Siungi mkono hoja...
Dr Slaa anafanya kazi kubwa sana ya kujenga chama. Hii stability iliyopo CDM kwa sasa ni kazi ya Dr Slaa, ukimuongezea majukumu mengine maana yake kuna mambo yatadorora, hasa kukijenga chama. Pia akigombea mtu mwingine anayekubalika itakuwa imeongeza wigo wa viongozi ndani ya chama. Kumbuka CDM huenda ikachukua nchi 2015 usitegemee akina Zitto na Mnyika kuchukua nafasi zote, lazima chama kiwape nafasi watu wengi zaidi. Hujiulizi kwa nini Dr Slaa anawanyima usingizi magamba? Kwa nini Kichaa Lusinde alikuwa anamtukana zaidi Dr kuliko watu wengine kwenye kampeni?