Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,059
- 79,416
KAMA UNAPATA UGUMU KUPATA PESA; FUATA NJIA HIZI KUWA NA PESA.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Elewa, pesa sio utajiri. Utajiri ni Afya, Muda na Rasilimali. Money is just a tool to get them(afya, Muda na Rasilimali).
Bila kupoteza wakati. Zifuatazo ni njia za kupata pesa na kujiweka katika nafasi ya kuwa tajiri;
1. Jiongezee thamani yako.
Mtu ni wewe. Mtu ni mawazo yako. Mtu ni kile unachokifanya. Mtu ni vile unavyoonekana. Mtu ni vile unavyozungumza.
a) Ongeza thamani yako kwa kuboresha kile unachokifanya, kifanye kwa ubunifu, kiwe kitu kizuri,
b) ongeza ujuzi na elimu yako kwa shughuli zinazokuzalishia kipato.
Kuza jina Lako.
Pesa huwatumikia watu waliojiongezea thamani.
2. Pata Ujuzi na Elimu ya Fedha( Financial skills and intelligence).
Jifunze namna na njia sahihi ya kupata pesa.
Jiimarishe kwa kujua namna ya ku-manage pesa.
Jielimishe, njia za kuzizalisha na kuwekeza pesa ili upate zaidi.
3 Jenga mahusiano yenye Tija na Mtandao Bora.
Money psychology+ Money Attitude + Money network= Wealthy.
Kadiri unavyozungukwa na network Bora unajiweka kwenye nafasi Bora.
Jinsi ya kuunda mtandao Bora WA kifedha hilo ni Somo la siku nyingine.
4. Ijenge Saikolojia na mtazamo wa kitajiri.
Elewa, utajiri sio kuwa tuu na pesa bali ni vile mtu anavyojihisi.
Miongoni mwa saikolojia na mtazamo wa kitajiri au wenye pesa.
a) Pesa sio Mungu ila ni silaha ya kumfikia Mungu.
b) lengo ni kuwa tajiri na sio kuonekana tajiri.
c) Privacy; utajiri unahitaji mtu mwenye mtazamo wa kulinda mambo yake nyeti hasa ya kiuchumi na kimahusiano kuliko kuya-expose nje.
Tajiri hata usipojua anapoishi au nyumba yake au Mali zake kwake ni advantage kuliko ukijua.
Moja ya dalili yakuwa unasaikolojia ya kimaskini ni kupenda kuonyesha Mali zako hasa kuliko pitiliza.
d) Kukusanya zaidi ya kutumia. Saikolojia ya utajiri inahita mtu awe na viashiria vya ubahili kwenye matumizi yasiyoongeza kipato ila awe mzuri kwenye uwekezaji.
d) Kukutana na mtu mpya kuwe na tija na sio kukutana kwaajilo ya kufurahia kijamii.
Attitude ya mtu tajiri hawezi kukuambia tukutane mkaongea tuu mambo ya kijamii. Yaani mtu akuambie tukutane Coco Beach au Mlimani City just kupiga stori tuu. Ukiona tajiri amekuita basi ujue kuna fursa ameiona na anataka aitumie kwako mpate wote au akutumie tuu. Ukiwa Mjinga hupati kitu.
e) Pesa inawatumikia na sio wao waitumikie.
Pesa ni nyenzo au silaha kwa wenye Money psychology. Lakini kwa wengine wao ndio silaha au nyenzo inayotumikishwa na pesa.
f) Kufanya kazi sana sio kupata pesa. Ila kuweka mitego sahihi na timing ndio kupata pesa.
5. Kumiliki na kutawala Muda.
Niliwahi kuandika, Miliki watu upate utajiri.
Huwezi kuwa tajiri kama humiliki Muda.
Kumiliki Muda ni kutumia Muda wa watu wengine.
Kadiri unavyotumia muda wa watu wengine unajiweka katika nafasi ya kuwa tajiri.
Muda ni utajiri.
6. Tumia udhaifu wa wengine kujinufaisha.
a) Mtu mjinga mtumikishe akutumikie kisha mpunje Mshahara. Mtu mjinga huwezi kumpa malipo makubwa.
b) Mtu mwerevu lakini Mwoga, mtumie kwa akili, MPE malipo angalau ili aendelee kukutumikia.
c) Mtu Jasiri lakini Mjinga, usimtumie kwa kazi za muda mrefu. Mpe vibarau vya Muda mfupi lakini mpe hela kiasi ambayo ataiona nyingi.
Lengo la kukusanya utajiri sio kukomboa watu bali kuwafanya wengine wasiwe matajiri kama wewe.
Chukulia mfano; Kuna shamba la hekta 100. Na wewe na wenzako mpo Mia Moja na wote mnataka mpate portions katika shamba hilo. Lakini wewe na miongoni mwa wenzako unataka kupata eneo kubwa zaidi. Unafikiri utasaidia wengine wapate kama wewe? Yaani kila mmoja hekta mojamoja?
Unaposema utajiri indirectly umetaja umaskini.
Mkiwagawana wote kwa usawa automatic hautaitwa utajiri.
Acha nipumzike
Robert Heriel
Kwa sasa Dar es salaam