*🪰Kama Nzi Hakai Juu ya Nyama Usinunue!*

*🪰Kama Nzi Hakai Juu ya Nyama Usinunue!*

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
4,780
Reaction score
8,155
Kuna hekima ya kiafrika inayosema:
"Kama nzi hawagusii nyama, basi kuna jambo."

⚠️ Usinunue nyama ambayo hata nzi hawavutiwi nayo. Inawezekana imewekewa kemikali, imechakachuliwa au haifai kwa matumizi ya binadamu. Nzi, ingawa ni wadudu, huwa na hisia kali sana za harufu wakikataa, jiulize kwa nini.

🟢 Vivyo hivyo kwenye mboga za majani kama:
  • Sukuma wiki
  • Mchicha
  • Mnavu
  • Figiri
  • Chinese

Kama mboga hizi hazina tundu hata moja au haziliwi na wadudu usichume!
Wadudu ni viumbe wa asili na kama hawali hiyo mboga, kuna uwezekano mkubwa kuwa imepuliziwa sumu au kemikali kali isiyofaa.

Kumbuka:
Chakula salama ni kile ambacho hata viumbe wa asili huweza kula.

Share ili na wengine wajifunze kula kwa usahihi na afya!
 
Unafahamu vimiguu ya nzii vinabeba mpaka chembechembe za nnyaa?
Mleta mada yupo sahihi na kaifikisha mada vizuri ila hajatoa ufafanuzi wa kidaktari/kitaalamu.

Iko hivi;

Kuna chemical inaitwa formalin ambayo ndiyo hutumika kuweka maiti mochwari isiharibike.

Kemikali hii hutumiwa na hawa wafanya biashara kwa ajili ya kuhifadhi minofu kama nyama na samaki. (Hii kesi iliwahi kutokea Mwanza kulalamikiwa kuwa samaki wanaweka kemikali za kuholifadhia maiti ili wasiharibike...Ndiyo hii formalin.)

Ukienda buchani ambako kunapatikana nyama,katika hali ya kawaida wadudu kama nzi walitakiwa waoneakane kwa sababu ya kuvutiwa na harufu ya nyama. But,kinyume chake unakutana na mabucha yakiwa masafi hakuna hata nzi mmoja hata kama milango ipo wazi muda wote. Ndiyo connection ya huu Uzi ulipo ambapo mleta mada The redemeer ameelezea.

Kuhusu mboga mboga ni the same.

Kinachopendwa na wadudu maana yake ni salama kwa kuliwa. Ndiyo mana tunashauri watu walime mboga nyumbani na muweke mbolea organic badala ya mbolea za viwandani kama UREA,CAN nk. Lakini pia Kuna madawa ya kuua wadudu na makemikali mengine (busters) kwa ajili ya kukuza mbogamboga. Unakuta mboga inapendeza shambani hadi unatamani uipeleke maonyesho...Hiyo kiafya haifai ila ndiyo tunakula tutafanyaje maana yake imekolea kemikali hadi wadudu wanaiogopa kuisogelea na wengine kufa.
-------------------------------------

Kuna movie ya kizungu niliangalia siku Moja,jamaa mlima tufaa(apples 🍏 ) alikuwa anafanyiwa figisu sokoni kwa sababu maepple yake Yana madoa na hayavutii kama ya wengi sokoni ambao wanafuata taratibu za afya na soko kuweka mbolea na dawa za kuua wadudu.

Jamaa alitembelewa na wanunuzi wa kimataifa siku Moja shambani kwake na kuwapa somo/darasa juu ya ulimaji wake.. kifupi jamaa alikuwa haweki mbolea Wala kemikali yoyote ya sumu na ndiyo maana matunda yake yalikuwa yanashambuliwa na wadudu.

Baada ya wanunuzi kusikia hivyo walikuwa wananunua bei mara tatu ya matunda ya wenzie hadi wenzake wakasema wewe mchawi unauza matunda mabovu lakini bei ipo juu kutuzidi ..Yeah ni movie na Ina mambo mengi ndani yake. Hiki kipande ilikuwa context tu ya huu Uzi.
 
Back
Top Bottom