missa nadhani hilo limekuwa fundisho siyo kwa huyo dada tu, bali hata marafiki zake waliokuwa wanamzunguka, na pia hata humu ndani ya jukwaa la MMU kwa ambao wamebahatika kulisoma bandiko hili maana najuwa watu wa aina hii wamo pia.
Nampongeza ndg yako kwa huo uamuzi na pia hongera zake kwa vile alikuwa mvumilivu sana kwa kifupi huyu alikuwa mwanaume mwenye wito wa ndoa ila tu aliangukia pabaya.
Muhimu kwake kwa sasa if possible abadili mawasiliano ili kumweupuka huyo dada, asione hatari sana hata kama ni kwa muda anaweza fanya hivyo ili huo upepo wa kishetani upite na kwa vile alishakuwa na mpango wa kufunga ndoa basi angalie kwenye list yake ili kusogeza yule wa plan B aweze kuchukua nafasi as soon as possible.
Jamani uzuri wa sura ndani ya ndoa sio issue ya msingi sana, itasadia nini kama ukoa mke mzuri wa sura, mbaya wa tabia nk, akiungua moto jikoni sura ikaharibika utampa talaka ama.
Hapo ndio nakumbuka mdau aliyesema "Mama hana hata baiskel..........." lakini mtu mwingine ambaye hajitambui anapewa fursa kibao anazichezea, kifupi huyo dada hiyo laana itamumaliza.
Ni mtizamo tu