Kama utaoa mke zaidi ya mmoja au unamchepuko umezaa nae andika wosia mapema

karv

JF-Expert Member
Dec 26, 2019
1,799
3,221
Habari za wakati huu watanzania wenzangu

Leo napenda kutoa ushauri wa bure kama ni mwanaume na umeoa mke zaidi ya mmoja au una mchepuko umezaa nao basi nakushauri andika wosia mapema isije tokea misuguano kwa watoto siku ukifariki.

Siku moja nilienda kwa ndugu yangu mmoja kumtembelea lakini hali niliyomkuta nayo ilinihuzunisha na akaanza kukisimulia kama ifuatavyo

Yeye aliolewa kama mke mdogo na katika ndoa yake mumewe alijenga nyumba 2 kila mwanamke akiwa na nyumba yake. Mke mkubwa alikuwa na watoto 4 mke mdogo mtoto 1 na mchepuko nao mke mmoja.

Baada ya mzee kufariki aliacha nyumba 2 nyumba ya mke mkubwa ilikuwa na frame 4 na vyumba 8 huku nyumba ya mke mdogo ikiwa na vyumba 6 self tena chumba na sebule.

Wale watoto wa mke mkubwa ambao kiumri mdogo anaelekea 45 sasa huku mkwe nae akiingia kugombea mali za baba mkwe wake. Huku nyumba nyingine akifaidika mtoto wa mke mdogo na mtoto wa mchepuko.

WATOTO WA MKE MKUBWA WAINGIA TAMAA
Baada ya baba na mama yao kufariki watoto 4 wa mke mkubwa wakagawana kila mtu vyumba 2 na frame moja kila mtu ili waishi humo halafu nyumba ya mke mdogo wakawa wanalazimisha iuzwe maana ni mali ya baba yao.

Hao watoto wakatafuta hati nyingine (kwa maelezo yake) wakiandika jina la mama yao kuwa ni mmiliki wa nyumba huku nyumba ya mke mdogo wakitaka iuzwe wagawane.

WAVAMIA NYUMBA YA MKE MDOGO
Basi watoto hao wakataka kuwaondoa mama yao mdogo kinguvu kwenye nyumba iyo. Wakakodi roli na mabaunsa wakavamia na kutoa mali zote ulifanyika uharibifu mkubwa lakini kwa juhudi za wananchi baadhi ya mali zikarudi.

Basi baada ya miezi takribani 6 wale watoto wakarudi tena wakabeba mali na kuzipeleka pasipojulikana hadi leo. Pia wametolewa kabisa kwenye nyumba iyo.

Nimejaribu kufupisha tu lakini hili swala rushwa zimetembea sana hadi baraza la usuluhishi la wilaya wameshindwa.

Nawashauri tu wanaume wenzangu tuandike wosia mapema kuepusha migogoro inayoepukika kwa watoto wako.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Kama ni muislam huitaji wosia wala nini

Kila kitu kimewekwa wazi kwenye Quran. Mahakama inashirikiana na bakwata kufata maandishi ya Quran

Matajiri wa kiislam wapo kibao na wana wake zaidi ya mmoja. Ila usikii mgogoro wanapofariki kabisa.
 
Umaskini wa akili kwa watoto wakubwa.
Na bahati mbaya ni kuwa sheria inalinda zaidi watoto wadogo kuliko wakubwa.
 
Kama ni muislam huitaji wosia wala nini

Kila kitu kimewekwa wazi kwenye Quran. Mahakama inashirikiana na bakwata kufata maandishi ya Quran

Matajiri wa kiislam wapo kibao na wana wake zaidi ya mmoja. Ila usikii mgogoro wanapofariki kabisa.
Waislam ndo wanaoongoza na migogoro sasa
Shida ni baada ya mzee kufa, familia zinabadrika zinakuwa idadi ya wake, sa kila familia ilobaki wanang'angania wapate pakubwa na kila moja anaona kaonewa
 
Back
Top Bottom