Mchokoo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2015
- 1,179
- 1,579
Nimewaza sana!
Na acha ninakiri mbele zenu kuwa kwa minyukano hii inayovuka mipaka ya kidemokrasia, sisi kama taifa; tusipoona faida ya mawazo mbadala, kamwe, narudia tena kamwe, tusitegemee kulipeleka taifa hili popote.
Juzi niliwasikia washabiki wa Yanga wakiwaambai wenzao wa Simba kuwa; wako tayari kuwalipia deni yote ile waliloamriwa na fifa kwa madai kuwa watani wao hao wakishushwa daraja; ligi haitakuwa na changamoto.
Sikia watu wa mpira wanavyojua maana ya ushindani.
Ndugu zangu watanzania chonde msiendelee kudanganywa na kudanganyika!
Ni kwamba nchi haiendelei, wala haitatokea iendelea; si kwa sababu ya nyingine yeyote ile, isipokuwa kwa ile ya kuukataa mwendo wa demokrasia unaoanzia kwenye msuguano wa fikra.
Viongozi wetu waliotangulia walikuwa si wabaya kivile lakini hata hivyo nao walikwama kwa sababu ya kukataa kitu kilekile kimoja kiitwacho mwendo wa demokrasia ya msuguano!
Ndugu zangu mara nyingi maendeleo hayaji katika jamii inayowahofu viongozi wao isipokuwa katika viongozi wanaozihofu jamii yao!
Iwapo wananchi watakuwa na mbadala wa chama tawala na kweli wakawa na uwezo wa kufanya mabadiriko ni hakika chama chochote kile kitakachokuwa madarakani kitawahudumia kwa hofu ya kuondolewa kisipofanya hivyo.
Ndiyo maana mimi huwa nasema heri kuwa na bunge la chama kimoja kikatiba kuliko kuwa na bunge la vyama vingi lenye wabunge wachache wa mawazo mbadala na hao wachache wakawa wamedhibitiwa vilivyo!
Najiuliza tena na tena tunalifanya hili na kulishabikia kwa faida ya nani?
Iwapo ccm hawatagundua kuwa wanatakiwa kubaki madarakani kwa utendaji wao na si vinginevyo, basi tusitegemee lolote la maana kutoka kwa wenzetu hawa.
Kwa kulitakia mema taifa hili na si kuwatakia mema wapinzani; kama wengi wao wanavyodhani!
Ni wao wanawajibika kuuandaa na kuuimalisha upinzani nchini ili wao watakapochokwa na wanachi wakae pembeni kama mawazo mbadala.
Na kuwa watakapo kuja katika kambi ya mawazo mbadala watanikuta nawasubiri maana mimi nilishaamua kuwa wa kudumu katika upande huu NASA pale nilipogundua kuwa wote hatuwezi kuwa na mawazo ya upande mmoja.
Tukipevuka na kufikia kiwango hicho, basi ni lazima maendeleo yatapatikana tu!
Maana tutakuwa tumetambua kuwa sisi sote ni ndugu ndani ya boma moja!
Nawasilisha.