Kama ushawahi kuachwa kihivi, njoo utupe mkasa

Nikiwa form 3 nilianzisha uhusiano na binti yupo form 1. Huyu binti alikua na X wake ambaye yupo form 2, wote tupo shule moja.

Yeye na ex wake walisoma primary pamoja ila jamaa alivyofaulu kuja seco akamtema binti.

Anyway, mapenzi na mimi yakanoga shule nzima ikajua. Nilikua na mashati 3 ya shule, kuna siku alinikumbatia lile shati nililovaa siku ananikimbatia sikulifua nililificha kwenye sanduku, nikimmiss nanusa shati.

Uhusiano ulikua hot mbaya, yaani ilikua siku za mitihani mmoja akimaliza mtihani anaenda kuzengea darasa la mwenzake, na mwenzake akiona tu kua partner kashamaliza na yeye anatoka muda huo huo regardless kamaliza pepa ama la.

Basi siku ikafika ilikua Alhamisi, kipindi cha mitihani, naangalia dirishani naona mchumba yuko nje tayari, nikakusanya pepa hata sijamaliza maswali nikatoka nje. Tukapiga stori mbili tatu kisha akaniambia kuna kitu ataniambia j3 tukimaliza pepa.

Nikakomaa aniambie siku hiyo, akajibu kesho ni pepa, nikamjibu kiingereza hakinisumbui aseme tu.

Akaniuliza "Unaonaje tukiachana?" Nikauliza "Hiki ndiyo ulitaka kuniambia?" Akajibu "Ndiyo"

Nikapiga magoti. Hapo tupo Sinza Kijiweni. Tupo Sinza Kijiweni na sare za shule ila mimi nikapiga magoti huku napigana na machozi yasitoke kumanina. Binti akageuka upande mwingine hata kuniangalia hataki.

Hasira zikanikaba nikainuka nikaingia ndani ya gari. Ghafla mshkaji wangu anaingia ndani ya gari ananiambia "Castr umepanda gari la Msasani" mimi ninaishi Mwananyamala wazee, kushuka nikashindwa.

Nikarudi nyumbani, lile shati nikafua.

Manina, hii ilikua ni break up iliyonijenga mno. Alhamisi nikatemwa. Jumamosi ombi langu kwa binti mmoja hata humu namuona likagonga mwamba.

Nilikua shit si kipolepole.

Binti aliitwa Mwanne.
 
Kwa hii thread yako nimekubali hlo ni funzo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daaaaah! Uzi huu umenikumbusha kitambo mno,,,,baada yakupigana na mdume mwenzangu kwakumuona anamfatilia xana manziyangu"""basi tulifumuana kinyama ila mwisho wapicha tukapelekwa kwamjumbe**mjumbe alifanya uwamuzi wakumuita manzi ili aamuwe ile kesi kwaulahisi ili yeye mjumbe asiumize kichwa,,,,,bhana weeeee manzi kaitwa front aeleze nani true boy wake
siakamtaja yule mdume mwenzangu kuwa ndo true boy wake, kwaiyo mm nikaonekana
,tokea hapo nikaapa kutokuja kufanya tena ushujaa kama huo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole mkuu... Najua itakuwa uliumia kinoma. Pole sana...!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu ungese sasa....kweli huyo ni ng'ombe


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka mi nliachwa July 2019 kwa Phone call. Kwa kweli nilimpenda sana yule binti na kwa muda mfupi nlokua naye alinichuna lakini mi nlichukulia poa kwa sababu nlimpenda saaaaaana

Baada ya kumpiga sound, Nilimsafirisha toka Dar kuja Arusha, bata mbili tatu na baadae nkamrudisha Dar huko huko kuna hela kanikopa ila hata nguvu ya kumdai sina


Akaanza kutopokea simu zangu, hajibu text, ndo ikawa nimepewa silent treatment iyooo na baadae breakup phone call

Aiseeeee nilivyokua na mipango naye nkaona kama ndoto zangu zooote zimezimika ghafla, nikaugua Insomnia, depression na anxiety juuu!

Mpaka sasa hivi bado naendelea ku-recover ila daaaaaa kuna wanawake wanajua kutu-take for granted

One day Yes!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole kiongozi hii applied to both side sema nyie wanaume mnatuachaga kimyakimya inauma hailezeki sijui kwanini tunadondokea kwa wasiothamini hisia zetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka demu wangu Chiku aliniacha kimasihara sana
Siku hiyo tulikua tupo ghetto, tunachezacheza kitandani, mara mim nikatoka nje ile narudi ndani nakuta kaweka furushi la nguo kitandani.(akili ikanikaa sawa nikahisi hapa pashaharibika) Kumbe alimaza uvunguni akatoka na furushi la nguo za kike( kulikua kuna nguo za wife mtarajiwa nikizitupia uvunguni ili uyu asizione)
Akaniuliza wee Akili hiki nin? Za nan hizi? Nikajitahidi kujitetea lakin utetezi wangu haukumtosheleza
Mwisho wa siku akanambia iviii "sikia Akili nakupa *Suspension* ya Wiki mbili ili ujirekebishe". Baada ya hapo nikaanza upya tena kujitetea nikatoa kila aina ya sababu hakutaka kunielewa.
Nlivoona na yeye amekaza basi mimi nikaamua kuleta ujeuri uliocost penzi letu
Nikamwambia "kama hutaki kunielewa basi iyo Suspension ya wiki 2 naona ndogo niongezee wiki2 nyingine jumla iwe Mwezi1" akanijibu basi nakupa *Suspension* ya mwezi baada ya hapo ndo unitafute ili nikufikirie. Akaondoka zake, nikajaribu kuendelea kumsolve lakin akakaza basi na mim nikasitisha zoezi la kumbembeleza na hata Suspension ya Mwezi ilivoisha sikumtafuta ndo tukapotezana kwa namna iyo
 
Me: hey love, morning!
Her: Hammy, naomba leo iwe mwisho kuwasiliana. Nimepata mtu hapa job na tunapendana sana. Naomba usinitafute tena.
Me: sawa, ukinihitaji nipo.
Her: never.
Me: okay

After 3 weeks
Her: hammy mpnz
Me: ......
Her: I am sorry
Me: .....

4th week
Her: hammy naomba unisamehe hata kama haunitaki, najua nlikuumiza. Pls
Me: okay
 
Una roho mbaya sana mkuu.
Samehe hao wanawake ni viumbe dhaifu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Stori yako inashabihiana na ID yako
Nahisi hicho ndio kilikuponza
Sent using my dyudyu
 
Wee jamaa bandidu sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah
...nakumbuka Kuna dem Mmoja nlimzungukia Sana Yan Sana Alikua mteja wangu. Nilipata Sana tabu kumuingiza 18 basi bhana nikaamua nimpotezee... Siku nimekaa nikakuta SMS asubuh "I love you" kutoka kwake ...sikuchelewesha nikapiga CM nikauliza are you serious akasema yes... Bas nikawa nachakata Sana Yan Sana.. After three weeks naamka asubuh Nakuta text "let's end this relationship " sikujibu mpaka Leo
kikubwa napumua tu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…