DOKEZO GE2025 Kama TAKUKURU wameshindwa. basi CCM angalieni hili

DOKEZO GE2025 Kama TAKUKURU wameshindwa. basi CCM angalieni hili

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
A

Anonymous

Guest
Ikiwa kama mustakhabali wa VITI MAALUMU Ndani ya Chama Utaamuliwa Kwa Rushwa tena
Rushwa ya Wazi Wazi basi hadhi ya Uwakilishi wa kundi Hili maalumu hauna faida yeyote Ile kwetu sisi Wanawake.


Hii ni Moja ya ripoti yenye Ukakasi na inayo vunja moyo Kwa Ustawi wa Wanawake Ndani ya Jamii zetu hizi.

Ubunge Una nunuliwa na Vyombo vipo kimyaa, Chama kinazungukwa na Kukikwa Moja ya Nguzo zake bado Tupo kimyaa??!.


TAARIFA JUU YA MUENENDO WA UCHAGUZI NDANI YA CHAMA KWA MKOA WA MBEYA
(VITI MAALUMU
)

Mnamo tarehe 30/07/2025 ilikuwa ni siku ya Uchaguzi Kwa Kura za Maoni Ndani ya Chama

Ambapo tulishuhudia Uchaguzi ukianza Kwa Umakini na Weledi Mkubwa.

Lakini katika hali ya kushangaza kulipatikana taarifa ya Uwepo wa Muenendo usiofaa Kwa Wagombea, Utoaji wa Rushwa na Takrima ya Ugharamiaji Huduma kama vile Upataji wa kifungua kinywa na kiasi cha 70000 Kwa Kila Mjumbe kama salamu toka Kwa Baadhi ya Wagombea.

Hali hii haikuishia hapo Usiku wa kuamkia Uchaguzi uligubikwa na Vitendo viovu vinavyo kiuka Katiba ya Chama chetu Kama Utoaji wa Rushwa

Kwani Baadhi ya Wagombea walifikia hali ya Kutoa kiasi cha Tsh 100000 kama hitaji la Kupigiwa Kura.

Ilifika mahali kukasika Msemo wa "Mwenye laki ndio apewe Kura "

Mara baada ya hapo tunendelea kushuhudia Uingiliwaji wa Siasa za Ndani ya UWT-MBEYA toka Kwa Baadhi ya Viongozi wakubwa wa kitaifa ambao sio tu wanaharibu Jumuia bali wamepelekea Kuondoa Uwakilishi wa Wanawake Bali unaenda kuwa Uwakilishi wa Mtu Kwa mgongo wa Wanawake.


Tujiulize Uwakilishi huu Wa Wanawake Bungeni
Ikiwa utakuwa wa kunuliliwa Utaleta faida gani Kwa Wanawake Wa Mkoa WA Mbeya.?

Tujiulize Uwakilishi huu Wa Wanawake Bungeni ikiwa utawekwa Kwa Mashinikizo ya Viongozi Fulani Tena Kwa upendeleo pasipo kufuata Uwezo na Uhalisia uliopo Utakuwa na Faida gani ???

Ndugu viongozi wakuu tunaomba mushughulilie hili UWT MBEYA inakwenda kufa kutokana na Ubinafsi na tabia za hovyo zenye Kukiuka maadili ya Chama Chetu.

Ndugu viongozi wakuu tunaomba mufuatilie hao watatu wa Juu wameshindaje????

Ndugu viongozi wakuu tunaomba mupime Uwezo na nafasi za Wanawake Wa Mkoa wa Mbeya tunataka nini???

Baadhi ya Viongozi ngazi ya Wilaya na Baadhi ya Wabunge kutoa Maelekezo kuwa Fulani ndie apigiwe kura na Fulani asipigiwe kura, Je kwa wagombea wenye uwezo na hawana watu ambao wapo madarakani ama hawana Ndugu Ndani ya Jumuiya ya UWT Taifa hao watasemewa na nani ngali uwezo wao ni mkubwa.
 
Mimi nasema hivi, ubunge sio sehemu ya kutafuta maisha na kupeleka hoja za kujilimbikia ukwasi bungeni , wabunge wanahitaji kulipwa wao na watoto wao kwa mantiko hiyo.

Mbunge inabidi awe mtoa huduma kwa jamii tu kama kazi Zingine, huta Ona watu wakiacha udaktari ,ualimu kwenda kuwa wabunge.

Watu wanakimbilia bungeni kupeleka hoja za kulinda biashara zao , na kutafuta ufahari tu, Dust
 
Vumilia mkuu, kama ulikuwa hujui basi jua ya kwamba hiyo ndio ccm na huna la kufanya labda uhame nchi, ndio maana mnaambiwa No reform No election.
 
Back
Top Bottom