Kama serikali hii ni ya masikini na wanyonge,basi itambue hao ndio wanalia njaa,isiwageuke

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
15,095
25,842
Serikali ya awamu ya tano imekuwa ikijinasibu kwamba ni "serikali ya masikini na wanyonge"

Nchi iko kwenye upungufu mkubwa wa chakula,njaa,na ni wazi watu masikini huwa ni wahanga wa baa hili,sitarajii kumsikia Reginald Mengi,Mohamed Dewji,au hata Mkuu wa wilaya akilia njaa.Ni watu masikini wa kutupwa ndio wanatoa kilio.

Cha ajabu,serikali hii inayotamba kulinda maslahi ya masikini NA wanyonge inataka kubadili gia angani pale masikini hawa wanapoomba msaada.

Tunaitaka serikali iwasaidie hawa masikini na wanyonge na umasikini wao isiwe karata ya kutafutia umaarufu wa kisiasa ili kupata kura
 
Wewe umekula leo?
 
Mbona amesema kama mna njaa mnataka akawapikie, Serikali yake haiwezi kutoa msaada wowote wa chakula
 
Wengi tunaotoa maoni tupo maeneo ya miji, katika hali kama hiyo ni ngumu kuelewa huko vijijini hali ikoje, kuna wananchi bank yao ni mazao kingine anauza ili kupata mahitaji mengine kama vile sabuni, mafuta ya taa n.k. kingine anatumia kama chakula sasa hali ilivyo baadhi ya maeneo wameishiwa kabisa hawana cha kuuza wala cha kula nyumbani kwa hiyo hata leo ukipeleka unga ukauza kilo sh 500/- mtu huyo hawezi kununua hivo ningeshauri hawa viongozi wetu wasiangalie masoko ya mjini haya huwa hayakosi chakula yenyewe huwa ni kupanda kwa bei ya vyakula wanaokosa chakula ni hawa wakulima wadogo (peasant) lakini kwa farmers na wafanyakazi hawa wao hulalamika bei zinapopanda tu na sio ukosefu wa chakula, sasa baadhi ya maeneo hawa wakulima wadogo wapo hoi kabisa na hao ndio tunaowasemea, viongozi waende vijijini wasitoe matamko wakiwa mjini wakati hali mbaya huko vijijini, najua baadhi ya maDC wanalijua hili kwani wameshaenda huko vijijini na kuona hali halisi ila wanashindwa kusema sababu wanaogopa kutumbuliwa na si kwamba watu hawakulima wamelima walitegemea vuli wangevuna wamekosa na mwaka jana mavuno hayakuwa mazuri katika maeneo hayo
 
Kweli kabisa
 
Back
Top Bottom