Kama uwezekano upo, kwanini tusiwe na mfumo wa luku katika utumiaji wa maji ya bomba?

Mwamba 3

JF-Expert Member
Dec 20, 2018
253
279
Nipo mkoa fulani , linapofika suala la ulipaji wa bili ya maji ni pasua kichwa sana . Yaani inavyoonekana wateja wa maji ya bomba bili zake nadhani zinakadiliwa tu na mamlaka husika .
Kuna kipindi fulani ilitoka bili kubwa , kama mara mbili na nusu ya bill tulipayo ya kawaida kwa kila mwezi . Kila mpangaji alishtuka lkn tukalichukulia poa .

Mwezi uliyopita ( wa kwanza ) , tukapewa tena bili kubwa sana kwa njia ya sms . Yaani kubwa kuliko matumizi . Ile tunajiuliza jiuliza kwa nini bili kubwa hivi wakatuma tena bili ya pili . Hapo wakasema bili ya kwanza ilikosewa .
Sasa nikajiuliza inakosewaje , au kuna mazingira idara husika wanawahujumu watumiaji ?
Kwa nini tusitumie mfumo wa LUKU ?

Karibuni wadau wa maji Nchini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom