Kama upo kwenye kundi hili basi umepata hasara sana.

GRAMAA

JF-Expert Member
Nov 1, 2014
1,155
3,399
Vijana wengi kipindi hiki wameomba vyuo na wengine bado wanaendelea kuomba vyuo. Ila cha ajabu wengi wao hawajui lolote kuhusu future yao, yaani wapo wapo tu.

Utakuta kijana mpaka anamaliza kidato cha sita hata hajui chuo kikuu anapaswa kusoma nini. Kikifika kipindi kama hiki cha kuomba vyuo anabaki anadandia dandia kozi za kusoma bila hata kuzielewa kwa kina kozi hizo. PUMBAVU SANA.

SASA KAMA WEWE NI MUHUSIKA WA HAYA BASI UNAPASWA KUJITATHIMINI SANA.
1. Kama mpaka unamaliza kidato cha sita ulikuwa hujui chuo utasomea nini na sasa ndiyo unahaha kutafuta kozi ya kusoma. UMEPATA HASARA SANA.

2. Kama umeomba kozi ambayo hata huna maelezo na ufahamu nayo wa kutosha ila umeomba kwa sababu tu ipo kwenye TCU BOOK. WEWE NI HASARA KUBWA SANA.

3. Kama umeomba chuo na kozi kwa ushawishi tu wa marafiki zako au jamaa zako ila wewe mwenye ulikuwa hujui lolote. WEWE NI HASARA KUBWA.

4. Kama umeomba chuo cha private na hata hujui direct cost na ada ya chuo hicho na huku unajua kabisa kwenu ni hali ngumu ya kimaisha. WEWE NI TATIZO KUBWA.

5. Kama umeomba chuo kwa sababu tu mwaka huu hutaki kukaa mtaani na unaona chuo ni sehemu ya kupotezea muda. WEWE NI TATIZO KUBWA.

WASOMI WA KITANZANIA NI JANGA KUBWA SANA TENA SANA
 
Usikremu maisha mdogo wangu.

Wapo walioenda kusoma kozi mbali mbali kwa mazingira hayo uliyosema na wamekuwa na mafanikio sana. Na wapo ambao tangu chekechea wanapanga kusoma kozi fulani na wakaenda kuisoma lakini leo hii hawana mbele wala nyuma!

Usipende ku poinyt fingers sana mkuu maishani. Kama mambo yamekunyookea na unahisi hujapata hasara shukuru Mungu na chapa life mkuu.
 
FB_IMG_1566484468682.jpeg
 
Mkuu hongera sana kwa kuliona hili na kwa kuongezea ili kwa wazazi wote :-

Kama wewe ni mzazi na unamlazimisha mwanao kwenda kusoma kozi fulani asiyoipenda kwasababu zako tu fulani basi na wewe mzazi ni TATIZO KUBWAA.

Mkuu nimefanyia wengi application za vyuo nashangaa mtu anafika unamuuliza kozi za kumjazia na yeye anakuuliza zipi zitanifaa??

Kiufupi asilimia kubwa ya watanzania wanaishi maisha ya kimazoea sana kiasi kwamba habari ya future kwao ni kitu ambacho hawakielewi kabisa. Unfortunately hata tahasisi za elimu haliwapi somo kuhusu masuala kama haya, huwa wanapenda sana kuelezea maisha ya kusoma chuo kuliko kile unachoenda kukifuata chuo.

Mkuu tungepata viongozi wenye mitazamo na uthubutu wa kuyazungumza haya nadhan leo wasomi wasingedharaulika kama tunavyodharaulika sasa.

Na ndio maana binafsi mkuu mtu afike uniambie nina degree ya kitu fulani, nikikaa nikaongea na wewe dakika mbili tu halafu naona kabisa degree yako haendani na uhalisia wako, nikija kukutafuta tena, labda nina idea ya kukupiga hela ndo ntarudi nikushawishi nichukue pesa yako kwa idea yangu nisepe.

NI ASILIMIA NDOGO SANA YA WATANZANIA WANAOISHI NDOTO ZAO KUANZIA SHULE MPAKA KAZINI.

Kwa bahati mbaya wengi kati ya hao wachache wanojitambua huwa hawana muda na ajira.

Aisee vijana wanaoenda vyuo jaribuni kuwa wadadisi, kuweni watu wa kufuatilia vitu kwa kuuliza, kusoma na kutembea pia. Wengi wanamiliki smartphone wanaishia instagram na Facebook sasa angalia followers wao ndo hapo utaelewa anachokifuatilia huko kwenye hizo social media.

Kwa waliopo vyuo pia kuna majipu kule mengi tu.

JITHATHMINI, JITAMBUE NA UISHI KILE UNACHOKIPENDA.

Binafsi nimeanza kugombana na wazazi baada ya kumaliza form four kuhusu combination ya kusoma advance, nikaziba masikio nikajaza kile ninachokipenda, baada ya kumaliza six tena mgogoro ukaanza juu ya kile cha kusoma chuo, hapo napo palikuwa mtihani si kawaida. Tokea siku hiyo mpka leo mzazi wangu hajawai nifanyie maamuzi zaidi ya kunishauri tu na siyo kila ushauri wa kubeba.

MKUU NIKUPE HONGERA NYIINGI KWA HUU UZI WATAKAO ELEWA MAANA NA UMUHIMU WAKE MUNGU AKAWAONGOZE KATIKA NDOTO ZAO.
 
Usikremu maisha mdogo wangu.

Wapo walioenda kusoma kozi mbali mbali kwa mazingira hayo uliyosema na wamekuwa na mafanikio sana. Na wapo ambao tangu chekechea wanapanga kusoma kozi fulani na wakaenda kuisoma lakini leo hii hawana mbele wala nyuma!

Usipende ku poinyt fingers sana mkuu maishani. Kama mambo yamekunyookea na unahisi hujapata hasara shukuru Mungu na chapa life mkuu.
Haya maisha ya kuamini katika bahati huwezi toboa mkuu. Mafanikio yanatengenezwa na target ya kila mwanadamu ni kujitengenezea furaha yake halisi kutoka ndani ya moyo wake, japo wengi wanasema kila mmoja anayo maana yake ya mafanikio ila destination huwa ni moja tu ambayo ni kuwa na furaha. Comment yako inadhiirisha mtazamo wako katika maisha. Bado muda upo unaweza badili mtazamo boss.
 
Back
Top Bottom