stickvibration
JF-Expert Member
- Feb 7, 2017
- 3,226
- 5,150
Ulichoandika kimejaa busara na hekima ya hali ya juu sana. Lakini kwa kundi la watu walio humu utapata wachangiaji wachache sana.! Ila ungeandika lolote la kumtukana ama kumkashfu Magufuli ama Paul Makonda,, wachangiaji wangekuwa tayari mia kadhaa.
Mkuu kama ulivyosema, kuna tatzo mahali ni kweli, yani mtu unaweza kujitoa sana kulima mwisho wa siku soko linashuka na unapata hasara, kwa mfano mwaka juzi kuna jamaa yangu alilima mbaazi hapo morogoro, baada ya mavuno zikakosa soko, na ukizingatia aliwekeza nguvu na mtaji wa kutoshaKuna tatizo kubwa nchi hii. Kuna jamaa kalima heka 100 za zao la mahindi kwa kutumia vifaa vya kisasa na aliwezeshwa na benki. Baada ya kuvuna ikawa kuna zuio la kuuza nafaka nje ya nchi. Bei ya mahindi ilishuka sana na akauza kwa hasara na hakuweza kurudisha pesa ya mtaji. Sasa hivi analia na deni. The foundation of this counry was not right. Kuna tatizizo mahali fulani na bahati mbaya sana wanaotuongoza miaka yote hiyo ni hao hao na ni ngumu wao kubadilika ndiyo maana wanakomaa na wapinzani bila sababu yoyote.
Unfortunately kuna watu nilisoma nao shule na kwa ajili ya nepotism na god father wakawa makatibu wakuu wa wizara fulani katika awamu zilizopita.. Kwa vile nilikuwa ninawafahamu kwamba walikuwa hawana uwezo hata wa kuwa wakuu wa wilaya nikasema kweli nchi yeu iko upside down. Mtu kama yule utampaje cheo kikubwa kama vile. I don't know when we shall move forward. Try to examinie leadership of this country since independence, there is nothing to celebrate. I was employed in goverment baada ya shule na wizi niliououkuta huko ukifanyika daylight bila hofu ulikuwa unatisha. Dhamiri yangu haikuniruhusu na nilijiondoa mwenyewe na kuondokai serikalini. Kitengo nilichokuwepo kilikuwa kinapokea pesa ya wafadhili lakini zilikuwa zinaliwa sana kwa njia ya ulaghai tu ndiyo maana hakuna maendeleo yanayotokana sana na misaada. Labda zile wanazokuja kusimamia wenyewe.
We unaheka ngapi mkuu, usije kuwa unatuzuga.Kilimo kizuri ila soko.Mahindi yamejaa hayana soko.Mwaka juzi wakulima wa mbeya viazi viliozea shamba.Wazungu ni wanafiki sana.Sisi tunalima wao wanatupangia bei lini tutatoka?Tunatakiwa tuwekeze katika teknolojia ili tuuze bidhaa zilizo sindikwa na si ghafi.Waafrika kinachotukwamisha ni teknolojia hakuna kingine, muangalie moe, bakhresa wote si walimaji wakubwa ila wachuuzi wakubwa na wanapepea kwa utajiri unaotokana na jasho la wanyonge.Mi naamini serikali ikitilia mkazo sera ya viwanda wakulima watatajirika.c&p
*BAADA YA MIAKA 20 MTAKUJA TANZANIA KUOMBA KAZI*
Nilipokuwa mwanafunzi nchini Poland miaka ya 90, tulikuwa na tabia ya kwenda Sweden wakati wa likizo na kufanya vibarua mbalimbali hasa kwenye mashamba ya wakulima. Watanzania kutoka nchi mbalimbali za Ulaya Mashariki tulikuwa na sehemu zetu tulikokuwa tunakutana na kufanya vibarua hivyo kwa malipo ambayo kwa mwenyeji yalikuwa madogo sana lakini kwa sisi toka Ulaya ya Mashariki ya wakati huo yalikuwa makubwa sana. Tukirudi Poland na hizo nchi zingine na dola zetu, basi tunaanza kuishi kama watoto wa mfalme wa Nsesi. Pombe kwa wingi, watoto wa kizungu, na sherehe kila weekend.
Hao wakulima wa Sweden walikuwa watu wa kawaida wenye elimu za chini lakini wakiwa matajiri wenye mashamba makubwa makubwa na machine kubwa kubwa. Sisi vibarua wao tulikuwa na elimu kubwa kubwa, wanafunzi wa Ph.D, Masters, Degrees. Tulikuwa engineers, madaktari, wanasheria, wachumi nk.
Siku mmoja boss wetu huyo mkulima akawa anapiga story na sisi na kuanza kumwuliza kila mmoja anasomea nini. Tukamwambia maelimu yetu makubwa makubwa. Tulipomaliza akasema yeye elimu yake ni ya msingi ambayo ilikuwa kama form four ya Tanzania lakini ana mashamba na anaweza kutuajiri sisi Wasomi. Akaendelea kusema amefika Tanzania mara nyingi na ni nchi nzuri sana na hali ya hewa nzuri kwa kilimo na uwekezaji mwingine. Anashangaa kwanini ni maskini hivyo mpaka wasomi wake tunakuja kufanya vibarua mashambani ili kujiongezea kipato? Akasema Sweden peke yake imeisaidia mno Tanzania lakini haoni tukisogea mbele.
Alichomalizia ndio kimenifanya niandike leo. Akasema tukibadilishana watu leo. Waswedish wote wakaenda Tanzania na mikono yao mitupu na Watanzania wote wakaja Sweden na mikono yao mitupu. Baada ya miaka 20 Tanzania itakuwa nchi tajiri na Sweden itafilisika na kuwa nchi maskini na mtaanza kurudi Tanzania kuomba vibarua.
Ukweli mwingine unauma lakini hubaki kuwa ukweli. Ni miaka karibu 25 toka tuambiwe hayo na bado Sweden ni nchi tajiri na Tanzania ni nchi maskini. Zile elimu zetu kubwa kubwa hazijatusaidia kitu. Naendelea kutafakari. Yule Mzungu ni kama alikuwa sahihi.
Tunakosea wapi watanzania na nani atakuja kutwambia kuwa sio kila kitu uwe na mtaji bali kama ardhi ipo basi fulsa ya kwako wewe ni kuwa na afya njema. Jifunze kuumia ili baadae uje uwaajili wasomi na wakuite bosi.
Bado nawakumbusha vijana rudini vijijini mkatumie ardhi ya familia ipasavyo na ukipata nafasi nunua pia ardhi itakusaidia. Limeni kila aina ya mazao yaani mazao ya mda mrefu miti nk na mazao ya mda mfupi mbogamboga na matunda.
KAMA UNATAKA MALI UTAIPATA SHAMBANI
Hongera mkuu hayo ndo mawazo. Vijana tuamke fulsa afya tu mashamba yapo vijijini ila kukaa dar bila malengo na umri unaenda ni mzigo kwa watotoMm nafikili ulimaji wa miti ni wazo bora kabisa ukilinganisha na mazao mengine ambayo ukivuna ukakosa soko basi yanaishia kuoza, miti unaweza vuna pale utakapokuwa na wakika wa mteja, pia mazao ya misitu uwa ayashuki bei. Mm pamoja na umasikini wetu baba yangu aliacha eneo kubwa sana ambalo lilikuwa sio kitu kiasi kwamba ata wale wanaogombania mirathi awakujishughulisha nalo ilikuwa 2003 wakati mzee anatutoka na mm nilikuwa darasa la saba. Nimesoma nimemaliza chuo 2010 nikakuta eneo bado lipo wazi ni vichaka vichaka tu, nililudi kutoka chuo na saving yangu ya boom kama 1,300,000/= nikawaza nikawazua hii pesa itanisaidia nini? Nikaona bora nianzishe shamba la miti aina ya karibea, nimepanda miti mm na wadogo zangu, miti ya 1,000,000/= ila eneo alikuisha baada ya mwaka mmoja nikapata dili yakunipa laki tano kila mwezi ikabidi kila mwezi napanda miti ya laki mbili kwahyo ukiangalia shamba langu miti inazidiana ukubwa kwahyo ata nikianza kuvuna nitakuwa navuna kwa awamu. Bado miaka miwili mbele nianze kupiga pesa. Sina gari marafiki zangu ambao tunachakalika pamoja kitaa uwa wakiona pesa tunatengeneza ila mm ata pikipiki sina wanafikili ninaonga mademu kumbe mm nimewekeza wao wamenunua magari. Uzuri wa kilimo cha miti wewe unafanya kupanda tu unaendelea na mambo yako mengine utaludi kufanya pruning. Vijana amka limeni miti mm ilo shamba nitapiga pesa mpaka watanitumia takukuru wakifikili nimekwapua sehemu kumbe nilijiongeza mapema.
Likizo zangu zote huwa nachukua kipindi cha mvua hivyo huwa napiga jembe haswaaaa na ukinikuta kijijini hutaamini kuwa ni mimi. Kuna mda watu hunishangaa kuwa kwa nn najitesa hivi? Huwa nawajibu naishi nikiangalia miaka 30+ huko mbeleniwewe mwenyewe mtoa mada umeajiriwa mbn uachi Kazi ukalime
Huwa silimi mahindi ila mashamba ya miti yapo zaidi ya eka 20+ na bado napanda kila mwaka eka 1 au mbiliWe unaheka ngapi mkuu, usije kuwa unatuzuga.Kilimo kizuri ila soko.Mahindi yamejaa hayana soko.Mwaka juzi wakulima wa mbeya viazi viliozea shamba.Wazungu ni wanafiki sana.Sisi tunalima wao wanatupangia bei lini tutatoka?Tunatakiwa tuwekeze katika teknolojia ili tuuze bidhaa zilizo sindikwa na si ghafi.Waafrika kinachotukwamisha ni teknolojia hakuna kingine, muangalie moe, bakhresa wote si walimaji wakubwa ila wachuuzi wakubwa na wanapepea kwa utajiri unaotokana na jasho la wanyonge.Mi naamini serikali ikitilia mkazo sera ya viwanda wakulima watatajirika.
İmefika muda wasomi kuungana na kuanza ku export vinginevyo tutalia sana na suruhu haipo.Wabunge wetu hawaisimamii vizuti serikali wanaisapoti tu lakini hatuoni mkulima kuinuka,.Jamani wakenya wapo mbali, wanaexport parachichi, wanaexport macademia nasikia hadi mboga mboga.Kwa nini watanzania tunashindw, mtanzania soko lake analowaza ni kariakoo tu.Hivi ndizi zikilimwa ipasavy huko tukuyu, moshi, arush, kagera, moro, pwani, kgm nk soko la Dar linaweza mudu kweli? Tujadili kwa kutafuta suluhu.Ardhi tunayo dhamira tunazo ila mbele ni giza nini? Tumebaki kulaumiana tu.Mkuu kama ulivyosema, kuna tatzo mahali ni kweli, yani mtu unaweza kujitoa sana kulima mwisho wa siku soko linashuka na unapata hasara, kwa mfano mwaka juzi kuna jamaa yangu alilima mbaazi hapo morogoro, baada ya mavuno zikakosa soko, na ukizingatia aliwekeza nguvu na mtaji wa kutosha
Panda na miti ya matunda huta juta, na haina gharama.miti peke yake ina risk ya moto, watanzania wanachoma hovyo, panda miti yote hutajuta, mazao ya msimu ni kupotesmza muda tu.Una vision sana elimu imekukomboa.Kama ni sehemu ya joto panda na mitiki.Huwa silimi mahindi ila mashamba ya miti yapo zaidi ya eka 20+ na bado napanda kila mwaka eka 1 au mbili
Iringa baridi sana mkuu. Kuna shamba nimenunua lipo bondeni nahitaji kusafisha ili mwakani nikapande parachichi.Panda na miti ya matunda huta juta, na haina gharama.miti peke yake ina risk ya moto, watanzania wanachoma hovyo, panda miti yote hutajuta, mazao ya msimu ni kupotesmza muda tu.Una vision sana elimu imekukomboa.Kama ni sehemu ya joto panda na mitiki.
Inategemeana na rutuba ya shamba na shamba lipo eneo gani kama pametulia hakuna upepo hata miaka 2 unavunaSorry I was wrong kwenye kumaliza chuo niliandika mwaka wakuanza chuo 2010 ndo nilianza chuo 2013 nilimaliza chuo mkaribea mpaka uvune nimiaka kumi nakuendelea toka umeipanda. Mambo nimengi muda ni mchache.
Nafikiri Mwafrika ana upungufu katika processing ya constructive ideas kwenye ubongo.
Mkuu ukiwa hai nicheki 2025..