DOKEZO Kama Wabunge wanalipwa kwa mkupuo mafao yote, basi NSSF irejeshe Fao la Kujitoa, utaratibu wa sasa unatuumiza wengi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
844
Reaction score
1,604
Kutokana na changamoto kubwa ya upatikanaji wa ajira na mitaji ya kujiajiri hapa nchini, ninaomba Serikali iangalie upya sera ya mafao ya NSSF na kurejesha rasmi Fao la Kujitoa kwa Wafanyakazi wanaoachishwa kazi au ambao mikataba yao imekoma katika sekta binafsi.

Kwa mujibu wa mfumo wa sasa, mfanyakazi aliyeachishwa kazi analipwa 33% ya mshahara wake kwa miezi 6 kama Fao la Kukosa Ajira. Baada ya hapo hulazimika kusubiri miezi 18 kabla ya kupewa salio la michango yake – ikiwa hajapata ajira nyingine.
Screenshot 2025-09-01 120127.jpg
Changamoto kubwa ni kwamba NSSF wala Serikali hawatoi msaada wowote wa ajira katika kipindi hiki cha kusubiri, hivyo wahanga wengi huishia katika hali ngumu ya kiuchumi bila mtaji, bila kipato na bila matumaini.

Pendekezo langu ni:
NSSF iwe na mfumo unaompa mwanachama uhuru wa kuchagua kati ya:
1. Kulipwa Fao la Kujitoa kwa mkupuo (kiasi chote cha michango yake), au
2. Kuendelea na utaratibu wa sasa wa Fao la Kukosa Ajira.

Ni ukweli mchungu kwamba vijana wengi wenye elimu ya juu ndiyo wanaathirika zaidi na mfumo huu, hali inayowafanya wengine hadi kuficha viwango vya elimu yao ili wapate michango yao. Kadri muda unavyosonga, ndivyo inavyokuwa vigumu zaidi kupata ajira mpya kutokana na ushindani mkubwa wa wahitimu wanaoingia sokoni kila mwaka.

Kwa kuwa Serikali yenyewe inahamasisha suala la kujiajiri, basi ni busara Fao la Kujitoa lirejeshwe ili liwe chanzo cha mtaji wa kuanzisha biashara na miradi midogo midogo.

NSSF pia inaweza kupata uhalisia wa tatizo hili kwa kuhoji wanachama waliolipwa au wanaolipwa Fao la Kukosa Ajira – wengi wao wangethibitisha kuwa kupata fedha zao kwa mkupuo ndilo chaguo lenye tija zaidi.

Inashangaza kuona wabunge – ambao ndio watungaji wa sera hizi – wao hulipwa mafao yao yote mara tu baada ya Bunge kuvunjwa, badala ya kupewa kidogo kidogo kama "Fao la Kukosa Ubunge." Hii ni dhihirisho la wazi kwamba sera hii inawabana wananchi wa kawaida pekee na si viongozi.

Ikiwa sera hii ilikopwa kutoka nchi za nje, basi hakika ilibebwa kutoka mazingira yenye urahisi wa kupata ajira mpya – hali ambayo haipo Tanzania. Hapa kwetu ajira ni haba, na ushahidi upo wazi katika idadi kubwa ya vijana wanaoomba nafasi chache za kazi zinazotangazwa.

Kwa ufupi, Fao la Kujitoa lirejeshwe mara moja ili kusaidia wananchi waliopoteza ajira katika sekta binafsi waweze kujiajiri, kujikimu na kusaidia familia zao, badala ya kulazimishwa kuishi maisha ya kuombaomba wakati michango yao ipo NSSF.
 
Hatari sana.

KIfupi kuna changamoto nyingi sana kuhusu hizi pesa zetu zilizopo huko NSSF.

Wengine tumechangia sana huko na sasa hivi tumeajiriwa serikalini lakini hatma ya pesa zetu tunaambiwa tusubiri hadi tutakapostaafu ndio tuzichukue, kama vipi waziunganishe na hizi huku PSSSF tuwe na amani.

Bunge liwe linatunga sera na sheria za kuwanufaisha wanainchi sio kuwaumiza.
 
Umeongea vyema, changamoto kubwa ya sera na sheria nyingi hutungwa bila kuwahusisha main stakeholder ambao ndiyo wanajua tamu na chungu na ndiyo wahanga wakuu wa sheria zinazopitishwa na wagonga meza.
Bad enough kama hili jambo lingekuwa ni zuri sana, kwanini lisingetumika na kwao pia?
 
Hii ndo maana tunataka reforms kabsa haiwezkani hela ni yangu mkataba wangu umeisha nataka hela yangu sio mkopo wala nini bado unanipangia namna inavyotakiwa nipewe iyo hela 😔
 
Kutokana na changamoto kubwa ya upatikanaji wa ajira na mitaji ya kujiajiri hapa nchini, ninaomba Serikali iangalie upya sera ya mafao ya NSSF na kurejesha rasmi Fao la Kujitoa kwa Wafanyakazi wanaoachishwa kazi au ambao mikataba yao imekoma katika sekta binafsi.

Kwa mujibu wa mfumo wa sasa, mfanyakazi aliyeachishwa kazi analipwa 33% ya mshahara wake kwa miezi 6 kama Fao la Kukosa Ajira. Baada ya hapo hulazimika kusubiri miezi 18 kabla ya kupewa salio la michango yake – ikiwa hajapata ajira nyingine.
Changamoto kubwa ni kwamba NSSF wala Serikali hawatoi msaada wowote wa ajira katika kipindi hiki cha kusubiri, hivyo wahanga wengi huishia katika hali ngumu ya kiuchumi bila mtaji, bila kipato na bila matumaini.

Pendekezo langu ni:
NSSF iwe na mfumo unaompa mwanachama uhuru wa kuchagua kati ya:
1. Kulipwa Fao la Kujitoa kwa mkupuo (kiasi chote cha michango yake), au
2. Kuendelea na utaratibu wa sasa wa Fao la Kukosa Ajira.

Ni ukweli mchungu kwamba vijana wengi wenye elimu ya juu ndiyo wanaathirika zaidi na mfumo huu, hali inayowafanya wengine hadi kuficha viwango vya elimu yao ili wapate michango yao. Kadri muda unavyosonga, ndivyo inavyokuwa vigumu zaidi kupata ajira mpya kutokana na ushindani mkubwa wa wahitimu wanaoingia sokoni kila mwaka.

Kwa kuwa Serikali yenyewe inahamasisha suala la kujiajiri, basi ni busara Fao la Kujitoa lirejeshwe ili liwe chanzo cha mtaji wa kuanzisha biashara na miradi midogo midogo.

NSSF pia inaweza kupata uhalisia wa tatizo hili kwa kuhoji wanachama waliolipwa au wanaolipwa Fao la Kukosa Ajira – wengi wao wangethibitisha kuwa kupata fedha zao kwa mkupuo ndilo chaguo lenye tija zaidi.

Inashangaza kuona wabunge – ambao ndio watungaji wa sera hizi – wao hulipwa mafao yao yote mara tu baada ya Bunge kuvunjwa, badala ya kupewa kidogo kidogo kama "Fao la Kukosa Ubunge." Hii ni dhihirisho la wazi kwamba sera hii inawabana wananchi wa kawaida pekee na si viongozi.

Ikiwa sera hii ilikopwa kutoka nchi za nje, basi hakika ilibebwa kutoka mazingira yenye urahisi wa kupata ajira mpya – hali ambayo haipo Tanzania. Hapa kwetu ajira ni haba, na ushahidi upo wazi katika idadi kubwa ya vijana wanaoomba nafasi chache za kazi zinazotangazwa.

Kwa ufupi, Fao la Kujitoa lirejeshwe mara moja ili kusaidia wananchi waliopoteza ajira katika sekta binafsi waweze kujiajiri, kujikimu na kusaidia familia zao, badala ya kulazimishwa kuishi maisha ya kuombaomba wakati michango yao ipo NSSF.

Hii nchi viongozi ndiyo huamua namna inavyokwenda kwa maslahi yao binafsi.

Ndiyo maana hao wabunge wameweka sheria na taratibu za wao kulipwa mafao kwa mkupuo, ni maslahi yao binafsi na si ya wengi.

Hatuna viongozi kwa ajili ya watu bali viongozi wanaotafuta na kusimamia maslahi yao binafsi.

Lakini yana mwisho, ni suala la muda tu kufika.
 
Watanzania wenzangu shida hatujui nani ndo shida,,,NSSF wanatekeleza sheria,,siyo maamuzi yao
 
Kutokana na changamoto kubwa ya upatikanaji wa ajira na mitaji ya kujiajiri hapa nchini, ninaomba Serikali iangalie upya sera ya mafao ya NSSF na kurejesha rasmi Fao la Kujitoa kwa Wafanyakazi wanaoachishwa kazi au ambao mikataba yao imekoma katika sekta binafsi.

Kwa mujibu wa mfumo wa sasa, mfanyakazi aliyeachishwa kazi analipwa 33% ya mshahara wake kwa miezi 6 kama Fao la Kukosa Ajira. Baada ya hapo hulazimika kusubiri miezi 18 kabla ya kupewa salio la michango yake – ikiwa hajapata ajira nyingine.
Changamoto kubwa ni kwamba NSSF wala Serikali hawatoi msaada wowote wa ajira katika kipindi hiki cha kusubiri, hivyo wahanga wengi huishia katika hali ngumu ya kiuchumi bila mtaji, bila kipato na bila matumaini.

Pendekezo langu ni:
NSSF iwe na mfumo unaompa mwanachama uhuru wa kuchagua kati ya:
1. Kulipwa Fao la Kujitoa kwa mkupuo (kiasi chote cha michango yake), au
2. Kuendelea na utaratibu wa sasa wa Fao la Kukosa Ajira.

Ni ukweli mchungu kwamba vijana wengi wenye elimu ya juu ndiyo wanaathirika zaidi na mfumo huu, hali inayowafanya wengine hadi kuficha viwango vya elimu yao ili wapate michango yao. Kadri muda unavyosonga, ndivyo inavyokuwa vigumu zaidi kupata ajira mpya kutokana na ushindani mkubwa wa wahitimu wanaoingia sokoni kila mwaka.

Kwa kuwa Serikali yenyewe inahamasisha suala la kujiajiri, basi ni busara Fao la Kujitoa lirejeshwe ili liwe chanzo cha mtaji wa kuanzisha biashara na miradi midogo midogo.

NSSF pia inaweza kupata uhalisia wa tatizo hili kwa kuhoji wanachama waliolipwa au wanaolipwa Fao la Kukosa Ajira – wengi wao wangethibitisha kuwa kupata fedha zao kwa mkupuo ndilo chaguo lenye tija zaidi.

Inashangaza kuona wabunge – ambao ndio watungaji wa sera hizi – wao hulipwa mafao yao yote mara tu baada ya Bunge kuvunjwa, badala ya kupewa kidogo kidogo kama "Fao la Kukosa Ubunge." Hii ni dhihirisho la wazi kwamba sera hii inawabana wananchi wa kawaida pekee na si viongozi.

Ikiwa sera hii ilikopwa kutoka nchi za nje, basi hakika ilibebwa kutoka mazingira yenye urahisi wa kupata ajira mpya – hali ambayo haipo Tanzania. Hapa kwetu ajira ni haba, na ushahidi upo wazi katika idadi kubwa ya vijana wanaoomba nafasi chache za kazi zinazotangazwa.

Kwa ufupi, Fao la Kujitoa lirejeshwe mara moja ili kusaidia wananchi waliopoteza ajira katika sekta binafsi waweze kujiajiri, kujikimu na kusaidia familia zao, badala ya kulazimishwa kuishi maisha ya kuombaomba wakati michango yao ipo NSSF.
Wakurudishie tu huku umekaa hapo sebuleni? Haki inakuja kwa kudaiwa. Endelea kusubiri...
 
Hao watu kwenye kukata wapo vizuri ila linapokuja suala la kutoa fedha ni kizungumkuti. Sasa wanawapangiaje watu Matumizi. Mtu ameacha kazi anataka fedha ili ajiajiri wao wanazuia. 😭😭
 
Hili ni moja ya Vitu vilifanya nisimuelewe JPM, alisema anapambanja wanyonge aliwezaje kuacha NSSF wakafika hapa, Au ndo vile anachota hela zao anaenda kujenga CHATO?
 
Back
Top Bottom