Kama unataka mali utaipata shambani

Acha uongo. 2003 LA saba then 2010 umemaliza chuo na serving ya bum 130000. Mnapeana moyo na ambayo hayapo.
Mbona nimeisha sahihisha hapo chini? Alafu sijakulazimisha uniamini ni wewe na maisha yako ila fahamu kuwa nilisoma kwa kulipwa boom la 150,000 kila mwezi mkopo asilimia 90 iliyobaki nilikuwa najilipia sikuwai kukaa hostel nilipanga mtaani nilifungua kijiwe kidogo cha chips japo biashara ilikuwa sio nziri ila faida ya buku tano ilikuwa haikosi. Mwisho nililudi nyumbani na 1,300,000/= kwahyo uniamini usiniamini ni wewe tu.
 
Bado nasema na nitazidi kusema kuwa vijana tuamke narudia tena tuamke maana tunasafari ndefu sana, tatizo letu kuwekeza kwenye miradi ya mda mrefu tunaogopa kuwa hatufaidi maana tutakufa, nani ajuaye kuishi kwake? Utaishi miaka zaidi ya 70 ukijitunza na hata zaidi sasa jifikirie utaishije miaka hiyo kama hujawekeza?

Ardhi ndo suruhisho. KAMA UNATAKA MALI UTAIPATA SHAMBANI
 
Tanzania kwnye kilimo hatuna tatizo changamoto kubwa ni masoko mfano tuna mazao mengi ambayo yanapatikana tanzania kwa wingi lakini waziri husika anashindwa kujenga mahusiano na nchi zinazohitaji hayo mazao tungekuwa tunafanya export zaidi ata haya mazao yanayouzwa hapa nchini thamani ingeongezeka sasa ndo hivyo tumebaki kuumia kila siku kila mkulima anatoka na fuso lake la nyanya mkoani wote wanakutana dar
 
Wabongo hata ukimpa somo kupitia mifano hai bado wataona uongo, cha msingi umeeleweka mkuu, katika maisha bisha kwa vitendo ndipo ubishe. Endelea kupiga kazi mdau maisha mazuri ya baadaye ni maamzi yako mwenyewe.
 
Nadhani ufumbuzi upo ndio maana humsikii mtu wa Ilula pale Kilolo Iringa analalamika humu ndani.
Usisahau tayari Ilula wana kiwanda cha kuchakata zao la nyanya "Dabaga tomato"
Jambo la msingi ni kuanza. Mengine utayakuta mbele ya safari.
 
Nilitaka kucomment..lakini ww umenisaidia nisicomment..!
 
So tuache kulima? Au tuendelee kulima ili taratibu za kutafuta masoko ziendane na uzalishaji?
 
Nadhani ufumbuzi upo ndio maana humsikii mtu wa Ilula pale Kilolo Iringa analalamika humu ndani.
Usisahau tayari Ilula wana kiwanda cha kuchakata zao la nyanya "Dabaga tomato"
Jambo la msingi ni kuanza. Mengine utayakuta mbele ya safari.
Nimeupenda ujumbe wako
 
Hebu jifunze kwa Emmanuel Mgaya. a.k.a Masanja mkandamizaji. Je ni mkulima wa Ulaya? Je, analalamikia soko? Je ana kelele za serikali? Mtu mvivu husema simba yuko njiani..
Tofauti yetu na wao ni kuwa hawa tumbo jembe la mkono,
Wana machine na kuvunia
Wana soko la kuaminika la mazao yao.
 
Nilitaka kucomment..lakini ww umenisaidia nisicomment..!
Basi sio lazima ukachukua wazo langu ila niliweka kama kujifunza. Kwa mwelewe hata hao waliofanikiwa masoko yalikuja baada ya uzalishaji kuwa juu na sio kwamba masoko yalianza hapana.
 
Hongera sana kwa kudhubutu ndugu. Omba sana uwe na afya ya mwili, roho na nafsi na usimsahau Mungu wako kwa kufanikiwa
Amen, ntakutafuta Pm kwa ushauri wa kilimo.
 
Nadhani ufumbuzi upo ndio maana humsikii mtu wa Ilula pale Kilolo Iringa analalamika humu ndani.
Usisahau tayari Ilula wana kiwanda cha kuchakata zao la nyanya "Dabaga tomato"
Jambo la msingi ni kuanza. Mengine utayakuta mbele ya safari.

Hahhaa kwa hapa una lack of information mkuu...nahakika huelewi sana kuhusu kilimo...!hyo dabaga ipo toka mie nakua...najionea uvv kucomment kwa kirefu...!limeni sie tutanunua mazao fullstop
 
Tulisoma uchumi hata kidogo huwa tunaamini kwa 100% kuwa unapozalisha sana ndipo na soko litafuatwa ila haliwezi kuanza soko kabla ya kuzalisha.

Mfano iringa miaka ya nyuma miti ilibakia kama mapambo ila masoko ya mbao yalipofunguliwa baada ya kuona uzalizaji upo juu wazee wetu na sio vijana walianza kula maisha na walijenga na usafiri wakapata na walisomesha.

UZALISHAJI KWANZA SOKO LITAFUATA
 
Nadhani ufumbuzi upo ndio maana humsikii mtu wa Ilula pale Kilolo Iringa analalamika humu ndani.
Usisahau tayari Ilula wana kiwanda cha kuchakata zao la nyanya "Dabaga tomato"
Jambo la msingi ni kuanza. Mengine utayakuta mbele ya safari.
Ndo mana nasema kama tungekuwa tunaexport zaidi mazao hasa ya biashara thamani ya mazao inge ongezeka
kuletwa kwa kiwanda ni kama kumetatua Changamoto kidogo na sio kumsaidia mkulima kuwa tajiri nimejibu kulingana na mtoa mada anavyosema mali ipo shambani akati watanzania wanakabiliwa na changamoto nyingi
 
Pole, endelea kuwekeza pesa tutakutana sokoni, kifupi wanunuzi pia wanahitajika ili mzunguko wa pesa uwepo hivyo kama umeamua kukaa upande huo ni jambo jema.
Kuhusu Dabaga. Ni kweli kipo lakini mimi nakizungumzia kile kilichojengwa hivi karibuni mara tu baada ya kumaliza mlima kitonga. Kama kungekuwa hakuna uhitaji huo sidhani kama kingejengwa.

Halafu tambua kusafirisha nyanya kuja Kariakoo au Buguruni ni hiyari ya mkulima anaweza akauza pale au akasafirisha kutegemea na bei anayo ona inamlipa.
Hahhaa kwa hapa una lack of information mkuu...nahakika huelewi sana kuhusu kilimo...!hyo dabaga ipo toka mie nakua...najionea uvv kucomment kwa kirefu...!limeni sie tutanunua mazao fullstop
 
Umeeleweka mkuu.
Lakini Export si inakuja baada ya production? Pale ambapo soko la ndani limezidiwa bila shaka njia ya nje itajitokeza tu, je unajua Mchele kutoka Kyela unauzwa Kenya? Unajua kuwa mahindi ya Mbeya yanauzwa Zambia na Kongo?
 
Ngoja turudi tukawape wazee wetu zawadi walai mi ntawapelekea hata tecno smart nione
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…