Kama ningekuwa sina kazi, sina pesa, ningefanya hivi nipate pesa

tatizo email zimejaa matapeli wa kinigeria

Wewe si mnaijeria.

Email marketing maana yake ni kuunda long term relationship na mteja na si kukurupuka.

Pia kila anayeamua kuingia “subscribe” kwenye list yako amefanya hivyo kwasababu yopo Interested na product au huduma unayotoa.
 
Ndiyo mkuu karibu.

Unajua inafika kipindi wateja wanaongezeka huwezi tena kuendesha Business kwakutumia Whatsapp kwasababu utashindwa kuwa organized na hivyo business itashindwa kukuwa.

Huu ni mtego biashara nyingi hizi ndogo zinakwama.

Cheers
Sawa boss.
Ukinifundisha nitashukuru
 
Wewe si mnaijeria.

Email marketing maana yake ni kuunda long term relationship na mteja na si kukurupuka.

Pia kila anayeamua kuingia “subscribe” kwenye list yako amefanya hivyo kwasababu yopo Interested na product au huduma unayotoa.
GLOBAL CITIZEN....una nondo/idea nzur xana lakin uko very tricky kwnye kuandika (NOTE; Nimeshasoma bussiness thread zako nying)......i think this is one of strategies kuendelea kujinufaisha......ss bas punguzaa technical language na vocabularies nyingi.......wasiojua kabsaa wakuelewe....mfano hyo email marketing; jins ya kuitengeneza had kuitumia step by step.....

Shukran pia kwa motivations......
 
Ml
Mkuu, Emails tunatumia kufanya kitu kinaitwa “retargeting” kwenye matangazo ya Facebook.

Ndiyo maana tunasema ni ASSET.

Msome mdau #12

Hii ni advanced feature ukitumia kwenye hako ka “Online Business” kako utashangaa jinsi itakavyo scale up”

Nimetumia sana Whatsapp Business lakini kadiri business inavyokuwa huwezi ku-hundle potential clients individually.

Hapa ndipo email marketing inaingia.

Kwa mfano mimi nina subscribers kwenye Email list yangu zaidi ya 8000+.

Hawa potential clients utaweza vipi ku-hundle relationship kwamaana ya kuwasiliana nao wote usiwapoteze?

Jibu ni Email marketing.

Kwenye Email marketing ninauwezo wakufanya automation. Yaani ninauwezo wakuweka series of Email ambazo zinakuweza kumshawishi kila mteja kati ya hawa 8000+ hadi kufikia hatua ya kunnua bidhaa bila mimi kufanya chochote.

Najua unasema duuuh

Ndiyo hivyo mkuu, wewe endelea kujifunza taratibu tu.

Cheers
Mleta mada upo sahihi.

Ila si kila bidhaa au biashara email inaweza kuwa na tija. Na kwa watanzania(natives) suala la email sio sana kama wenzetu wageni.

Kwenye uzi wako umesema unadeal na real estate ambapo umesema wateja wako ni watu kutoka nje, kwako email it is the things. Ila kwetu sisi tunaodeal na local market njia nyingine kwetu ni sawa kabisa.

Suala la kutuma jumbe automatic hata whatsapp lipo mbona.
 
what about website mkuu, lakini pia business yoyote inaangalia unafanya biashara na nani.
kwa nini hapa Tanzania wengi hawako active kwenye emails?
kama hawako active how can you do with emails upate wateja.
 
Amesema vizuri, Tatizo nyie mnasoma documents mtandaoni zilizoandikwa mazingira ya Nje, mnataka mtumie kutemgeneza pesa hapa kwenye utamaduni wa maduka ya kina Mangi. Yupo sahihi, wewe mwenyee unalitambua hili unauhakika unatengeneza pesa kupitia njia hii? Labda kwa mafundisho unayotoa
 
Kuwa mkweli katika haya ipi inakutengenezea pesa mda huu, au ni menda?
Wakuu,

Kwa dhati kabisa niseme pesa zipo nyingi sana kama utafahamu tu namna yakuzipata.

Ngoja nikwambie kitu.

Kwa muda mrefu nimekuwa nikichunguza na kujaribu mbinu tofauti zakuanzisha biashara hasahasa Online kwakutumia mtaji mdogo kabisa au kutotumia pesa kabisa na mwisho wa siku kufanikiwa katika biashara ninayofanya. Niseme wazi kuweza kuanzisha business ya namna hii inahitaji kuwa strategic kwamaana ya kwamba ukianza hizi business basi unafahamu goal yako ni nini. Hii inakuwa rahisi kufikia goals zako kwa haraka.

Kwa maana hiyo basi nataka nikupatie step by step process jinsi unavyoweza kuanzisha side hustle sehemu yoyote ulipo na kuanza kutengeneza pesa hata kama huna kumi mfukoni ilimradi tu uwe na access ya internet.

Kabla sijaanza nataka nikuonyeshe maana ya pesa ili iwe rahisi kukubaliana hapa vinginevyo unaweza usinielewe. Nataka niweke hili sawa kwasababu watu wengi wamekuwa na mawazo siyo kabisa kuhusu pesa . Hii hali inasababisha watu wengi kushindwa kuona huu “mtego” ninaoenda kukuonyesha hapo chini.

Sasa niseme pesa ni nini?

Pesa maana yake ni chochote kile kinachofanikisha exchange of VALUE.

Nimeweka Value kwa herufi kubwa kwasababu ndiyo msingi wa wewe kuanza kuelewa pesa ni nini hasa.

Ukiwa unataka kupata pesa inabidi ubadili vile unavyoiwazia pesa. Inabidi uione pesa ni exchange of value kwamaana ya kwamba kama unauwezo wakutoa value kwenye jambo lolote lile basi mtu wangu soon utapata pesa.

Kama wewe hakuna VALUE yoyote unayoweza kutoa hiyo maana yake wewe ni valueless kwahiyo pesa utaiona kwenye picha tu.

Value maana yake ni uwezo wakufanya chochote kile kinachoongeza ustawi katika maisha ya watu au biashara.

Kama Wewe unafahamu kuuza kwa mfano, na ukanipatia mimi customer atakayenunua bidhaa nayouza hiyo maana yake umetoa value. Watu wengi wanachanganya vyeti na uwezo wakutoa value ndiyo maana inakuwa ngumu kupata kazi au pesa sehemu yoyote ile. Kama unapitia hili tatizo unahitaji usaidizi my friend.

Alright,

Sasa tuanze hatua ya kwanza kabisa kama ningekuwa sina pesa, nimepigika aka broke. Je, ningfanya nini?

1 • Kujifunza kushawishi + kuuza

Jambo la kwanza kabisa ningeingia YouTube au ningetafuta mtu yeyote mwenye weledi katika eneo hili anipige brush je nijiweke namna gani niweze kuwa na ushawishi zaidi ninapojaribu kumuuzia mteja bidhaa au huduma? Je, nitawezaje ku close deals nyingi ninapowasiliana na clients kuliko ninazokataliwa?

Nitahakikisha najinoa kwenye haya maeneo mawili ya USHAWISHI NA KUUZA na nitaanza kufanyia kazi kila nalojifunza kwakujaribu kuuza vitu vilivyo ghetto lakini situmii. Haitajalisha watu watanunua au vipi. Lengo langu hapa nataka nipata ile experience yakukataliwa au kukubaliwa ili niwe na confidence zaidi kwasababu lengo langu ni kupata pesa kidogo hapa mwanzo + confidence.

Nitaweza kuuza chochote nilichonacho kwakutimia JF au Kupatana, Instagram, Facebook etc.

Ok tuendelee...

Unajua persuation kwenye kuuza ni muhimu sana kwasababu watu wengi huwa hawatoi pesa bila kushawishiwa.

Na ili uweze kuwa mbobezi katika skill hii muhimi kabisa ya ushawishi basi inabidi utape real experience na si vinginevyo.

This skill alone will make you millions.


2 • Nitatafuta wafanyabiashara wenye kumiliki real estate (lodges, nyumba za kupanga/apartments etc) na kuonge nao.

Hatua ya pili sasa ni kuupgrade my game ili nianze kutengeneza pesa yakueleweka kwasababu mbinu ya kwanza ya kuuza chochote nisichokitumia ghetto si sustainable.

Hapa nitajikita “kuwawinda” wafanyabiashara wa business nilizotaja hapo juu na kuwaeleza iwapo wapo tayari nikiwalete wateja iwe kwenye lodge, apartments wanazopangisha, commercial buildings etc na wao kunilipa commissions. Hata kama sijawahi kuuza real estate nitawapiga sound kwasababu sina chakupoteza lakini wapo pia hawana cha kupoteza na ninafahamu wafanyabiashara wengi wanapenda sana ukiwambia unawaletea wateja.

Nitahakikisha wafanyabiashara wote ninapata email zao kwasababu huu ni mtaji kwa baadaye. Nitakuonyesha ni kwa jinsi gani.

Baada ya wafanyiashara kadhaa kunipatia go ahead sasa nitaanza rasmi kazi ya kuuza. Nitatumia Internet kuweka matangazo yangu na kwasababu kuna njia nyingi za bure kama vile kutangaza hapa JF site inayotembelewa na thousands of visitors daily. Hii ni opportunity kubwa sana kufikia pontential customers kwa hapa Tz.

Nikianza kuingiza pesa kwa kila mpangaji nayempeleka kwa hawa Businessmen ninaowasaidia kuwapatia wateja, sasa nitakuwa nimeanza kuwa expert na ninafahamu watu wengi watakuwa wananitafuta kwakutumia number ya simu au email kwaajili ya kupata nyumba, lodge au apartment kwahiyo hawa wateja ni muhimu kuendelea kuwa nao. Na mbinu yakuweza kuendelea kuwa na mahusianao mazuri nao ni kutumia email marketing ndiyo maana nitahakikisha napata email ya yoyote yule anayehitaji au atakayehitaji huduma nayotoa.


3 • Nitaanza kuunda Email list kwaajili ya Email marketing.

Email marketing ni powerful.

Pengine zaidi ya neno lenyewe powerful.

Email marketing inauwezo wakubadilisha potential customers kuwa paying customers.

Unajua mara nyingi sana tunashindwa kuuza kwasababu tu unakuta mfanyabiashara amejaribu kumshawishi mteja mara moja sasa mteja asiponunua unamuachia. You are doing big mistake my friend.

Huyu mteja ungeweza kumpata iwapo ungetumia mbinu hii ya email marketing ninayokufahamisha.

Kwa wasio fahamu, Email Marketing maana yake ni kutumia email software kuwasiliana na watu wote walio sibscribe katika list yako. Hii njia ni amazing kwasababu inasaidia sana kujenga trust. Sasa na kama ujuavyo potential customers wakikuamini basi hapo utakatengeneza pesa kwasababu watakuwa tayari kutoa pesa.

Ok, niendelee.....hapa kwenye kuunda Email list maana yake nitahakikisha ninakusanya Email za kila mtu aliye interested na na real estate, awe mtu anayetafuta chumba cha kupanga, anataka kununua nyumba etc. Hawa subscribers kila wiki nitakuwa nawatumia Email zakuwafahamisha deals au offer mpya.

My friend kama upo na idadi kubwa kwneye email list yako basi utatengeneza pesa hadi utajicheka kwanini ulikuwa unashindwa kutengeneza pesa kwakukosa maarifa. Trust me on this. Ukitaka ninaweza kukufahamisha zaidi. Just send me message.

4 • Nitatumia same technique number mbili na number tatu kuanzisha biashara nyingine. Na biashara hii nitakayoanzisha this time ni digital marketing.

Kwasababu nimeweza kufanikiwa kwenye real estate na nimefahamu mbinu zakutumia Email Marketing kushawishi wateja sasa basi nitajitanua zaidi kwakuanza kutafuta wafanyabiashara katika maeneo mengine ili niwasaidie kwenye marketing & sales mtandaoni. Hapa nitakachofanya nikutafuta team. Si lazima nifahamu au nifanye kila kitu mwenyewe.

Kama nilivyosema skill muhimu kabisa nitakayokuwa naitegemea ni PERSUASSION kwahiyo kazi kama vile Kutengeneza Facebook Ads au mambo mengine yote ya kiteknolojia nitakuwa nawapatia team yangu.

Kufikia hapa sasa nitakiwa na leverage experience kupata watu au biashara zakufanya nazo kazi mpya lakini pia nitakuwa naendelea kukuza Email list yangu. Na ikitokea nimefikisha subscibers let say 50,000 hiyo maana yake mimi nina “soko” langu binafsi na ninaweza kutengeneza pesa nyingi bila kikwazo au kutengemea platform nyingine mfano JamiiForums au Facebook au Google Advertising. Baada ya hapa nitaendelea kutumia same techniques kuendelea kukuza Business zangu 10X.

Yes, ni hayo kwa leo na ninaomba niishie hapa.

Cheers
 
Mi naamini mwisho wa siku kila mmoja ana njia yake ya kupata pesa, kupata wateja kulingana na mazingira ya kazi yake. So kinacho mfaa A kinaweza kisimfae B kikamfaa C, kikubwa linda wateja wako kwa namna yoyote ile. Nimeshuhudia watu wanasio na elimu ya kusoma na kuandika tena ya ata la 6 ila wanaweza kuuza na kukuza wateja. Ebu fikiri kizazi cha baba zetu au babu zetu waliwezq vipi ku run biashara zao .

Kumbuka hakuna kitu rahisi changamoto zipo hakuna kukata tamaaa
 
Mi naamini mwisho wa siku kila mmoja ana njia yake ya kupata pesa, kupata wateja kulingana na mazingira ya kazi yake. So kinacho mfaa A kinaweza kisimfae B kikamfaa C, kikubwa linda wateja wako kwa namna yoyote ile. Nimeshuhudia watu wanasio na elimu ya kusoma na kuandika tena ya ata la 6 ila wanaweza kuuza na kukuza wateja. Ebu fikiri kizazi cha baba zetu au babu zetu waliwezq vipi ku run biashara zao .

Kumbuka hakuna kitu rahisi changamoto zipo hakuna kukata tamaaa
Mhh hebu jaribu uone
 
Kuwa mkweli katika haya ipi inakutengenezea pesa mda huu, au ni menda?
Bro ulichokisema mm nilianza kufanya 2015 nikiwa diploma ya IT,Nikawa natafuta wateja wanao hitaji magari kutoka nje nikatafuta mawasiliano na wauzaji wa magari japani nikapata kama sita saivi hii nikazi rasmi na ofisi nikafungua tunaagiza magari kutoka nje kwa bei poa kabsa huna haja ya kwenda showroom unakuta kuna increment ya 2mil to 6mil inategemea na gari .ALL IN ALL INAWEZEKANA KIKUBWA HUAMINIFU
 
Back
Top Bottom