Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,806
- 15,369
Tendo la ndoa linapopewa uzito mkubwa kwenye uhusiano wivu ni lazima utakuwa mkubwa. Mtu akiacha tendo la ndoa na wivu huondoka. Wapenzi ambao hawapendani na kufikia mahali hakuna anayetaka kusikia kuhusu tendo la ndoa, kamwe hawaoneani wivu. Unafikiri ni kwa nini? Ni kwa sababu wivu unatoka kwenye tendo la ndoa na siyo mahali pengine.
Kwa hiyo ukitaka kuacha wivu inabidi ulibadili swala la tendo la ndoa liwe upendo. Kama ukipenda mtu ile kumpenda tu ni dhamana na usalama wa kutosha kuwa hatakwenda kwa mtu mwingine. Kama kweli unampenda mtu utajua kwamba huwezi kwenda kwa mtu mwingine. Lakini kama akienda ujue hakuna upendo na huwezi kufanya lolote ameamua kwenda ni yeye. Hata kama utaamua kumuua bado haina maana kwa sababu maiti haina matumizi yeyote ya maana huwezi kuipenda.
Kama kuna wivu ujue kabisa hakuna upendo bali hapo kuna tamaa ya mwili ambayo imefichwa nyuma ya neno kupenda. Kilichopo kati yenu ni tendo la ndoa tamaa ya mwili lakini siyo upendo. Mtu anayependa analijua jambo hili kwa sababu hana wivu. Hivyo hana shida ya kukagua simu ya mwenzake kuchakura mifuko au mikoba yake au kumtumia watu wamlinde.
Hatukufundishwa kupenda na hivyo wengi hatujui hata kupenda maana yake ni nini. Tumefundishwa kwamba watu wawili wakisema ni wapenzi jambo linalo wafunga ni tendo la ndoa. Ndiyo maana unaweza kusikia yule mwanamke aliyemuoa alikuwa Malaya sana nguvu inawekwa kwenye tendo la ndoa siyo mahali pengine. Lakini huyu Malaya anapopenda hawezi tena kuwa Malaya. Kama alikuwa Malaya ni kwa sababu hajawahi kupenda. Watu wanaishi kama hawaishi, wanaishi kwa kuogopana. Kila mmoja anamwogopa mwenzake anaamini kwamba atatoka atamwacha. Unajiuliza ni kwa nini hawa watu wanaishi pamoja kama wanaogopana? Lakini siku zinaenda na maumivu yanaendelea.
Kumbuka kwamba uaminifu upo au haupo. Kama haupo huwezi kuulazimisha kwa kutumia wivu. Wivu ni dhana ya kujaribu kuleta uaminifu lakini haina nguvu hiyo. Kama uaminifu upo basi hapo kuna kupenda. Kama uaminifu haupo huwezi kuuleta wewe. Ni bora kujitenga kwa sababu huamini kwamba unaweza kuishi bila huyo mwenzio, kwa hiyo unajaribu kulazimisha kutafuta uaminifu.
Kama hakuna uaminifu basi hakuna haja ya kufanya uharibifu, Una haja ya kujua tu kwamba huyo mwenzako ambaye unampenda hawezi kupokea upendo. Kumbuka upendo wako unapomwagika kila ukiutoa inachosha. Huna haja ya kuchoka au kuumia .. toka