti kule aliko ni kuchafu na kwako ni kusafi du!


Nimependa sana mfano wa Dr.Mihogo kwmaba kuna chama ambacho chenyewe ni choo na chama kingine kimechukua uchafu wa hicho choo,Dr.Mihogo akasema hicho chama ambacho kimechukua huo uchafu kitanuka zaidi kuliko choo,

Ni kweli chumba kitanuka sana lakini naweza kukisafisha na kesho kikanukia lakini choo ni sahemu najisi takataka zote chafu hutupiwa mle na choo ni sehemu ya kutunza uchafu na kamwe choo hua hakiishwi na uchafu hata ukiita gari ya maji taka kuja kusafisha choo kinatabakia kua ndo sehemu kuu ya kuhifadhi uchafu.Na ni bora kubeba sehemu ya uchafu kuliko kubeba choo chenyewe.



Wajinga tu ndio mtaendele kuwadanganya na kuwahodhi kwa kutumia mbinu za siasa za maji taka,kamwe mwenye akili timamu hawezi kudanganyika hata hata mumlete malaika aisemee vibaya UKAWA daima chama tawala mmechoka muda wenu umefika wa kuachia nchi propaganda za ajabu ajabu hazita wasaidia;zaidi zaidi mnazidi kututia hasira tu wananchi na tutawashikisha adabu octoba 25;msidhani bado mnaishi na jamii ya watu wasio jielewa,hata asipo kuwa Lowassa UKAWA wakiweka JIWE ni bora tulichagua jiwe mara milioni kuliko kuwachagua nyie ambae hadi saizi naandika ujumbe huu umeme umekatika sijafanya kazi mwezi watatu huu,nchi inaenda kisela tu,harafu mtu anapanda jukwaani anasema siju nini na nini!

Ngoja mfumo uondoke mengine baadae.
 
CCM itanunua wengi lakini haiwezi kununua watanzania wote. Hii mitandao husan whatsapp inatusaidia sana maana tunajua nani kanunuliwa na kwakiasi gani hata kabla huyo mtu hajaanza kutimiza lile alillonunuliwa kwalo.

CCM imemtumia Slaa sababu inamjua madhaifu yake. Kizuri nikwamba watanzania tulishamshtukia Slaa mapema.
 
Ahadi za ccm ni zilezile kila uchaguzi. Ivo wakiwa madarakani wanafanyaga nini? Namna hii nchi itaendelea lini? Uchaguzi wetu wetu umekuwa wa maigizo kwa miaka mingi. Turudishe heshima ya uchaguzi. Chagua ukawa/lowassa, uongo wa ccm umepitiliza.
 
Ukawa lindeni kura zenu kwa udi na uvumba.
Watu wanasubiri uchaguzi tu, hizi kampeni zinatupotezea muda.
 
Mimi wakiweka marehemu na ccm nachagua marehemu.



Hata ujawa wakiweka fisi agombee na ccm nachagua fisi.
Heri kuchagua fisi au mzoga kuliko ccm, cccm ni jannga la kitaifa.
 
Back
Top Bottom