Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,390
Wadau, amani iwe kwenu.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuna Waziri na Msemaji wa Wizara. Pia kila taasisi ndani ya wizara hiyo iwe Jeshi la Magereza, Zimamoto, Uhamiaji na Polisi wana msemaji wao ambaye ndiye hutoa ufafanuzi pindi hoja inapoibuka inayohitaji ufafanuzi.
Hiyo haipo kwa TISS. Wanafanya kazi kubwa sana katika kulinda amani ya nchi hii na kuzuia matukio kabla hayajatokea. Ni kutokana na kazi zao ndio maana Tanzania inakuwa nchi ya mfano Barani Afrika kwa kuwa na amani na utulivu. Ukiona vyaelea ujue vimeundwa. Hawa jamaa hawalali na kila mahala wapo. Wanawajibika usiku na mchana kuhakikisha kila mtu analindwa na anatendewa haki.
Kwa sasa imekuwa ni kama fasheni kila mtu anaibuka na hoja na kujifanya anaijua sana TISS na kuihusisha na kila jambo baya linalotokea katika nchi hii. Waandishi wa Habari, wanasiasa na hata wasanii ambao hawajui hata nini maana ya TISS ndio hujifanya wanaijua sana Taasisi hiyo ambayo nina hakika hata viongozi wakuu wa nchi hawaijui na hawatakuja kuijua kwa vile na wao ni sehemu ya watuhumiwa wa taasisi hiyo.
Kila mtu ana uhuru wa kuongea. Ila uhuru usio na mipaka ni vurugu. Kutokana na TISS kuwa na muundo ambao haulazimishi kazi zao kutangazwa kwenye public, kumetoa mwanya kwa ngumbaru wa taasisi hiyo kujitokeza na kujifanya kuwa wasemaji. Hawana Waziri mwenye dhamana ya moja kwa moja na Taasisi yao. Hawana Msemaji wa Taasisi. Hawana Bajeti inayoonekana. Hawana specific goals ambayo public inaweza kuwajudge. Kwa ujumla TISS ndio kila kitu katika nchi hii.
Kwa upande wangu siamini kama TISS ni wauaji, watesaji na wanyanyasaji kama wengine wanavyosema. Siamini kama TISS inajihusisha na utekaji kama wengine wanavyodai. Ninachojua TISS kote ulimwenguni huwashughulikia wavurugaji wa amani na hufanya hivyo kabla wahusika hawajafanya tukio. Tena wanakushughulikia hadharani na hata ukipiga kelele hakuna atakayekutetea.
Wale wote mnaolalamikia kuwa TISS inaua na kutesa watu, mna uhakika na hayo msemayo? Hivi kama TISS inamshughulikia kila mtu, mbona Mgombea wa CHADEMA, 2015, Edward Lowasa na Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani, Frederick Sumaye wanalindwa na maafisa Usalama wa Taifa? Kama lengo ni kuua wapinzani, si hao walinzi wangewatumia kuwafyatulia risasi ama kuwapa sumu ili wakufilie mbali?
Kuna wakati Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe aliwahi kutekwa na nusura auawe. Ni Maafisa wa Idara ya Usalama wa Taifa ndio waliomuokoa na Mbowe anajua hayo.
Kuna wakati Zitto Kabwe aliwahi kuwekewa sumu kwenye Maji ya kunywa pale Lunch Time Hotel na aliyehusika kuweka sumu hiyo ni Ben Saanane. Ni Maafisa wa Idara ya Usalama wa Taifa ndio waliofichua mkakati huo na Zitto analijua hilo. Ipo mifano mingi sana na laiti kama hawa Maafisa watatoa ushuhuda wa jinsi walivyoliokoa taifa hili basi leo hii wanasiasa wangekuwa wa kwanza kuitetea na kuipa nguvu TISS na si sasa ambapo kila mmoja anajifanya ni mkosoaji na anaijua sana taasisi hiyo.
Najiuliza sana. Hivi ikitokea TISS wakaamua sasa kutekeleza matakwa wanayovikwa na wanasiasa wa upinzani ya kuua, kuteka na kutesa watu, kuna mwanasiasa wa upinzani atasalimika?