Kama Seif hataki Serikali mbili Ajiuzulu

Kama Seif hataki Serikali mbili Ajiuzulu

ras mkweli

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2012
Posts
280
Reaction score
105
Kama Seif hataki Serikali mbili Ajiuzulu Katibu wa CCM itikadi na uenezi wa CCM Nape Nnauye amemtaka Makamu wa kwanza wa Rais ambaye pia ni katibu Mkuu wa CUF taifa Maalim Seif Sharif Hamad ajiuzulu nafasi hiyo kama hataki Muungano wa Serikali mbili.




kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Magharibi Unguja, bwana Yusufu Mohamedi Yusufu, wakati akiwakaribisha kuhutubia mkutano wa hadhara.

Viongozi wa juu wa chama hicho, wanaoendelea na ziara katika visiwa vya unguja na pemba, ambapo amewatahadharisha watanzania kutokubali hadaa za wanasiasa wenye nia ya kuvunja muungano kwa maslahi yao binafsi.


Akizungumza katika mkutano huo Katibu wa CCM itikadi na uenezi wa CCM Nape Nnauye amemtaka Makamu wa kwanza wa Rais ambaye pia ni katibu Mkuu wa CUF taifa Maalim Seif Sharif Hamad ajiuzulu nafasi hiyo kama hataki Muungano wa Serikali mbili.

Nape amepinga kauli ya katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF aliyodai haina mashiko kufuatia chama cha CUF kudai kuchukua majimbo 18 ya uwakilishi na ubunge katika uchaguzi ujao na kudai kuwa wamejipanga kushinda kwa kishindo katika uchaguzi huo, kauli inayoungwa mkono na katibu mkuu wa chama hicho komredi Abdulrahman Kinana.

Wakihutubia wananchi waliofurika katika uwanja wa Tomondo baadhi ya viongozi wa chama hicho walioambatana na katibu mkuu upande wa Zanzibar wakiwemo wabunge wa bunge la jamuhuri ya mungano wa Tanzania na wawakilishi wa baraza la wawakilishi la serikali ya mapinduzi Zanzibar wamesihi wazanzibar kuipigia kura ya ndiyo katiba iliyopendekezwa muda utakapo wadia.

Chanzo: EATV

 
Wananchi wengi hawataki serikali mbili nao "wajiuzulu"?
 
Mtu mwenye akili zako timamu unatega sikio kumsilkiliza Nape...!!!! Huyuhuyu Vuvuzela la Lumumba???

Aaaaah bora nikacheze bao Jangwani nipoteze Stress......!!!

BACK TANGANYIKA
 
Huyu Nape anamjuwa maalim seif au anasikia sikia tu, ivi Nape anaijuwa Zanzibar au anaota ota tu kama anakaa kwenye viriri na kuanza kuroja roja tu October si mbali. Mara hii Zanzibar ni ama fa imama ccm ishinde kihalali iendelee kutuongoza lakini kama CUF itashinda! kama CUF itashinda! Kama CUF itashinda kutakuwa na habari nyengine katika Visiwa vya Zanzibar.
 
Huyu Nape anamjuwa maalim seif au anasikia sikia tu, ivi Nape anaijuwa Zanzibar au anaota ota tu kama anakaa kwenye viriri na kuanza kuroja roja tu October si mbali. Mara hii Zanzibar ni ama fa imama ccm ishinde kihalali iendelee kutuongoza lakini kama CUF itashinda! kama CUF itashinda! Kama CUF itashinda kutakuwa na habari nyengine katika Visiwa vya Zanzibar.

CUF imeshinda uchaguzi wa Zanzibar mara zote ..hakuna mwaka CCM imewahi kushinda na hilo wanalijua vizuri sana
 
Ukifuatilia Mikutano ya CCM ni dhahiri kwamba wameishiwa na Sera , ni kama wiki sasa Kinana na Nape wapo huku Zanzibar lakini wanapofanya mikutano yao hotuba zao mwanzo mwisho ni Seif weeeeeee, Seif weeeeeeee, Seif weeeeeeeee! Wakiacha kumzungumzia Seif wanaleta msamiati wa CUF. Hawa watu wameishiwa na Sera vichwani mwao
 
Nikiwa mwananchi wa kawaida kama ningekutana na Nape ningemuambia hivi:-
Kama Maalim Seif kakosea, na kama Maalim Seif ni kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na CCM kupitia kwa Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dr Shein; basi mfukuzeni kwenye Serikali yenu. Simple. Vinginevyo kama mtaendelea kulalamika na nyie tutawaona ni walalamishi tu. Katiba ya Zanzibar ilivyobadilishwa mwaka 2010 si ndo nyie mlishangilia? Ndo tuseme mlipigwa chenga ya mwili au? Ni mawili, mfukuzeni kama mnaweza, au mnyamaze muendelee kusikilizia maumivu ya Katiba ya Zanzibar mliyoibadilisha bila kulazimishwa na mtu. CCM vipi jamani?
 
King'ora amuachie nani? Hakuna mtu anayependa foleni tusidanganyane bwana.
 
Huyu Nape anamjuwa maalim seif au anasikia sikia tu, ivi Nape anaijuwa Zanzibar au anaota ota tu kama anakaa kwenye viriri na kuanza kuroja roja tu October si mbali. Mara hii Zanzibar ni ama fa imama ccm ishinde kihalali iendelee kutuongoza lakini kama CUF itashinda! kama CUF itashinda! Kama CUF itashinda kutakuwa na habari nyengine katika Visiwa vya Zanzibar.
Mkuu Maalimu Self alishasema cheo hicho hakupewa na CCM bali katiba ya Zanzibar kupitia sanduku la kura , kwa hiyo hawezi kumwachia fisi bucha watabanana humo humo mpaka kieleweke.
 
Ninavyoelewa Seif ameingia SUK kwa mujibu wa katiba ya nchi ya Zanzibar na siyo katiba ya CCM. Katiba ya Zanzibar inaitambua kama nchi yenye mipaka na dola.
 
Eti Mtanganyika Nape wa CCM anamtaka Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif ajiuzulu?

Kwanini asijiuzulu Rais Shein kwa kutaka serikali mbili? Au makamu wa pili kwa kutaka serikali mbili?

Au ndio mambo ya zidumu fikra za Chenge na Katiba yake?

Je watanzania wengi tuliopendekeza serikali tatu nasi tujiuzulu? Kha!
 
sijawahi kuona kiongozi mpumbavu kama nape hakuna anachokijua zaidi ya kuimba taarabu
 
Hawezi kujiuzulu kwa kuwa kaonja utamu wa kiti,yupo kimaslahi yule.
 
Ccm wanaonyesha kutokomaa ktk siasa hili swala c mmetuachia wananchi Ata ina maana na kula mmesha piga wenyewe
 
Back
Top Bottom