Kama unatabia ya kuokota mademu usiku, sona hii

Kuna mjita mmoja nimemwokota jana katikati ya tukio akaanza kunipiga vibao,na kusumbua ikabidi nimpige vice Kisha niongeze maarifa ya kushughulikia lile pepo baya ili lishindwe na lilegee.
Hata hivyo kwenye pilikapilika hizi za kudhibiti pepo wa huyu binti, nasikitika Anko Kipara aliishia kupata injury kwenye frontal lobe,tragic!
Tuweni makini aisee....
 
Jana mida ya saa nane nikiwa maeneo ya sinza kwa meeda,nilipiga bia zangu kadhaa,pembeni nikamuona binti,mrembo.nikabonga naye akaonekana katokea nje ya dar na ni mgeni.nikakubaliana naye twende gheto mitaa ya ubungo external kufika gheto.ile kushikana shikana ghafla demu kaanza kunyoosha mikono huku anatetemeka.mikono ikamkakamaa akaanza kupiga mayowe huku anaongea lugha za ajabu.duuuh,wapangaji wakaamka.sasa humu ndani kwangu bachelor nipo alone na baba mwenye nyumba ni mshenga wangu kwa binti mmoja ambaye nimetoa posa.Baba mwenye nyumba pamoja na wapangaji wakanigongea kufungua binti katoka uchi huku anazungumza lugha zilezile.ikabidi ashikwe na jirani yangu mmoja ni mlokole akaanza kuombea,akaniuliza mkeo kaanza matatizo lini .........kwa aibu nikasema kaanza leo usiku.Baada ya kutulia majini nikaita boda boda fasta imchukue mi sitakagi ujinga
Hakukuibia?
 
Aiseee umenikumbusha mbali sana Mimi inshi kama hiyo ilinitokea kwa Binti flani nilikuwa maeneo ya beach naogelea. Nikamwomba Dada mmoja kampani ya kuoga nae akakubali ile anaingia kwenye maji tu akaanza kupiga kelele nikastuka. Kumbe alipandisha mashetani .tokea hapo nimekoma kuomba kampani na watu nisiowajua
 
Ukijitahidi unaweza kuwa memba wa Operesheni Fichua Maovu (OFM) ya Shigongo na ukawa unarusha stori zako moja kwa moja kwenye Ijumaa Wikienda!!!
 
Jana mida ya saa nane nikiwa maeneo ya sinza kwa meeda,nilipiga bia zangu kadhaa,pembeni nikamuona binti,mrembo.nikabonga naye akaonekana katokea nje ya dar na ni mgeni.nikakubaliana naye twende gheto mitaa ya ubungo external kufika gheto.ile kushikana shikana ghafla demu kaanza kunyoosha mikono huku anatetemeka.mikono ikamkakamaa akaanza kupiga mayowe huku anaongea lugha za ajabu.duuuh,wapangaji wakaamka.sasa humu ndani kwangu bachelor nipo alone na baba mwenye nyumba ni mshenga wangu kwa binti mmoja ambaye nimetoa posa.Baba mwenye nyumba pamoja na wapangaji wakanigongea kufungua binti katoka uchi huku anazungumza lugha zilezile.ikabidi ashikwe na jirani yangu mmoja ni mlokole akaanza kuombea,akaniuliza mkeo kaanza matatizo lini .........kwa aibu nikasema kaanza leo usiku.Baada ya kutulia majini nikaita boda boda fasta imchukue mi sitakagi ujinga
UKOME
 
aseee me nlikua na mmoja geto akipiga bao anazimia nliogopa sana nimekoma
 
Unaoneka kuwa Mtunzi mzuri wa riwaya. Ila umekosea kidogo uliposema mpangaji mwenzio mlokole alikuliza "mkeo alianzwa lini...' Kiuhalisia asingestahili kuuliza kwa vile mnaishi nyumba moja na anajua hujaoa
kasema jirani yake mmoja sio mpangaji mwenzake, au me ndo sijaelewa sijui.......
 
Kama umeishi nyumba za kupanga utaelewa jirani ya mpangaji ni nani.
Jirani ya mwenye nyumba ni mwenye nyumba mwingine, lakini jirani ya mpangaji ni mpangaji mwenzake kwenye nyumba hiyo hiyo.
 
Unaoneka kuwa Mtunzi mzuri wa riwaya. Ila umekosea kidogo uliposema mpangaji mwenzio mlokole alikuliza "mkeo alianzwa lini...' Kiuhalisia asingestahili kuuliza kwa vile mnaishi nyumba moja na anajua hujaoa
Heshima yako mkuu.
 
Back
Top Bottom