Kama TANESCO wamehakiki LUKU basi..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama TANESCO wamehakiki LUKU basi.....

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Columbus, Sep 12, 2012.

 1. Columbus

  Columbus JF-Expert Member

  #1
  Sep 12, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,010
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ikiwa shirika la umeme Tanesco wameamua kuhakiki mita zao za LUKU ili kujua kama mapato sahihi ya umeme kwa wateja basi imefika wakati muafaka kwa sisi wateja kuhakiki vyombo vyetu vinavyotumia umeme majumbani na kuwasilisha Tanesco. Zoezi hili litasaidia kuandaa madai ya fidia kutokana na uharibifu wa vifaa unaoendelea majumbani kutokana na kukatwa katwa kwa umeme unaoendelea mitaani hivi sasa na kusababisha hasara kubwa ikiwemo kuharibika kwa vyakula kwenye mafriji na vifaa vyenyewe kuharibika. Nawasilisha!
   
 2. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Safi sana, tena zamani kulikuwa kuna form unajaza vyombo vyako ulivyonavyo, sijui bado wanatoa hizo form, ngoja nitembelee tovuti yao kama ntazikuta.

  Ahsante kwa wazo zuri.
   
 3. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #3
  Sep 12, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Hawa jamaa hawafai, wao watuibie wao watuwekee LUKU na wao watufundishe namna ya kuchakachua wakishagombana wanatoa SIRI
  Nipeni muda mtaniPM (nimtafute mtaalam) niwapeni maujanja km ilivyo kwa modem za HUAWEI,
  nasikia kuna no. za kuingiza ili kucheck salio km ulichakachua
  zipo no. za ku-pause au kstop Du ngoja nistop na mm
  hiwezekani Mvua zetu, Gasi yetu wenye Symbion hata hawafiki wa3 wanakula hela yetu kiulaini
   
 4. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #4
  Sep 12, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Uzuri wa Tanzania hakuna kuwajibika!! umeme ukikatika sawa, umeme ukharibu vifaa sawa, maji hakuna sawa, huduma za afya na nyinginezo mbovu sawa. Kwa mazoea haya ndiyo maana SSM wanatukanyaga mdomoni!!! Itafika mahali watatuwekea .... na .... mdomoni!!!
   
 5. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #5
  Sep 12, 2012
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Usidanganye watu please téna kwanini hutaki kulipia?

  Ukipause tutakukamata kwenye zero purchase report!
   
 6. A2 P

  A2 P Senior Member

  #6
  Sep 12, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 184
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ukwaju. Hiyo imetulia sanaa nakuaminia kamanda

   
 7. patience96

  patience96 JF-Expert Member

  #7
  Sep 12, 2012
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 1,187
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mmmh PDP inakusubiri wewe!
   
 8. sun wu

  sun wu JF-Expert Member

  #8
  Sep 12, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 0
  Utajuaje kama ame-pause anaiba au ni kwamba amesafiri kwahio kazima vyombo vyake vya umeme au mida hio huwa hayupo nyumbani hence hatumii chombo chochote kwa masaa hayo (kumbe ndio muda anachapa kazi kwa kuchomelea welding na kupigia pasi mtaa mzima)
   
 9. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #9
  Sep 12, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  sawa Mhandisi
  acha nikae na elimu yangu,
  tutakutana kwenye mada ingine kwanini Tanesco mnatoza Bill kubwa kuliko nchi zote na hata zenye maziwa na mito mingi ulimwenguni, kwanini hizi hela wanakula wachache,
  sasa hivi nanunua LUKU kwa Simu na nitawapa wenzangu hizo namba za kugundua balance au bado kosa?
   
Loading...