Kama siyo Lema awe nani?

Ingawa siungi mkono hoja, lakini ni dhahiri magamba wanapumua sana na kuzidisha ufisadi wao kutokana na kukosekana kwa mtu kama Dr Slaaa Bungeni. Mbadala wa kuwaumbua watu hawa bado simuoni.
 
Hii hoja niliitarajia, nilikuwa nasubiri tu kuona nani kaianzisha na sababu zake ni zipi.
Hata arumeru visingizio vilikuwa vya namna hii lakini mwisho wa siku arumeru mashariki wamejipatia mbunge bora kabisa na makini.
Kimsingi siungi hoja mkono hata kidogo. Dr. Slaa alishahama huko majimboni na wanachama wenye uwezo mkubwa ni wengi sana kwahiyo ni nafasi yao kuonyesha uwezo.
Mkuu piganieni Lema arudi kwenye nafasi yake! Duh naona Lema kama ananyanyapaliwa
 
Dr. Slaa sio lazima awe bungeni kuwaanika mafisadi anaweza fanya hivyo popote pale, nakubaliana na wajumbe wanaosema hadhi, na majukumu ya dr. Slaa si ubunge tena kwa sasa tunamhitaji aandae mazingira ya cdm kuchukua nchi 2015 or so.
 
hili nimekuwa nikilifikiria sana,sidhani kama akiwa mbunge,atashindwa kuendeleza hayo majukumu mengine,mbona hata mwenyekiti wetu ni mbunge?dr akiingia bungeni CCM wamekwisha maana atakuwa anawasukumia kwenye kifo 2015,mi sioni kama atashindwa kuendeleza majukumu mengine mkumbuke huyu ni dr wa ukweli
 
Hata mimi ningependa sana hawa magamba waabike kwa Lema kuendelea kuwa mbunge wa Arusha, lakini wanasheria wa chama waangalie waone strength and weakness za cdm katika kesi hiyo ili waepuke mapingamizi ambayo hawa jamaa huenda wameyaandaa kuhakikisha wanatimiza nia yao. kwa sababu hiyo mimi naona kama wataona mitego lema afanye kazi ya chama kitaifa zaidi na hapo atakuwa amewapifa bao la kisigino, na hapa akasimamishwa kamanda mwingine ambaye atachukua jimbo kiulaini!!
 
Wapendwa wana jf wa Arusha na Tanzania nzima.Hivi kama Kipenzi chetu Lema akizuiliwa kugombea, Chadema imsimamishe nani? Kwanini tusiwaombe viongozi wa cdm wamsimamishe Bata au Nguruwe halafu tumpitishe kwa ushindi wa kishindo kwa ajili tu ya kuyakomoa magamba? Nawasilisha.
acheni hizi habari bana, magamba wamesha tuudhi sana,
hakuna haja ya kuchezea chanc eyote tunayopata.
hapa ni kuchukua majimbo tu.
weka lema hapo tumpe ushindi wa asilimia 90 hraka.
arudi bungeni halaf mahakamasisiem iaibike na sisiem yenyewe iaibike.
 
Dr Slaa anaweza kuwa mgombea Arusha lakin tumwache ajenge kina Slaa wengine ili kukijenga chama zaidi.Pia mbona pana vijana weng tu wa kugombea jimbo ambao wanaweza.Tusubir tamko la chama leo,ukomboz una gharama zake kwa Lema pambana na uendelee na ujasir wako na pia uendeleze yalo uloyapanga.
 
Watajitokeza wana CCM wengi tu na kutoa ushauri ambao unawa.favour wao
 
ccm itampisha Chitanda!!

Chitanda ni mbunge wa viti maalum sijui katiba inasemaje kwa hilo, ila akimpitisha huyo mama ccm wataonyesha kuwa wanakuja Arusha kushiriki tu sio kushinda!!
 
Back
Top Bottom