Kama Ufisadi ulivyotanguliwa na Ulanguzi tutegemee nini baadaye?

DoubleOSeven

JF-Expert Member
Jul 5, 2008
661
143
Napenda kunukuu yaliyowahi kusemwa na aliyekuwa Waziri Mkuu JMT hayati Sokoine kwamba;
1. TUMERUHUSU walanguzi na Wahujumu uchumi kuongoza nchi
2. Walanguzi na Wahujumu uchumi ni maadui wa taifa na ni lazima kuwapiga vita na kuwatokomeza waelekezwe katika shughuli za kilimo ili waweze kuishi kwa jasho lao
3: Tabia ya rushwa na magendo inavuruga haki za wananchi na kupunguza imani ya wananchi kwa serikali, vyombo vyake na hata Chama tawala na kutokana na hali hiyo SERIKALI ILIKUWA IMEKWENDA LIKIZO

Haya yalisemwa 1983 na baadaye ikaja operesheni dhidi ya WALANGUZI. kILICHOFUATA HAPO KINAJULIKANA.
Leo hii, takriban miaka 30 baadaye tunasumbuliwa na MAFISADI, yaani wale waliojulikana kama WALANGUZI, wamejikuza katika hujuma zao dhidi ya uchumi na maovu mengine na ku-graduate kwenye UFISADI ila safari hii wakiwa ndio CHAMA tawala. Serikali bado iko likizo. Baada ya UFISADI tutegemee nini?
 
Back
Top Bottom