Kama waliweza kupiga virungu vilema, kupiga wanawake mabomu hawawezi kushindwa

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,372
Jamani tuwe na kumbukumbu.Ni katika awamu hii tuliwahi pia shuhudia kupitia picha za mitandao vilema wakipigwa virungu na hatukuwahi kusikia wala kuona kiongozi yoyote wa hii serikali akikemea wala kuonya waliotekeleza unyama ule hivyo kwa wanawake wa CHADEMA kupigwa mabomu ni muendelezo tu wa matendo ya waliopewa mamlaka kuongoza vyombo vya dola na huenda yana baraka za wakubwa wao wa kazi na ndio maana hawachukuliwi hatua.

Hata hivyo,vitendo hivi japo ni vya hovyo na vya kikatili,vina faida moja kubwa tu ya kuamsha na kuchochea fikra na hisia kudai/kutaka mabadiliko.

Kwahiyo,kama ilivyokuwa kwa Wayahudi waliomsulubisha Yesu huku wakiwa hawajui walitendalo, vivyo hivyo watu hawa na mabosi wao nao hawajui walitendalo(wanajiandalia anguko pasipo kuelwa).

Kwa kifupi, watu hawa wamenyimwa maarifa,kujazwa viburi na kutiwa upofu ili waanguke.


Muda utakuja kuthibitisha.
 
Vilema nao watu wanaakili wakijichanganya kwa vile ni vilenma eti watahurumiwa watajuta
 
Back
Top Bottom