Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,539
- 4,854
[07:56, 06/01/2016] Idd Ninga: 1)mwenzenu roho ya uma,yote nikifikiria.
Najionea huruma,kwa yote nilotendea.
Sina mbele wala nyuma,nahisi nateketea
Kama siyo serikali,panya rodi nisingewa
2)yapo mengi nayaficha,kukumbuka nachukia
Macho ninayapikicha,tena nisijejonea.
Siju lini niliacha,vyema sizikumbukia.
Kama siyo serikali,panya rodi nisingewa.
3)nchi yetu ni tajiri,kwani sisi masikini
Ni kipi kilitujiri,tukatengwa masikini.
Tena tukiwa na hari,kutoka nayo shuleni.
Kama siyo serikali,panya rodi nisingewa.
4)sasa leo nateseka,nipo humu gerezani.
Wamenifanya mateka,hata mbele mi sioni.
Wapi nitaenda cheka,ama fia gerezani
Kama siyo serikali,panya rodi nisingewa.
5)ni mabaya tulifanya,watu wakakimbizana.
Haki yenu tulibinya,wengi mkaumizana.
Tulikosa cha kufanya,ndo mana tukapigana.
Kama siyo serikali,panya rodi nisingewa.
6)wao hawakutambua,wenyewe walijuana.
Wakajifanya wajua,sisi kudhulumiana.
Nasi bila kujijua,tukaanzisha mchana.
Kama siyo serikali,panya rodi nisongewa.
7)mapesa wanagawana,ikulu hadi bungeni.
Magari wanapeana,hali sisi masikini.
Majirani wanaona,mapesa ya mjengoni
Kama siyo serikali,panya rodi nisingewa.
8)nchi ya kitu kidogo,nitabu kwa masikini.
Hata watoto wadogo,thamani gani shuleni.
Taifa lakuwa mbogo,latutenga ajirani.
Kama siyo serikali,panya rodi nisingewa.
9)wakatunyima ajira,wenyewe wakapeana.
Si tukapoteza dira,mtani tukauana.
Tukawa twapenda mira,mawazo kuumizana..
Kama siyo serikali,panya rodi nisingewa 10)jamani siwezi jua,ni wangapi niliua.
Kuchinja kwangu likua,sijambo la kuchagua.
Kila nilipoamua,panga langu nichukua.
Kama siyo serikali,panya rodi nisingewa.
11)gerezani nimewekwa,nahisi ninaonewa.
Mbona yule hakusekwa,ama mimi nachukiwa.
Ukidhani nipaukwa,akilini ni mkiwa.
Kama siyo serikali,panya rodi nisingewa.
12)naona danu yasema,mizuka inahamka
Inakuja ikihema,na laana yatamka.
Huku yatoa lawama,iso weza kubebeka.
Kama siyo serikali,panya rodi nisingewa.
13)hata kama nikitoka,nahisi nitarejea.
Kushika panga na shoka,riziki jitafutia.
Ila pia nimechoka,natamani kutubia.
kama siyo serikali,panya rodi nisingewa.
14)nahitaji msamaha,kwa yote niloyatenda.
Kweli siioni raha,wapi nitaweza kwenda.
Imenikufa furaha,siisomi kwa kalenda.
Kama siyo serikali,panya rodi nisingewa.
Shairi😛ANYA ROAD.
mtunzi:Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
0765382386
iddyallyninga@gmail.com