Uchaguzi 2020 Kama upinzani ni uadui, UFUTWE!

iamokay

JF-Expert Member
Jul 13, 2019
979
2,218
Tumefika nyakati ambapo:-

Unaahidiwa kuwa ukichagua upinzani, hutapata au kuletewa maendeleo

Kuweka bendera ya upinzani kwenye duka lako ndio chanzo cha kufungiwa biashara zako zote

Kuweka bango la mgombea wa upinzani ni kujitafutia dhahama

Kumsifia mpinzani, inaonekana ni sawa na kumtukana mtawala

Vyombo vyote vya habari havimtangazi mgombea wa upinzani live

Mawakala wa upinzani ndio wanaopitia taabu zote

Kumtangaza mpinzani kashinda ni marufuku iliyowekwa kitambo sana

Wagombea mbalimbali walioenguliwa, asilimia kubwa ni wa upinzani

Wanaharakati wanaosota magerezani, na kufukuzwa kwenye ofisi zao, wote wanamlengo wa upinzani

Viongozi wa dini wanaowasapoti wapinzani, wanashambuliwa vikali na wenzao

Wanamuziki maarufu na bongo movie, wote sasa wamewapa kisogo wapinzani kwa maslahi ya kazi zao

Viongozi wa upinzani, karibu wote wana kesi mahakamani na wengine wameshahukumiwa vifungo gerezani

Viongozi wa upinzani ndio wanaopigwa na kudhalilishwa bila hatua kuchukuliwa kwa wahusika

Hoja za wapinzani bungeni ndio zinazoongoza kwa kunyamazishwa


Kama upinzani ni uadui, basi tuufute, wote tuwe chama kimoja, tupendane kinafiki, maisha yaende. Hakuna anaefurahia kusikia mpinzani kafanyiwa hiki au kile kibaya, hakuna. Sasa ili tusifanyiane ubaya, basi tuufute usiwepo kisheria kabisaaaa.

NB: Yeyote atakaeshinda, iwe ni ACT, CCM au CHADEMA. Ukishashika dola, ushauri, chakwanza futa vyama vingi. Wote tubaki kwenye chama tawala basi.
 
Back
Top Bottom