Kama UDA iliuzwa kifisadi mbona mtukufu ameibariki?

Jan 15, 2017
50
64
Wasalam, kuna taarifa kwamba CCM chini ya Didas masaburi waliuziana UDA ili kujinufaisha kama walivyojinufaisha kwa kupora viwanja vyama mipira na kujimilikisha. Swali langu je mtukufu hana taarifa hizi za zabuni bubu au ndo funika kombe mwanaharamu apite? Iweje aagize matumizi ya fedha hizi ambazo zinanuka ufisadi? Mwenye kujua naomba anifafanulie hili maana lina ukakasi.
 
Mvinyo ni ule ule unaotengenezwa kiwandani Lumumba. Oktoba 25, 2015 ilibadilishwa chupa tu.
Tangazo lao lingekuwa hivi, "Ladha ile ile unayoifahamu lakini sasa katika muonekano mpya. Haiuzwi kwa walio chini ya uwezo wa kujitambua".
 
Wizi wa Makaburi ni makaburi ya kale hayafukuliwi,na Muhusika Mkuu ni wa Kunyumba,siye Sera na Ilani yetu ni kuhakikisha Kaskazini wanalimia meno.Na tumeanza na Mbowe huyo wa CCM hakuna shida kwanza ndiyo Sera yetu kubwa kuliiibia Taifa.Aliyekwambia tunapiga vita rushwa na ufisadi nani??Kama yupo muulize nani yupo nyuma ya Meli Mbovu na Zile Bilioni nane?
 
mkuu wenu kabariki ufisadi wa UDA kwakuwa hana dhamira ya dhati kwenye mapambano dhidi ya mafisadi.

Ile mahakama ya mafisadi aliyohubiri nchi nzima imeishia kuwa makazi ya popo na mbayuwayu.

"wazee wangu nawahakikishia kamwe sitafukua makaburi" By JPM
Umesahau kuwa ni kutoka Ku nyumba aka.mnyalukolo wange
 
Waliosema muda ni rafiki wa ukweli utawaelewa walichomaanisha sasa, pia utamwelewa aliyesema ccm hakuna msafi!
Kwani zile Bilioni nane za Meli Mbovu nani yuko nyuma??Tukifukua makaburi hata siye tunaofukua tutafukiwa
 
Mkulu kasha onjaa inchi mwanzo alikua ajazoea ofisi ila ndo maana ukaona akisema uwezi kuvumilia mikataba ya ovyo ovyo ila sasa anasema kila mtu atabeba msalaba wake
 
Kama Lowasa yupo kwenye List of shame ya chadema,
Iweje tena chadema hao hao wamtembeze nchi nzima kumuombea kura awe rais wa Tanzania??

Kwa tope hili hata kama ni lofa utazinduka
 
mkuu wenu kabariki ufisadi wa UDA kwakuwa hana dhamira ya dhati kwenye mapambano dhidi ya mafisadi.

Ile mahakama ya mafisadi aliyohubiri nchi nzima imeishia kuwa makazi ya popo na mbayuwayu.

"wazee wangu nawahakikishia kamwe sitafukua makaburi" By JPM
Asante sana mkuu .
 
Siamini kama Jpm amebariki uuzwaji huu wa kifisadi wa UDA na kama akibariki basi atakuwa amechagua ndani ya uraisi wake kufanya siasa za kichama badala ya kujenga nchi
 
Mvinyo ni ule ule unaotengenezwa kiwandani Lumumba. Oktoba 25, 2015 ilibadilishwa chupa tu.
Tangazo lao lingekuwa hivi, "Ladha ile ile unayoifahamu lakini sasa katika muonekano mpya. Haiuzwi kwa walio chini ya uwezo wa kujitambua".
Teh, teh ....! Nimeipenda hiyo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom