Kama Ruto na Uhuru wa Kenya wamechiwa, ni nani alihusika?

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,815
Nimekuwa nikifwatilia hii kesi iliyokuwa inawakabili Viongozi wa nchi ya Kenya,
Uhuru Kenya na Ruto, kesi ilikuwa ni kwamba walihusika na fujo zilizotokea huko nchini Kenya na kusababisha vifo vya watu wengi na wengine kupoteza mali na makazi!

Sasa hawa wawili wote wameachiwa ina maana hawana kosa yaani hawakuhusika, sasa Je ni nani alihusika?? Kwa maana watu walikufa hivyo ni lazima kuna aliyehusika!

Na hapa ndipo ninapoona usanii wa Wazungu kwamba hii Mahakama (ICC) haiko kwa ajili ya haki bali kwa ajili ya Maslahi ya Wazungu, hapo itakuwa Uhuru Kenya na Ruto wamewaridhisha Wazungu na kuendelea kututumia Waafrika kama kiatu na hivyo kufutiwa kesi, kwa maana haingii akilini kwani lazima mtu ashitakiwe na kuhukumiwa, sasa ni nani huyo wa kushitakiwa?? Uhalifu ulifanyika!
 
Aliyepaswa kuwa hatiani ni yule Mwenyekiti wa Tume Kivuitu (R.I.P) ndio chanzo cha yote yaliyotokea kule Kenya.
 
Nadhani nguvu ya umoja wa viongozi wa Africa kujilinda imewatisha ICC, wamehofu kupoteza legitimacy.

Hata hivyo ushahidi ulikosekana
 
Daah ni bora demokrasia ya ulaya kuliko ya afriCa n u-popo tu yani jamaa kiuraisii wee kaachiwa but ipo siku zile nafsi zilizopotea kwa haki zitanena na atakuwa mashakani tena# life does on#viva mandela ur my first black president holaaa..!
 
Hawajaachwa huru kwa eti kutohusika ila USHAHIDI umekosekana/haujitoshelezi/ wa kuwatia hatiani.
 
Hawajaachwa huru kwa eti kutohusika ila USHAHIDI umekosekana/haujitoshelezi/ wa kuwatia hatiani.

Sasa maana yake nini? Kama hakuna ushahidi maana yake ni kwamba hawana hatia, yaani hawajahusika hiyo ndiyo maana yake, na kama hawajahusika sasa ni nani alihusika? Kwa maana watu walikufa!
 
Sasa maana yake nini? Kama hakuna ushahidi maana yake ni kwamba hawana hatia, yaani hawajahusika hiyo ndiyo maana yake, na kama hawajahusika sasa ni nani alihusika? Kwa maana watu walikufa!

Kukosekana kwa ushahidi na kutokuwa na hatia vitu 2 tofauti. Wanasheria watatusaidia zaidi.

Mahakama imesema baadhi ya mashahidi waliogopa kutoa ushahidi au waligoma kabisa au walitoa ushahidi dhaifu kabisa ambao hautoshi kumtia mtu hatiani. Kwa maana nyingine ukipatiaka ushahidi mwingine, mbona akina Ruto bado wanalo
 
Sidhani kama unahitaji kuwa Mwanasheria kujua kwamba kama umefikishwa Mahakamani na Mahakama ikashindwa kukushitaki kwa kuwa hakuna ushahidi dhidi yako na kukuachia huru, basi wewe ni kwamba hauna hatia ni rahisi kihivyo tu, kwa maana kama ungekuwa nayo wasingekuachia, vipi kama wewe ni mtu mbaya na muuwaji ukirudi uraiani na ukaua tena???
 
Hivi hii kesi bila Mwai Kibaki na Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ambaye alikili wazi kulazimishwa kutangaza matokeo mimi sikuona kama ingekuwa fair, Uchaguzi wa Kenya 2007 unafanana na kilichotokea Zbar.
 
Back
Top Bottom