Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,270
- 4,470
Tunaimbiwa wimbo wa nchi yetu kuwa na maendeleo ya kila uchwao huku tukisikia taarifa kuwa uchumi unapanda, wengine tukisikia tunajua huenda keki ya Taifa itafika na kwetu angalau tuache kupiga miayo tukiiwaza siku itaishaje baada ya asubuhi na mchana kupita pakavu yaani bila bila.
Cha ajabu ukipata fursa ya kuwaona kwa bahati mbaya wanaotuaminisha juu kuna kazi ngumu sana wanachoka huku wao wakiwa hawataki kabisa kuja huku kwetu wakiwa wananeemeka na keki ya taifa japo wanataka tuamini hali zao ni kama zetu.
Ukiona wakinunua mahitaji yao au kulipa bili zao unabaki kujiuliza hivi kumbe kuna maisha ya hivi watu wanaishi na sisi tunawasindikiza hapahapa, unajikuta unawaza mbona hii pesa anayotumia ni nyingi sana karibu mapato yangu ya miezi 6 yeye anatumia kwa dk kadhaa tena huenda kwenye starehe tu.
Kama vipi wote tuchukue fomu ili nasi tufaidi keki ya taifa kama wao wanavyofaidi maana njia ya kufiia keki si fomu tu, walahi mwakani natia nia nachukua fomu.
Pia soma:Ukiacha Wabunge, kundi jingine linaloila keki ya taifa kisawasawa ni hili hapa