Stephen Ngalya Chelu
JF-Expert Member
- Oct 31, 2017
- 8,288
- 18,579
Walinipenda kwa dhati kabisa kutoka ndani ya mioyo yao. Niliwapitisha katika milima na mabonde makali lakini bado walibaki. Na nyakati ambazo uvumilivu uliwashinnda na kuamua kuondoka, hawakusita kurudi kwa moyo mmoja nilipoonyesha majuto ya kweli.
Wanafanana vitu vingi mno; mawazo, mitazamo, tabia, rangi mpaka majina. Ni mapacha waliozaliwa katika familia tofauti. Ingekuwa vyema kama wangeishi nyumba moja pamoja nami.
Wamenisaidia kufungua akili yangu katika mambo mengi katika maisha kwa ujumla. Ni watu ambao nahisi kuwa karibu nao katika kipindi chote cha maisha yangu, kama wake zangu.
Ila nitawezaje,
Wakati dini yangu imeharamisha ndoa ya mke zaidi ya mmoja?
Nitawezaje.
Wakati uchumi wangu hauruhusu kuweza kuwamudu wote wawili? (hata mmoja kwa mbinde)
Nitawezaje,
Wakati wao wenyewe hawakubali ndoa ya mke zaidi ya mmoja?
Nitawezaje,
Wakati jamii ina mtazamo hasi kuhusu ndoa za wake wengi?
Nitawezaje,
Wakati wataalamu wa afya wanadai kuwa ndoa za wake wengi zinachochea kuenezwa kwa magonjwa ya zina?
Nitawezaje,
Wakati ndoa za ya mke mmoja zina mitikisiko mikubwa, je vipi kuhusu ndoa yagu ya wake wawili?
Nitawezaje,
Wakati shughuli zangu za kila siku zinanifanya nikose muda wa kutosha kuhudumu vyema katika mahusiano yangu?
Nitawezaje,
Wakati mimi mwenyewe nayahofia hayo niliyataja hapo juu?
Nitawezaje?
It was always me versus the world until I found it is me versus me.
ONLY IF YOU KNOW WHAT I MEAN.